Jumamosi, 28 Mei 2016

Lessoni juma hili: Yesu akiwa Yerusalemu

Utangulizi:
Kumkubali kiongozi kuna
matokeo yake. Ukubali wako unamaanisha
kwamba unamkubali mtu huyo aweze
kuongoza na kufanya maamuzi ya msingi.
Mathayo anaendelea na mwendelezo wake
wa kuthibitisha kwamba Yesu ni Masihi,
Yesu ni Bwana. Sasa Mathayo ananukuu
matokeo ya kukataa kumfuata Yesu kwa
dhati. Hebu tuzame kwenye somo letu la
Biblia ili tujifunze zaidi!

I. Kuingia
A. Soma Mathayo 21:1-3. Je,
ungetilia mashaka maelekezo haya endapo
Yesu angekupatia hayo maelekezo?
(Ningepata ugumu sana kuchukua vitu vya
thamani kwa msingi kwamba nitamwambia
mwenye navyo “Bwana anawahitaji.” Hata
hivyo, ikiwa Yesu anaweza kuyaona mambo
yajayo, ninawezaje kutilia shaka jambo
lolote analolisema?)
B. Soma Mathayo 21:4-5.
Mathayo anathibitisha jambo gani hapa?
(Kwa mara nyingine, Mathayo anathibitisha
kuwa Yesu anatimiza unabii kwamba yeye
ni Masihi. Utaona kwamba anakuja kwa
upole.)
C. Soma Mathayo 21:6-9. Soma
Mathayo 16:20. Jambo gani limetokea? (Sasa
ni wakati wa kutangaza kuwa Yesu ni
Masihi.)
1. Makutano wanasema nini
kumhusu Yesu? (Kwamba Yesu ni “Mwana
wa Daudi,” Yeye ajaye “kwa jina la Bwana,”
na “Hosana.”)
2. Soma Zaburi 118:25-26.
“Hosana” maana yake ni “utuokoe sasa” au
“tafadhali tuokoe.” Je, Zaburi 118
inatufundisha jambo gani la ziada kuhusu
makutano kupaza sauti? (Kwamba Yesu
ndiye anayekuja kuwaokoa. Kitendo hiki
kinatangaza kwamba Yesu ni Bwana na
Masihi aliyeahidiwa.)
D. Soma Mathayo 21:10-11. Je,
jibu hili lilisababisha matatizo? (Soma
Mathayo 2:3-6. Ikiwa watu walikuwa wana
ufahamu juu ya unabii wa Masihi, kusema
kwamba Yesu alikuwa anatokea Nazareti
kungesababisha mtafaruku.)
1. Je, ungefanya nini endapo
ungekuwepo mahali pale ukisikiliza jambo
hili? (Natumaini ningefanya uchunguzi
zaidi!)
II. Hekalu
A. Soma Mathayo 21:12-13.
Tulisikia wanachokisema watu wengine
kumhusu Yesu. Tumefuatilia mfululizo wa
uthibitisho wa Mathayo kumhusu Yesu. Yesu
anajizungumziaje hapa? (Analiita hekalu
kuwa ni “nyumba yangu” na anaonesha
mamlaka juu ya kile kinachoendelea
hekaluni.)
B. Soma Mathayo 21:14-15. Je,
viongozi wa dini wanaudhika kutokana na
Yesu kuwaponya watu? (Soma Mathayo
21:16. Walikasirika kuhusu Yesu kuitwa
“Mwana wa Daudi” na yeye (Yesu)
kuenenda kama kiongozi wao.)
C. Soma Zaburi 8:1-2. Hili ndilo
fungu ambalo Yesu analinukuu. Fungu hili
linabainisha jambo gani? (Kwamba Yesu ni
Bwana, Kwamba Mungu anabariki sifa
anazopewa kutoka kwa watoto, na sababu
ya kufanya hivyo ni “kuwanyamazisha,
kuwakomesha adui na mijilipiza kisasi!”)
III. Mtini
A. Soma Mathayo 21:17-19. Je, hili
ni jambo jema au baya? Je, Yesu
anauangamiza mti kutokana na hasira?
1. Mtini umetenda jambo gani
lililosababisha uangamizwe? (Majani yake
yanakudanganya na kukufanya udhani
kuwa una matunda.)
2. Je, hili ni fundisho kwa
Wakristo wanaojiita kuwa ni Wakristo?
B. Soma Mathayo 21:20-22. Hivi
karibuni nilitazama sinema iliyoonesha
miujiza kadhaa isiyo na maana (ya kipuuzi).
Watu waliota meno ya dhahabu, vito vya
bandia vilitengenezwa bila kutumia
rasilimali yoyote, nk. Asili ya kipuuzi ya
miujiza hiyo ilinifanya nishangae na
kutafakari asili yake. Je, tunashughulika na
miujiza isiyo na maana katika Mathayo 21:
kuufanya mtini unyauke na kuhamisha
milima? (Mti ni fundisho kwa wanafiki.
Milima inaweza kuwa inawakilisha
changamoto na matatizo yaliyopo maishani
mwako. Yesu anatuambia kuwa imani ndio
jibu kwa changamoto za maisha.)
IV. Shamba la Mizabibu
A. Soma Mathayo 21:33-36.
Wapangaji wanaweza kujenga hoja gani
kutokana na mwenendo (tabia) wao?
(Hawana kisingizio kwa ajili ya jambo hili.)
B. Soma Mathayo 21:37-39. Nia
ya kumwua mwana wa mwenye shamba ni
ipi? (Mali. Uroho/ulafi. Wizi.)
