Katika kifungu cha maneno ambacho huwa kinanukuliwa mara nyingi, Ellen G. White anaeleza kwa ufupi Matendo Yesu aliyotenda ili kuwapatia watu wokovu( Angalia Mt.9:35-36).
Mbinu ya Yesu pekee ndiyo itatoa mafanikio thabiti ya kuwafikia watu. Mwokozi aliwafikia watu kama mmoja wao aliyetamani mazuri kwao.Alionesha huruma yake kwao, Aliwahudumia katika mahitaji yao,na kuzishinda Imani zao,na ndipo alipoamuru “Wamfuate”-Ellen G.White, The ministry of Healing, uk. 143.
Hebu na tuchambue jambo hili kidogo:
1.Yesu alijichanganya na watu kama aliyetamani mema kwao( Alifungua mitandao ya kuwasiliana nao)
2.Yesu aliwahurumia watu(Alianzisha umoja nao)
3. Yesu aliwahudumia katika mahitaji yao (Hili pia lilileta umoja)
4.Alipounganisha kipengele cha kwanza, cha pili, na cha tatu, Ali hakikisha kuzivuta Imani za watu wale.
5. “ Ndipo alipo amuru, ‘Nifuateni’(Kuwa wanafunzi)
Tunachokiona hapa ni injili kwa ujumla, na inavyo jumuisha mambo yote kimsingi. Huduma hii itatusaidia na kutuelekeza sisi katika kutangaza habari njema. Yesu hakutenganisha masuala yote ya kijamii (Hesabu 1-4) na ule wa kutoa mwaliko wa kumfuata yeye, ( Hesabu 5) na sisi pia hatupaswi kutenganisha. Hatua zote zikifuatwa ‘zitatoa mafanikio ya hakika’ Somo hili lita sisitizia katika hatua ya kwanza ya mbinu ya Yesu. Somo la 7-11 yatakazia katika mbinu zile nyingine.
Mafungu yafuatayo hutuambia nini kuhusu Mungu mwana kujichnganya na sisi? Mt. 1:22,23; Yn. 1:14.
Sote tumeumizwa na kuharibiwa na dhambi.Ila kila kitu ulimwenguni kilichoharibiwa na dhambi, kinarejeshwa upya kupitia upatanisho wa Mungu na mwanadamu,kwa kupitia upatanisho kamili wa huduma ya Yesu kufanyika mwili. Alijichanganya na kutamani mema kwa mtu halisi na mbari yote ya wanadamu,hata kwa kuwahudumia wale walioonekana na tamaduni zao kama watu wasio faa kitu.
Fikiri juu ya huu ukweli wa kushangaza,kwamba,Yeye aliye viumba vitu vyote(Yohana 1:3)Yesu aliuvaa ubinadamu na kwa ubinadamu huo alijichanganya na kuhudumia jamii ya wanadamu iliyoanguka dhambini (aliwahudumia kama vile ni yeye). Ni kwa njia gani ukweli huu,wenye matumaini kiasi hiki, unaathiri tunavyojichanganya na kuwahudumia wengine?
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni