Unabii wa Miaka 2300💚
✔✔✔✔✔✔💚Daniel 8:13, 14…. 13, Ndipo niamsikia mtakatifu mmoja akinena na mtakatifu mwingine akamuuliza huyo aliyenena, Haya maono katika habari sadaka ya kuteketezwa ya daima, na lile kosa lifanyalo ukiwa, yataendelea hata lin, kukanyagisha patakatifu na jeshi? 14, Akamwambia, Hata nyakati za jioni asubuhi elfu mbili na mia tatu; ndipo patakatifu patakapotakaswa.
Ni katika kipindi cha utawala wa Belshaza mfalme wa Babeli mwana wa mfalme Nebukadneza (Daniel 5:2) ndipo Daniel anaoneshwa maono haya Daniel 8:1 Katika mwaka wa tatu wa kumiliki kwake mfalme Belshaza maono yalinitokea mimi, naam, mimi Danieli, baada ya yaliyonitokeahapo kwanza. Akiwa katika wilaya ya Elimu, shushani ngomeni katika mto ulai huko Babeli
Mwanzo wa njozi ya Danieli anaoneshwa kondoo mwenye pembe mbili akisimama na kutawala dunia akisukuma upande wa magharibi na kaskazini na kusini (Daniel 8:3, 4). Kisha anaona beberu akiinuka upande wa mashariki akiwa na pembe mashuhuri kati ya macho (Daniel 8:5). (kwa faida ya msomaji pembe katika unabii huwakilisha ufalme au utawala). Akamkaribia Yule kondoo akamkasirikia kwa ghadhabu nyingi naye akampiga hata kuvunja pembe zake, akamwangusha chini hata kumkanyaga-kanyaga
Baadaye ile pembe ikavunjika kwa kujitukuza hata zikatokea pembe nne zikaielekea pepo nne za mbingu nazo zikatwala kwa kipindi Fulani (Daniel 8:8). Daniel 8:9 Na katika moja ya hizo pembe ilitokea pembe ndogo, iliyokuwa sana, upande wa kusini, na upande wa magharibina upande wan chi ya uzuri. Pia katika fungu la 23; Na wakati wa mwisho wa ufalme wao, wakosao watakapotimia, mfalme mwenye uso mkali, afahamuye mafumbo………atasimama. Hii humaaniasha wakati wa mwisho wa utawala wa falme nne zilizoinuka kutoka kwa Yule beberu ndipo utainuka tena ufalme mwingine unaowakilishwa na pembe ndogo, mfalme mwenye uso mkali, afahamuye mafumbo.
Daniel 8:10-14 Nayo ikakua, kiasi cha kulifikilia jeshi la mbinguni ; ikaangusha chini baadhi ya jeshi lile, na nyota ikazikanyaga. Naam ikajitukuza hata juu ya aliye mkuu wa jeshi hilo, ikamwondolea sadaka ya kuteketezwa ya daima, na mahali pa patakatifu pake pakaangushwa chini. Na jeshi likatolewa kwake pamoja na sadaka ya kuteketezwa ya daima, kwa sababu ya makosa; nayo ikaangusha kweli hata chini; ikatenda ilivyopenda, na kufanikiwa. Ndipo niamsikia mtakatifu mmoja akinena na mtakatifu mwingine akamuuliza huyo aliyenena, Haya maono katika habari sadaka ya kuteketezwa ya daima, na lile kosa lifanyalo ukiwa, yataendelea hata lin, kukanyagisha patakatifu na jeshi? Akamwambia, Hata nyakati za jioni asubuhi elfu mbili na mia tatu; ndipo patakatifu patakapotakaswa.
Kuinuka kwa pembe hii ndogo na matendo yake ndiko kunamhuzunisha mtakatifu mmoja na hivyo inampelekea kutaka kujua hatima ya haya yote. Nayo ni nyakati za jioni na asubuhi elfu mbili na mia tatu (2300).
Nini✔✔✅✅ tafsiri yake miaka hii 2300??
Katika sura ya Daniel 8:14 tunaambiwa matukio haya yatachukua muda nyakati za jioni na asubuhi 2300 lakini hatuambiwi chochote kuhusu mwanzo wala mwisho wake.
Katik♿ kuelewa tafsiri hii lazima tuelewe mambo yafuatayo.
nyakati za jioni na asubuhi ni sawa na siku nzima amabyo pia huanza jioni hata jioni. Mwanzo 1:5………… ikawa jioni ikawa asubuhi, siku moja. kwahiyo nyakati za jioni na asubuhi 2300 ni sawa na siku kamili 2300
Katika unabii siku moja ni sawa na mwaka mmoja Ezekiel 4:6………siku arobaini, siku moja kwa mwaka mmoja, nimekuagiza kwahiyo siku 2300 za kiunabii ni sawa na miaka iliyokamilika 2300.. Hivyo tunasema ili haya yote yafikie mwisho ni mpaka kukamilika kwa miaka 2300.
Unabii wa miaka 2300 ndio unabii mrefu kwenye biblia kuliko mengine yote, hivyo unabii mwingine kama vile miaka 1260, majuma 70, miaka 1335 na 1290 zote huangukia kwenye miaka 2300.
Mwanzo♐♐♐♐♐ wa miaka hii ni upi?💯💯💯
Mwanzo wa miaka hii tunaelewa kwa kuelewa mianzo ya majuma 70 katika Daniel 9:24. Muda wa majuma sabini umeamriwa juu ya watu wako, na juu ya mji wako mtakatifu………,25 Basi ujue na kufahamu, ya kuwa tangu kuwekwa amri ya kutengeneza na kujenga upya mji wa Yerusalemu….. kutakuwa na majuma saba………….
💚💚💚Majuma sabini ni sawa na miaka 490. 70×7=490. Hii hutuambia kuwa kulikuwa na miaka 490 ulioamriwa juu ya taifa la Israeli.
Amri juu ya ujenzi wa mji wa yerusalemu ulitolewa na mfalme Artashasta mfalme wa uajemi mnamo mwaka wa 457 K.K (kabla ya kristo) Ezra 7:21-26 Na mimi, naam mimi, mfalme Artashasta, nawapa amri wote wenye kutunza hazina…..hata kiasi cha cha talanta mia za fedha …. kila neon litakaloamriwa na Mungu wa mbinguni, na litendeke halisi kwa ajili ya ya nyumba ya Mungu wa mbinguni…….. Kuanzia mwaka wa 457 hitimisho la miaka 490 au majuma 70 hufikia 34 B.K (baada ya Kristo), (kumbuka kuna mwaka kutoka 0-1)….katika miaka 2300 baada ya kukamilika kwa miaka 490 tunasalia na miaka 1810.
490+1810=2300.na
Siku 2300 zilioneka kuanza wakati amri ya Artashasta kwa ajili ya urejeshwaji wa na ujenzi wa Yerusalemu ilipotolewa majira ya kipupwe ya mwaka 457 K.K. Kwahiyo mwanzo wa miaka 2300 ni mwaka 457 B.K na huishia mwaka 1844 B.K.
Somo hili limeandaliwa na mwinjilisti Peter nakuletwa na Chuminames.
Ubarikiwe kwa kujifunza.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni