Jumamosi, 30 Julai 2016

Lessoni leo. Tar 30/07/2016 Yesu alichangamana na watu

Sabato Mchana
Soma Kwa Ajili ya Somo la Juma Hili: Mt. 1:22, 23;Yn. 1:14Luka 15:3–24Mt. 9:10–13Zab. 51:171 Yoh. 2:16Flp. 2:13–15

Fungu la Kukariri: “‘Basi watoza ushuru wote na wenye dhambi walikuwa wakimkaribia wamsikilize. Mafarisayo na waandishi wakanung’unika, wakisema, Mtu huyu huwakaribisha wenye dhambi, tena hula nao.’”(Luka 15:1, 2).

Shemasi katika kanisa fulani Aliendesha gari lililokuwa limebeba vijana kwenda katika nyumba ya wazee na kuendesha Ibada katika kila mwezi.Katika juma la kwanza, Wakati vijana wakiongoza Ibada ile, Mzee mmoja mlemavu aliyekua ameketi kwenye kiti cha magurudumu, Aliushika kwa nguvu mkono wa shemasi na kuung’ang’ania wakati wa ibada nzima. Huduma hii iliendelea mwezi hata mwezi. Siku moja vijana wale walipokuja kwaajili ya Ibada Mzee yule hakuwepo.Msaidizi wao alipoulizwa alisema, hali yake ilikuwa mbaya usiku mzima kiasi cha kufikiri kwamba kusingekucha akiwa hai. Shemasi alikwenda katika chumba cha yule Mzee, alimkuta amelala pale akiwa hajitambui. Shemasi yule aliushika mkono wa Mzee yule na kumwomba Mungu amwokoe kwaajili ya uzima wa milele. Mzee huyu aliyekua hajitambui aliuvuta mkono wa Shemasi na kuushika kwa nguvu, na shemasi akagundua kuwa maombi yake yalikuwa yamesikiwa. Akitokwa na machozi shemasi alinyanyuka na kutoka nje ya chumba kile,aligongana na mwanamke aliyekuwa mlangoni, Akisema, “mimi ni binti yake, Baba yangu amekua akikusubiri wewe, huku akisema, ‘Yesu huja mara moja kwa mwezi na kuushika mkono wangu, na sitaki kufa kabla sijapata nafasi ya kuushika mkono wake kwa mara nyingine’ ” Imetolewa katika, The least these, video iliyotengenezwa na Old Fashioned Pictures(2004).

Ukiristo ni kuhusu kuwa kama “Yesu” kwa mtu Fulani, Masomo kadhaa yatakayofuata yatalenga masuala ya Huduma ya Yesu na jinsi kanisa lake linavyoweza kuishi kulingana na huduma hiyo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni