Jumanne, 23 Oktoba 2018

*JEE NYAMA YA NGURUWE (KITI MOTO) NI SALAMA KWA BINADAMU???*

Ona.

Hapa huwa kuna mvutano wa kidini sana juu ya nguruwe, Ila Leo napenda kuliweka sawa, kitaalamu kwa mujibu wa *MEDICINE (Science)!!*

Nguruwe ni mnyama anaeliwa na 38% ya watu wote duniani  Na walaji wake ni nchi Magharibi na Kusini mwa Asia, Europe, Sub-Saharan Africa, America ya kaskazini , kusini mwa America, na Oceania.

Nguruwe ni mnyama ambae, Ana umbo la pekee sana, tukiangalia kuhusu madhara yake au faida yake , tunangalia vitu vinavyopatikana ktk mwili wake, tukilinganisha Na Faida.

*FAIDA ZA NYAMA YA NGURUWE KITAALAMU*
👉🏾Kunapatikna vitamini muhimu ktk mwili Wa binadamu; ambavyo ni B1, B6 and B12
👉🏾Unapata madini ya Chuma, ambayo husaidia kuimarisha mifupa.
👉🏾Nyama ya nguruwe inaimarisha ngozi yako Na kuifanya iwe laini.
👉🏾Nyama ya nguruwe ina magnesium kwa wingi ambayo ina faida ktk mwili Wa binadamu
👉🏾Nyama ya nguruwe ina protein ya kutosha, ambayo husaidia ulinzi wa mwili
👉🏾Nyama ya nguruwe ina mafuta ambayo hutupa nguvu mwilini

*HASARA YA NYAMA YA NGURUWE*
Licha ya faida tajwa hapo juu, vile vile kuna hasara ya kutumia nyama hii.
👉🏾Nyama ya nguruwe ; ina sumu ya *carcinogen* ambayo inasababisha kansa; kwa mujibu wa utafiti uliofanyika Na shirika la afya duniani ( *WHO*), Na *The International Agency for Research on Cancer!!* Utafiti huo ukaonesha kuwa ukila kila siku 50gms basi uwezekano Wa wewe kupata kansa unaongezeka kwa 18%
👉🏾Anasababisha Swine Flu kwa binadamu; hivi ni virusi vinavyosababisha mafua kwa binaadamu. Kwa mujibu wa utafiti uliofanyika na *Centers for Disease Control and Prevention* inaonesha influenza virus H1N1 na H3N2 ambaye anatokana Na Nguruwe(kiti moto) imeripotiwa kusababisha maradhi ya mripuko kwa nchi za *MAREKANI*
👉🏾Nyama ya nguruwe ina minyoo wajulilanao kwa jina la trichinella worm , ambao wadudu hawa ni vigumu sana kuweza kufa kwa joto Hata la 100C , utafiti uliofanyika 1998 Na WHO ukaonesha nyama ya Nguruwe iliopikwa kwa Joto la 104C , Huwa asilimia 52.37% ya trichinella worm wanabaki kuwa hai!! Wadudu hao wakiingia ktk mwili Wa binadamu husababisha ugonjwa ujulikanao kwa jina la trichinosis; *ambao huwa Na dalili kama ifuatavyo:*
✅Homa kali sana
✅Kichwa kuuma
✅Kukosa nguvu
✅Maumivu ya nyama za mwili
✅Macho kuwa rangi ya pink(conjunctivitis)
✅Kuvimba uso Na kope
✅Kudhuriwa Na mwanga
👉🏾Nyama ya nguruwe ina virus aina ya Hepatitis E virus (HEV); ambaye husababisha homa ya ini aina E
👉🏾Wadudu wengine ni kama;
🥄Nipah virus
🥄Menangle virus
🥄Viruses Ktk kundi Paramyxoviridae
Ambao wote hao; huwa wanaleta madhara kwa mwili Wa binadamu!!
👉🏾Nyama ya nguruwe husababisha Maradhi ambayo Yana resistance(ukinzani) Na *ANTIBIOTICS*
👉🏾Nyama ya nguruwe ina minyoo aina ya Taenia solium. Kwa mujibu ya shirika la Afya duniani(WHO) - Reference....open_http://www.who.int/news-room/fact-sheets/detail/taeniasis-cysticercosis
Wanasema; minyoo hii huwa;
👉Unaweza kuipata ikiwa hautapika nyama vizuri au Ukila nyama ya kuruwe ilioathirika(infected): Kwa hyo sio kila nyama ya Nguruwe iliopikwa vizuri, huwezi kupata minyoo hii.
👉Minyoo hii ikiingia ktk mwili Wa binadamu husababisha matatizo ya mfumo Wa fahamu (central nervous system) iitwayo neurocysticercosis
Mfano wake ni kifafa
👉30% ya wagonjwa wenye kifafa huwa ni wale ambao hushambuliwa Na minyoo hii ipatikanayo kwenye nguruwe
👉🏾Watu milioni 50 duniani wanaopata kifafa , huwa ni walaji wazuuri Wa Nguruwe.

*JEE NG'OMBE, MBUZI, KONDOO NA WANYAMA WENGINE WALIWAO NA WENGI HAWANA MINYOO??*
Ukweli ni kwamba Hata wanyama wengine nyama zao huwa zina minyoo aina ya Taenia saginata.
Ila minyoo ya Taenia saginata ni tofauti Na Taenia solium kwa sababu; Saginata wanakufa kwa joto Dogo sana, lakini solium wanahitaji 71C bila Hata kupungua!!
Swali langu kwako wewe msomaji Wa nakala hii;
👉🏾Nani anaepika huku akipima joto limefika au laa???

*HITIMISHO*
Tahadhari, sana Na nyama ya nguruwe , kwa sababu madhara yake ni makubwa kuliko faida yake!!!

*IMEANDIKWA NA ;*
Dr Isack
0715691898
Call 0745498485

Jumamosi, 13 Oktoba 2018

UJINGA.

WAJUE WANAUME 15 WAJINGA..

KAMA KUNAMTU NITAMKWAZA ABADILIKE.

1) Anaemshawishi mwanamke akatoe mimba ili aendelee kufanya anasa. Huyo NIMJINGA

2) Anaenyoa viduku kuvaa milegezo nakusuka dred kama mwanamke. Huyo NIMJINGA

3) Asiyemjali mke na familia yake  nakumthamini mchepuko anaemchuna pesa kila siku. Huyo NIMJINGA

4) Anaemdhalilisha mwanamke wakati anajua fika amezaliwa na mwanamke. Huyo NIMJINGA.

5) Anaeishikwa dada au shemeji yake wakati hana kazi yeyote kutwa nzima anaangalia tv nakusubili agongee msosi kwa dada yake utafikili nae kaolewa. Huyo NIMJINGA..

6) Anaeshinda vijiweni nakwenye mitandao yakijamii kila kukicha nakupost ujinga bila kazi yeyote wala faida yeyote. Huyo NIMJINGA..

7) Anamiliki simu ya gharama ya juu wakati hana kazi yeyote inayomfanya aingize pesa. Huyo NIMJINGA..

8 ) Anaevaa nguo za kubana zimechanika mpaka magoti yanaonekana kwakigezo kuwa anaenda na wakati. Huyo NIMJINGA.

9) Anaeishi bado kwa mama na angali ana miaka 30

10) Aliye na zaidi ya miaka 30 alafu anaishi kwa wazazi wake mpaka wembe,kula, maji ya kuoga kwa wazazi..Huyo NIMJINGA..

11) Anaye jadili mafanikio ya wengine... Huyo NIMJINGA

12) Anayechonganisha watu na kuwa na tabia za kimbea hadi kusutwa... Huyo NIMJINGA

13) Anayecheza kamali kama njia pekee ya kujipatia kipato... Huyo NIMJINGA

14) Anayedharau kazi na kujifanya baadhi ya kazi hawezi kuzifanya kwasababu si za hadhi yake... Huyo NIMJINGA

15) Asiyemheshimu Mungu,  wazazi na jamii inayomzunguka... Huyo NIMJINGA.

KAMA KUNA TABIA ZINGINE AMBAZO UNAZIFAHAMU ZIANDIKE HAPA..
Imeandikwa na Young thinker 0745498485

Ijumaa, 12 Oktoba 2018

Somo: ALAMA YA MNYAMA.

 Alama Ya Mnyama
Yapo maelezo mengi saana kuhusiana na alama ya mnyama kilamtu anasema kulingana na uelewa wake na jinsi anavyofahamu. Katika hayo yote nadharia pekee yenye mashiko zaidi yaweza kuwa ni Je alama ya mnyama ni nini? Kuna maelezo mengi yaliyotolewa na baadhi ya watu juu ya alama ya mnyama, wengine hudhani kuwa alama ya mnyama ni “chip” ya computa, au kadi, au kitu halisi kinachoweza kubebeka! Lakini Je Biblia inaelezea vipi kuhusu alama ya mnyama? Ngoja tuangalie Mungu anachokisema juu ya alama ya mnyama.

(NB: manenoalama”, “muhuri”, “ishara” au “dalili” ni visawe
Moja kati ya maonyo yenye lugha kali kabisa katika Biblia linapatikana Kitabu cha Ufunuo. Katika onyo hilo Mungu anaelezea adhabu watakayopata wale watakaopokea alama ya mnyama.Mtu awaye yote akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa (alama) katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake, yeye naye atakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipo kuchanganywa na maji.” Ufu. 14:9-10.
Ufunuo 14:12,Hapa ndipo penye subira ya watakatifu,” hao wazishikao Amri za Mungu, na Imani ya Yesu.” Hapa tunayaona makundi mawili ya watu katika siku za mwisho. Wale wenye alama (muhuri) ya Mungu, ndio wale wazishikao Amri za Mungu, na Imani ya Yesu, na wengine ni wale wenye alama ya mnyama, ndio wale waliokubaliana na hila za shetani.

Lakini kama mtu hajui alama ya mnyama ni ipi, bila shaka ataishia kuwa nayo hata bila kujua kuwa anayo. Je, una uhakika kuwa unaweza kuitambua alama ya mnyama? Bila hivyo maisha yako yako hatarini.

Somo hili linaweza kufunua ukweli dhidi ya mambo ambayo umekuwa ukiyaamini na kuyapenda sana tangu utoto. Lakini kwa kuwa Mungu katika upendo wake anatutumia ujumbe huu maalum, ni vyema kuupokea na kufuata ushauri wake.

Heri asomaye na wao wayasikiao maneno ya unabii huu, na kuyashika yaliyoandikwa humo; kwa maana wakati u karibu.” Ufu. 1:3.
1. Kwa kuwa tunataka kujifunza juu ya Alama ya Mnyama, mnyama mwenyewe ni kitu gani?

Wanyama hao wakubwa walio wanne ni wafalme wanne watakaotokea duniani.” Dan. 7:17.

Katika unabii mnyama anawakilisha ufalme, serikali au taasisi yenye mamlaka.
2. Mnyama anayeelezewa katika Ufunuo 13 ana sifa zipi?

Kisha nikaona mnyama akitoka katika bahari, mwenye pembe kumi, na vichwa saba, na juu ya pembe zake ana vilemba kumi, na juu ya vichwa vyake majina ya makufuru. Na yule joka akampa nguvu zake na kiti chake cha enzi na uwezo mwingi. Nikaona kimoja cha vichwa vyake kana kwamba kimetiwa jeraha la mauti, na pigo lake la mauti likapona. Dunia yote ikamstaajabia mnyama yule. Wakamsujudu yule joka kwa sababu alimpa huyo mnyama uwezo wake; nao wakamsujudu yule mnyama, wakisema, Ni nani afananaye na mnyama huyu? Tena ni nani awezaye kufanya vita naye?

Naye akapewa kinywa cha kunena maneno makuu, ya makufuru. Akapewa uwezo wa kufanya kazi yake miezi arobaini na miwili. Akafunua kinywa chake amtukane Mungu, na kulitukana jina lake; na maskani yake, nao wakaao mbinguni. Tena akapewa kufanya vita na watakatifu na kuwashinda, akapewa uwezo juu ya kila kabila na jamaa na lugha na taifa. Na watu wote wakaao juu ya nchi watamsujudu, kila ambaye jina lake halikuandikwa katika Kitabu cha Uzima cha MwanaKondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia.

Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo; maana ni hesabu ya kibinadamu. Na hesabu yake ni mia sita, sitini na sita.” Ufu. 13:18.

Mnyama huyu anaonekana wazi kuwa ni taasisi ya kidini inayopingana na Mungu. Ni taasisi inayotaka kusujudiwa au kuabudiwa. Hebu tuziangalie alama nane za kuweza kuitambua taasisi hii.

A. Inapokea mamlaka yake toka kwa Joka (12)

Joka hapa anawakilisha Shetani (Ufu. 12:3,4,9), lakini Shetani alifanya kazi yake kwa njia ya ufalme wa Roma. Mfalme wa Kiroma Herode alijaribu kumwua Yesu kwa kuua watoto wa Bethlehemu (Mt. 2:16-18). Hivyo Joka anamaanisha pia ufalme wa kipagani wa Roma.

Kuna taasisi moja tu ya kidini iliyopokea kiti cha enzi na mamlaka toka Ufalme wa Roma. Historia inatueleza wazi kuwa taasisi hiyo ni Kanisa la Roma.

“Kanisa la Roma lilijiingiza mahali pa Ufalme wa Roma na kuuendeleza. Papa ni mrithi wa Kaisari.” Bila shaka alama ya kwanza inahusu Mamlaka ya Papa.

B. Ni ufalme ulioenea dunia nzima (3,7).

Hakuna anayeweza kubisha kuwa mamlaka ya papa ilienea dunia nzima katika karne za kati. Alama hii tena inahusu Mamlaka ya Papa.

C. Ingedumisha uwezo wake kwa miezi 42.

Miezi 42 ni sawa na siku 30 x 42 = 1260. Katika unabii siku moja ni sawa na mwaka mmoja (Eze. 4:6). Uwezo wa Mamlaka ya Papa ulifkia kilele mwaka 538 B.K. kutokana na barua ya Mfalme Justinian iliyomtambua askofu wa Roma kama mkuu wa makanisa yote. Hata hivyo, uwezo wa Mamlaka ya Papa ulikomeshwa mwaka 1798 ambapo Jemadari wa Kifaransa, Berthier, aliingia Roma na kumteka Papa. Kuanzia mwaka 538 B.K. hadi mwaka 1798 ni miaka 1260 kamili.

D. Ni taasisi yenye kufanya makufuru (5,6).

Biblia inaelezea kuwa makufuru ni kudai kuwa yeye ni Mungu, na kudai kuwa ana uwezo wa kusamehe dhambi (Yn 10:33; Luka 5:21).

Mamlaka ya Papa tena inayo alama hii, kwani inadai kuwa mapadre wanaweza kusamehe dhambi. Angalia jinsi Katekisimu moja inavyosema: Swali: Je, Padre husamehe kabisa dhambi, au huwa anatangaza tu kwamba zimeondolewa?

JIBU: Padre husamehe kabisa dhambi kwa uwezo aliopewa na Yesu Kristo.

Pia mamlaka hii hudai kuwa Mungu. Hii hapa ni baadhi ya kauli zake: (i) “Wewe ni Mungu mwingine hapa duniani.” (ii) “Papa siyo mwakilishi wa Yesu Kristo tu, lakini ni Yesu Kristo mwenyewe aliyefichwa katika mwili.”

E. Ni taasisi iliyopata Jeraha la Mauti, kisha likapona, na “dunia nzima ikamstaajabia” (fungu la 3).

Mamlaka ya Papa ilipata pigo la mauti mwaka 1798 Papa alipotekwa na Jemadari Berthier na kufa uhamishoni. Ulaya yote ilidhani kuwa huo ulikuwa mwisho wa Mamlaka ya Papa. Lakini leo hii kila mtu anatambua kuwa Mamlaka ya Papa ndiyo yenye ushawishi na mvuto kuliko zote duniani. Jeraha la mauti lilipona pale Kiongozi wa Italia (Musolini) alipomrudishia Papa Mamlaka ya Kiserikali na kuunda Taifa la Vatikani mwaka 1929. Leo hii mamilioni wanaiangalia Mamlaka ya Papa kama tumaini pekee la umoja, upendo, amani na uungwana. Hivyo tena Mamlaka ya Papa inayo alama hii.

F. Ina namba ya siri 666. Ufunuo 13:17-18

inatuambia tuihesabu hesabu ya mnyama maana ni hesabu ya kibinadamu.

Zingatia kuwa baadhi ya heruf za Kirumi hutumika pia kama namba. Hivyo basi, hesabu ya jina la mtu ni jumla ya heruf zote zilizo katika jina lake zinazotumika kama namba.

Binadamu tunayemfkiria kila tunapozungumza juu ya Mamlaka ya Papa ni Papa mwenyewe. Moja kati ya majina rasmi ya Papa ni “MWAKILISHI WA MWANA WA MUNGU kwa Kirumi ni ‘VICARIUS FILII DEI’.
Kitabu cha Ufunuo kinasema kuwa jumla ya namba za Kirumi katika jina lake ni 666

Hivyo Mamlaka ya Papa inayo alama hii tena.

G. Ni Taasisi au Mamlaka ya Kidini.

Inajihusisha na mambo ya kiroho. Neno “kusujudia” limetumika mara 4 katika Ufunuo 13. Sura hii inahusu ibada ya bandia. Hii ni alama nyingine inayoonekana katika Mamlaka ya Upapa.

H. Itafanya vita na kuwatesa Wakristo (fungu la 7).

Historia inaonyesha wazi kuwa Mamlaka ya Papa ilitesa na kuangamiza Wakristo, hasa katika kilele cha utawala wake katika karne za kati. Wanahistoria wengi wanasema zaidi ya watu milioni hamsini waliuawa kwa ajili ya imani zao katika kipindi cha dhiki kuu. Kanisa lilidhani kuwa lilikuwa linamsaidia Mungu kuondoa “uzushi.” Lakini ukweli unabaki pale pale kwamba lilitesa na kuangamiza. Mamlaka ya Papa tena inayo alama hii.

Nb Wapo Wakristo wengi wa Kikatoliki ambao ni wema, waaminifu na wenye upendo, wanaomtumikia Yesu, na Yesu anawahesabu kuwa ni watu wake.

Papa Yohana Paulo II mwenyewe anaonekana kuwa mtu mchangamfu, mwenye huruma, mwenye kupenda mapatano, na jasiri anayempenda Mungu. Hili sio somo la kuwasuta rafki zetu, Wakristo wa Kikatoliki. Hili ni shambulio dhidi ya Ibilisi aliyesababisha yote haya. Hata hivyo ni kweli kwamba Mungu mwenyewe ndiye aliyetuambia kuwa Taasisi hii ina alama ambayo hatupaswi kuipokea. Waprotestanti waaminifu, Wakatoliki, Wayahudi, na wasiokuwa katika kanisa lo lote, wanapaswa kuijua alama hii ili wasiipokee. Tunamshukuru Mungu kwa kuifunua mipango mibovu ya Shetani ya kutuangamiza sisi sote.

ALAMA YA MUNGU
Ili tuijue alama hii ya Mamlaka ya Papa, ni lazima kwanza tuijue Alama ya Mungu.

3. Je, Mungu naye anayo alama?

Nikaona malaika mwingine, akipanda kutoka maawio ya jua, mwenye muhuri ya Mungu aliye hai;… Akisema, Msiidhuru nchi, wala bahari, wala miti, hata tutakapokwisha kuwatia muhuri watumwa wa Mungu wetu juu ya vipaji vya nyuso zao.” Ufu. 7:2,3. “BWANA akamwambia, Pita kati ya mji, kati ya Yerusalemu, ukatie alama katika vipaji vya nyuso vya watu wanaougua na kulia kwa sababu ya machukizo yote yanayofanyika kati yakeWaueni kabisa, mzee, na kijana, na msichana, na watoto wachanga, na wanawake; lakini msimkaribie mtu ye yote mwenye hiyo alama; tena anzeni katika patakatifu pangu.” Eze. 9:4,6.

Mungu anayo alama kwa ajili ya watu wake.

4. Je, tunaweza kuijua alama hiyo kwa uhakika?

Tena naliwapa Sabato zangu, ziwe ishara kati ya mimi na wao, wapate kujua ya kuwa mimi, BWANA, ndimi niwatakasayeZitakaseni Sabato zangu; nazo zitakuwa ishara kati ya mimi na ninyi, mpate kujua ya kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.” Eze. 20:12,20.

Kwa uhakika kabisa. Mungu ameweka Sabato ili iwe ishara ya watu wanaomtambua kwamba yeye ndiye Muumbaji na kwamba yeye ndiye anayewatakasa watu wake (angalia pia Yer. 10:10-16).

MAMLAKA YA PAPA
5. Biblia inasema kuwa Mamlaka ya Papa ingeazimu kufanya jambo gani?

Naye ataazimu kubadili majira na Sheria.” Dan. 7:25.

Kubadili majira (muda) na Sheria. Mamlaka ya Papa inajigamba yenyewe kuwa ilifanya jambvo hilo. Hebu angalia mahojiano haya yaliyo katika Katekisimu ya Waumini ya Mafundisho ya Kikatoliki, katika ukurasa wa 50.

Swali: Siku ya Sabato ni ipi?
Jibu: Siku ya Sabato ni Jumamosi.
Swali: Kwa nini tunaiadhimisha Jumapili badala ya Jumamosi?
Jibu: Tunaadhimisha Jumapili badala ya Jumamosi kwa sababu Kanisa Katoliki lilihamisha utakatifu wa siku hiyo kutoka Jumamosi kwenda Jumapili.”

Mtu mmoja aliposoma mahojiano haya alishangaa, naye akidhani kuwa wachapaji walikuwa wamekosea, alimwandikia James Cardinal Gibbons wa Baltimore na kumwuliza kama kweli kanisa lilibadili siku ya Ibada kutoka Jumamosi kwenda Jumapili Kadinali alijibu: “Ndiyo, Kanisa Katoliki linadai kuwa badiliko hilo lilikuwa ni tendo lake. Na tendo hilo ni ALAMA ya uwezo wake wa kikanisa na mamlaka yake katika masuala ya kidini.”

Angalia pia mahojiano haya katika Katekisimu ya Mafundisho iliyoandikwa na Stephen Keenan.

Swali: Je, unayo njia nyingine ya kuthibitisha kuwa kanisa lina uwezo wa kuweka sikukuu?

Jibu: “Kama lisingekuwa na uwezo kama huo, lisingeweza kufanya jambo ambalo hata wanadini wa leo wanalikubali. Lisingeweza kuweka maadhimisho ya Jumapili, siku ya kwanza ya juma, badala ya maadhimisho ya Jumamosi, siku ya saba ya juma, mabadiliko ambayo hayakutokana na Maandiko.”

Mamlaka ya Papa hapa inauliza swali. Hapa kuna swali maarufu ambalo Mamlaka ya Papa imekuwa ikiwauliza mara kwa mara Waprotestanti, na cha kushangaza Waprotestanti wamekuwa hawalijibu:

Mtaniambia kuwa Jumamosi ilikuwa Sabato ya Wayahudi. Lakini Sabato ya Wakristo ilibadilishwa kwenda Jumapili. Ilibadilishwa! Lakini na nani? Ni nani aliye na mamlaka ya kubadili amri dhahiri ya Mungu Mwenyezi? Mungu anaposema, “Ishike siku ya saba uitakase,” ni nani anayeweza kusema, hapana. Unaweza kufanya kazi na kushughulika na mambo yote ya kidunia katika siku ya saba, lakini uishike na kuitakasa siku ya kwanza badala yake? Hili ni swali muhimu ambalo sijui namna mnavyoweza kulijibu. Ninyi ni Waprotestanti na mnadai kuwa mnafuata Biblia, tena Biblia peke yake, na bado katika suala muhimu kama la kuadhimisha siku moja kati ya saba mnakwenda kinyume na andiko la Biblia na kuweka siku nyingine badala ya ile ambayo Mungu ameamuru. Amri ya kushika siku ya saba ni moja kati ya Amri kumi. Mnaamini kuwa zile nyingine tisa zinapaswa kushikwa, ni nani aliyewapa ruhusa ya kuichezea ile ya nne? Kama kweli mnashikilia msimamo wenu, kama kweli mnataka kufuata Biblia, tena Biblia peke yake, mnapaswa kutuonyesha sehemu katika Agano Jipya ambapo amri ya nne imebadilishwa. (Nukuu kutoka, Library of Christian Doctrine. Burns and Oates, uk. 3-4., London.)

Mamlaka ya Papa inadai kuwa ilibadili siku ya Ibada toka Jumamosi kwenda Jumapili na kwamba Jumapili au kushika Jumapili ni Alama ya Mamlaka na Uwezo wake. Alama au Ishara ya uwezo wa Mungu wa kuumba na kutakasa ni Sabato au kushika Sabato, na Ishara au Alama ya uwezo wa mnyama ni Jumapili.

6. Je, kuna wakati ambapo watu watalazimishwa kupokea Alama ya Mnyama?

Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao; tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake.” Ufu. 13:16,17.

Biblia inasema wazi kwamba watu watawekewa vikwazo vya kiuchumi na hata kuuawa wasipoipokea Alama ya Mnyama.

7. Nifanye nini sasa ili nisiipokee alama hiyo?

Ufunuo 14:9-11 inaonya juu ya Alama ya Mnyama; fungu la 12 linaelezea jinsi watakatifu watakavyofanya ili kuepuka alama hiyo. Watashika Amri za Mungu na kuwa na Imani ya Yesu. Bwana asifwe, ni imani ya Yesu inayofanya mwujiza kwa watu wanaoshika amri.

Ujumbe wa Onyo la Mwisho toka kwa Mungu (Ufu. 14:6-12).

Onyo hili ni pamoja na:

(i) Msujudieni Muumbaji (fungu la 7).
Maana yake ni kuishika ishara au alama ya uumbaji wake, yaani, Sabato yake.

(ii) Msipokee Alama ya Mnyama (fungu la 9-10).
Maana yake usiikubali wala kuipokea ishara ya bandia ya utakatifu wa Jumapili.

Ni Mungu anayetupa maonyo haya. Shetani, adui wa Mungu anataka nimtii kwa kushika alama yake. Yesu, Mwokoziwangu anataka nimtii kwa kuiadhimishaishara au alama yake.

Je, sasa umeelewa kwamba mtu ye yote Akiipokea Alama ya Mnyama atapotea?

Yesu anabisha kwenye mlango wa moyo wako.
Anasubiri jibu toka kwako. Je, utaamua kuipokea ishara yaani kupokea chapa yake tukufu kama ushahidi kwamba umempokea yeye kama Bwana na Mwokozi wako?
Mawasiliano 0745498485

Jumamosi, 31 Desemba 2016

UNABII WA SIKU 2300

Unabii wa Miaka 2300💚

✔✔✔✔✔✔💚Daniel 8:13, 14…. 13, Ndipo niamsikia mtakatifu mmoja akinena na mtakatifu mwingine akamuuliza huyo aliyenena, Haya maono katika habari sadaka ya kuteketezwa ya daima, na lile kosa lifanyalo ukiwa, yataendelea hata lin, kukanyagisha patakatifu na jeshi? 14, Akamwambia, Hata nyakati za jioni asubuhi elfu mbili na mia tatu; ndipo patakatifu patakapotakaswa.

Ni katika kipindi cha utawala wa Belshaza mfalme wa Babeli mwana wa mfalme Nebukadneza (Daniel 5:2) ndipo Daniel anaoneshwa maono haya Daniel 8:1 Katika mwaka wa tatu wa kumiliki kwake mfalme Belshaza maono yalinitokea mimi, naam, mimi Danieli, baada ya yaliyonitokeahapo kwanza. Akiwa katika wilaya ya Elimu, shushani ngomeni katika mto ulai huko Babeli

Mwanzo wa njozi ya Danieli anaoneshwa kondoo mwenye pembe mbili akisimama na kutawala dunia akisukuma upande wa magharibi na kaskazini na kusini (Daniel 8:3, 4). Kisha anaona beberu akiinuka upande wa mashariki akiwa na pembe mashuhuri kati ya macho (Daniel 8:5). (kwa faida ya msomaji pembe katika unabii huwakilisha ufalme au utawala). Akamkaribia Yule kondoo akamkasirikia kwa ghadhabu nyingi naye akampiga hata kuvunja pembe zake, akamwangusha chini hata kumkanyaga-kanyaga

Baadaye ile pembe ikavunjika kwa kujitukuza hata zikatokea pembe nne zikaielekea pepo nne za mbingu nazo zikatwala kwa kipindi Fulani (Daniel 8:8). Daniel 8:9 Na katika moja ya hizo pembe ilitokea pembe ndogo, iliyokuwa sana, upande wa kusini, na upande wa magharibina upande wan chi ya uzuri. Pia katika fungu la 23; Na wakati wa mwisho wa ufalme wao, wakosao watakapotimia, mfalme mwenye uso mkali, afahamuye mafumbo………atasimama. Hii humaaniasha wakati wa mwisho wa utawala wa falme nne zilizoinuka kutoka kwa Yule beberu ndipo utainuka tena ufalme mwingine unaowakilishwa na pembe ndogo, mfalme mwenye uso mkali, afahamuye mafumbo.

Daniel 8:10-14 Nayo ikakua, kiasi cha kulifikilia jeshi la mbinguni ; ikaangusha chini baadhi ya jeshi lile, na nyota ikazikanyaga. Naam ikajitukuza hata juu ya aliye mkuu wa jeshi hilo, ikamwondolea sadaka ya kuteketezwa ya daima, na mahali pa patakatifu pake pakaangushwa chini. Na jeshi likatolewa kwake pamoja na sadaka ya kuteketezwa ya daima, kwa sababu ya makosa; nayo ikaangusha kweli hata chini; ikatenda ilivyopenda, na kufanikiwa. Ndipo niamsikia mtakatifu mmoja akinena na mtakatifu mwingine akamuuliza huyo aliyenena, Haya maono katika habari sadaka ya kuteketezwa ya daima, na lile kosa lifanyalo ukiwa, yataendelea hata lin, kukanyagisha patakatifu na jeshi? Akamwambia, Hata nyakati za jioni asubuhi elfu mbili na mia tatu; ndipo patakatifu patakapotakaswa.

Kuinuka kwa pembe hii ndogo na matendo yake ndiko kunamhuzunisha mtakatifu mmoja na hivyo inampelekea kutaka kujua hatima ya haya yote. Nayo ni nyakati za jioni na asubuhi elfu mbili na mia tatu (2300).

Nini✔✔✅✅ tafsiri yake miaka hii 2300??

Katika sura ya Daniel 8:14 tunaambiwa matukio haya yatachukua muda nyakati za jioni na asubuhi 2300 lakini hatuambiwi chochote kuhusu mwanzo wala mwisho wake.

Katik♿ kuelewa tafsiri hii lazima tuelewe mambo yafuatayo.

    nyakati za jioni na asubuhi ni sawa na siku nzima amabyo pia huanza jioni hata jioni. Mwanzo 1:5………… ikawa jioni ikawa asubuhi, siku moja. kwahiyo nyakati za jioni na asubuhi 2300 ni sawa na siku kamili 2300
    Katika unabii siku moja ni sawa na mwaka mmoja Ezekiel 4:6………siku arobaini, siku moja kwa mwaka mmoja, nimekuagiza kwahiyo siku 2300 za kiunabii ni sawa na miaka iliyokamilika 2300.. Hivyo tunasema ili haya yote yafikie mwisho ni mpaka kukamilika kwa miaka 2300.
    Unabii wa miaka 2300 ndio unabii mrefu kwenye biblia kuliko mengine yote, hivyo unabii mwingine kama vile miaka 1260, majuma 70, miaka 1335 na 1290 zote huangukia kwenye miaka 2300.

Mwanzo♐♐♐♐♐ wa miaka hii ni upi?💯💯💯

Mwanzo wa miaka hii tunaelewa kwa kuelewa mianzo ya majuma 70 katika Daniel 9:24. Muda wa majuma sabini umeamriwa juu ya watu wako, na juu ya mji wako mtakatifu………,25 Basi ujue na kufahamu, ya kuwa tangu kuwekwa amri ya kutengeneza na kujenga upya mji wa Yerusalemu….. kutakuwa na majuma saba………….

💚💚💚Majuma sabini ni sawa na miaka 490. 70×7=490. Hii hutuambia kuwa kulikuwa na miaka 490 ulioamriwa juu ya taifa la Israeli.

Amri juu ya ujenzi wa mji wa yerusalemu ulitolewa na mfalme Artashasta mfalme wa uajemi mnamo mwaka wa 457 K.K (kabla ya kristo) Ezra 7:21-26 Na mimi, naam mimi, mfalme Artashasta, nawapa amri wote wenye kutunza hazina…..hata kiasi cha cha talanta mia za fedha …. kila neon litakaloamriwa na Mungu wa mbinguni, na litendeke halisi kwa ajili ya ya nyumba ya Mungu wa mbinguni…….. Kuanzia mwaka wa 457 hitimisho la miaka 490 au majuma 70 hufikia 34 B.K (baada ya Kristo), (kumbuka kuna mwaka kutoka 0-1)….katika miaka 2300 baada ya kukamilika kwa miaka 490 tunasalia na miaka 1810.

               490+1810=2300.na

Siku 2300 zilioneka kuanza wakati amri ya Artashasta kwa ajili ya urejeshwaji wa na ujenzi wa Yerusalemu ilipotolewa majira ya kipupwe ya mwaka 457 K.K. Kwahiyo mwanzo wa miaka 2300 ni mwaka 457 B.K na huishia mwaka 1844 B.K.

Somo hili limeandaliwa na mwinjilisti Peter nakuletwa na Chuminames.
Ubarikiwe kwa kujifunza.

Alhamisi, 1 Desemba 2016

Jumamosi, 30 Julai 2016

Mbinu Pekee ya Kristo. Jumapili 31/07/2016

Katika kifungu cha maneno ambacho huwa kinanukuliwa mara nyingi, Ellen G. White anaeleza kwa ufupi Matendo Yesu aliyotenda ili kuwapatia watu wokovu( Angalia Mt.9:35-36).

Mbinu ya Yesu pekee ndiyo itatoa mafanikio thabiti ya kuwafikia watu. Mwokozi aliwafikia watu kama mmoja wao aliyetamani mazuri kwao.Alionesha huruma yake kwao, Aliwahudumia katika mahitaji yao,na kuzishinda Imani zao,na ndipo alipoamuru “Wamfuate”-Ellen G.White, The ministry of Healing, uk. 143.

Hebu na tuchambue jambo hili kidogo:

1.Yesu alijichanganya na watu kama aliyetamani mema kwao( Alifungua mitandao ya kuwasiliana nao)

2.Yesu aliwahurumia watu(Alianzisha umoja nao)

3. Yesu aliwahudumia katika mahitaji yao (Hili pia lilileta umoja)

4.Alipounganisha kipengele cha kwanza, cha pili, na cha tatu, Ali hakikisha kuzivuta Imani za watu wale.

5. “ Ndipo alipo amuru, ‘Nifuateni’(Kuwa wanafunzi)

Tunachokiona hapa ni injili kwa ujumla, na inavyo jumuisha mambo yote kimsingi. Huduma hii itatusaidia na kutuelekeza sisi katika kutangaza habari njema. Yesu hakutenganisha masuala yote ya kijamii (Hesabu 1-4) na ule wa kutoa mwaliko wa kumfuata yeye, ( Hesabu 5) na sisi pia hatupaswi kutenganisha. Hatua zote zikifuatwa ‘zitatoa mafanikio ya hakika’ Somo hili lita sisitizia katika hatua ya kwanza ya mbinu ya Yesu. Somo la 7-11 yatakazia katika mbinu zile nyingine.

Mafungu yafuatayo hutuambia nini kuhusu Mungu mwana kujichnganya na sisi? Mt. 1:22,23Yn. 1:14.

Sote tumeumizwa na kuharibiwa na dhambi.Ila kila kitu ulimwenguni kilichoharibiwa na dhambi, kinarejeshwa upya kupitia upatanisho wa Mungu na mwanadamu,kwa kupitia upatanisho kamili wa huduma ya Yesu kufanyika mwili. Alijichanganya na kutamani mema kwa mtu halisi na mbari yote ya wanadamu,hata kwa kuwahudumia wale walioonekana na tamaduni zao kama watu wasio faa kitu.

Fikiri juu ya huu ukweli wa kushangaza,kwamba,Yeye aliye viumba vitu vyote(Yohana 1:3)Yesu aliuvaa ubinadamu na kwa ubinadamu huo alijichanganya na kuhudumia jamii ya wanadamu iliyoanguka dhambini (aliwahudumia kama vile ni yeye). Ni kwa njia gani ukweli huu,wenye matumaini kiasi hiki, unaathiri tunavyojichanganya na kuwahudumia wengine?

Lessoni leo. Tar 30/07/2016 Yesu alichangamana na watu

Sabato Mchana
Soma Kwa Ajili ya Somo la Juma Hili: Mt. 1:22, 23;Yn. 1:14Luka 15:3–24Mt. 9:10–13Zab. 51:171 Yoh. 2:16Flp. 2:13–15

Fungu la Kukariri: “‘Basi watoza ushuru wote na wenye dhambi walikuwa wakimkaribia wamsikilize. Mafarisayo na waandishi wakanung’unika, wakisema, Mtu huyu huwakaribisha wenye dhambi, tena hula nao.’”(Luka 15:1, 2).

Shemasi katika kanisa fulani Aliendesha gari lililokuwa limebeba vijana kwenda katika nyumba ya wazee na kuendesha Ibada katika kila mwezi.Katika juma la kwanza, Wakati vijana wakiongoza Ibada ile, Mzee mmoja mlemavu aliyekua ameketi kwenye kiti cha magurudumu, Aliushika kwa nguvu mkono wa shemasi na kuung’ang’ania wakati wa ibada nzima. Huduma hii iliendelea mwezi hata mwezi. Siku moja vijana wale walipokuja kwaajili ya Ibada Mzee yule hakuwepo.Msaidizi wao alipoulizwa alisema, hali yake ilikuwa mbaya usiku mzima kiasi cha kufikiri kwamba kusingekucha akiwa hai. Shemasi alikwenda katika chumba cha yule Mzee, alimkuta amelala pale akiwa hajitambui. Shemasi yule aliushika mkono wa Mzee yule na kumwomba Mungu amwokoe kwaajili ya uzima wa milele. Mzee huyu aliyekua hajitambui aliuvuta mkono wa Shemasi na kuushika kwa nguvu, na shemasi akagundua kuwa maombi yake yalikuwa yamesikiwa. Akitokwa na machozi shemasi alinyanyuka na kutoka nje ya chumba kile,aligongana na mwanamke aliyekuwa mlangoni, Akisema, “mimi ni binti yake, Baba yangu amekua akikusubiri wewe, huku akisema, ‘Yesu huja mara moja kwa mwezi na kuushika mkono wangu, na sitaki kufa kabla sijapata nafasi ya kuushika mkono wake kwa mara nyingine’ ” Imetolewa katika, The least these, video iliyotengenezwa na Old Fashioned Pictures(2004).

Ukiristo ni kuhusu kuwa kama “Yesu” kwa mtu Fulani, Masomo kadhaa yatakayofuata yatalenga masuala ya Huduma ya Yesu na jinsi kanisa lake linavyoweza kuishi kulingana na huduma hiyo.