C. Soma Mathayo 21:40-43. Yesu
anasema huu ni muujiza kuhusu viongozi
wa dini na watu watakaomwua (Yesu).
Walitaka mali gani? Shamba lao la mzabibu
lililoibwa ni lipi? Mungu alitarajia taifa lake
teule kuzaa matunda ya roho. Badala yake,
walijielekezea faida na kujisifu wao
wenyewe.)
D. Fikiria tena kuhusu mtini
ulionyauka. Je, kweli huo ni muujiza wa
kipuuzi? Uangamivu wa kipuuzi? (Hii
ilielezea sababu ya taifa la Kiyahudi
lililomkataa Yesu litakavyoangamizwa hivi
karibuni.)
E. Soma Mathayo 21:44. Je, hizi
ndizo chaguzi zetu mbili maishani?
F. Soma Mathayo 21:45. Je,
walengwa wa mjadala wa Yesu wana
mashaka? (Hapana. Mathayo anabainisha
jambo hili kwa dhahiri kabisa.)
V. Harusi
A. Soma Mathayo 22:1-5. Kwa nini
wale walioalikwa harusini hawaji?
(Wametingwa na shughuli nyingi sana.)
1. Kisingizio chao kinafananaje
na nia ya wale waliotaka kuiba shamba la
mzabibu? (Makundi yote mawili yalikuwa
yanatafuta kujipatia fedha. Walikuwa
wanataka kuongeza mali zao.)
2. Harusi ni ya muhimu kiasi
gani kwa mfalme?
B. Soma Mathayo 22:6-7. Je, hii
ni haki? (Wao ni wauaji! Walimdhihaki na
kumkasirisha mfalme wao.)
1. Je, si kitendo kikubwa kupita
kiasi kuwaua watu kwa sababu
wamekudhihaki na kukukasirisha? (Kwa
mara nyingine, tafakari muktadha uliopo.
Hapo awali Mathayo alielezea kisa cha mtini
na kisa cha shamba la mizabibu. Kuwa
mnafiki, kuipinga injili, kuwatendea vibaya
na kuwaua wafuasi wa Mungu, na
kumkataa Mungu kuna matokeo yake.)
C. Soma Mathayo 22:8-10. Hapa
kigezo cha kuwachagua watu ni kipi? Je,
kuna wanafiki na watu wabaya katika kundi
hili? (Mwaliko ulikuwa kwa ajili ya watu
wote. Watu “wabaya” (pamoja na wema)
waliutikia mwaliko. Kigezo cha kuchaguliwa
ni kuukubali mwaliko.)
D. Soma Mathayo 22:11-12. Kuna
jambo gani la kushangaza kuhusu kutokuwa
na mavazi sahihi? Watu hawa walitolewa
kutoka sehemu mbalimbali za mitaa,
walikuwa wamevaa mavazi ya kuendea
sokoni na kufanya manunuzi mengineyo,
mavazi ya kazini, na mavazi kwa ajili ya
mapumziko ya kawaida!
1. Unadhani kwa nini mtu
mmoja pekee ndiye hakuwa amevaa mavazi
sahihi? (Hii inatusaidia kujaza mashimo
katika kweli zisizoepukika. Lazima kila mtu
alikuwa na upungufu kwenye suala la
mavazi, sio mtu mmoja pekee. Hivyo,
tunajifunza kuwa lazima mfalme atakuwa
aligawa mavazi rasmi ya harusi kwa wageni
wote, lakini mtu huyu aliyakataa.)
a. Hebu tuangalie mantiki hapa.
Mwishoni mwa fungu la 12 linatuambia
kuwa mtu yule “alitekewa.” Je, tunaweza
kuongezea kweli zipi nyingine? (Mfalme
hana makosa. Ikiwa mfalme aliwatoza fedha
kwa ajili ya kupata mavazi maalumu, ikiwa
mavazi hayo hayakuwatosha, ikiwa mtu yule
hakufahamu lolote kuhusu mavazi
maalumu, basi angetoa kisingizio. Kwa
namna fulani alidhani kwamba alikuwa
sahihi kuyakataa mavazi ya mfalme.)
b. Jambo gani linaweza kuwa
lilimfanya mtu huyu adhani kuwa yuko
sahihi kukataa kuvaa vazi maalumu la
harusi lililotolewa na mfalme? (Aliyapenda
mavazi yake zaidi. Hakuhitaji ukarimu wa
mfalme, alikuwa mtu mwenye kujali sana
suala la mavazi.)
(1) Vipi kuhusu wewe? Je,
unajivunia kazi zako?
E. Soma Mathayo 22:13. Jambo
gani linamtokea mtu huyu? (Anafungwa na
kutupwa gizani.)
1. Hebu tujikite mwishoni mwa
fungu hili. Hisia gani zinasababisha kulia
na kusaga meno? (Ilikuwa rahisi sana
kuyakubali mavazi ya mfalme. Anawezaje
kufanya kosa kama hilo katika kufanya
uamuzi?)
F. Soma Mathayo 2:14. Tuliona
kuwa kila aliyetajwa kwenye kisa
alikaribishwa. Yesu anamaanisha nini kwa
kusema “wateule ni wachache?” Mtu mmoja
pekee ndiye anayeonekana kushangaa
kuikosa harusi. (Jibu pekee lenye mantiki ni
kwamba Yesu anarejea (anazungumzia)
uchaguzi binafsi. Wageni wote walioalikwa
waliukataa mwaliko wa mfalme kwa sababu
walikuwa na shughuli nyingi sana kiasi cha
kushindwa kuwa wasikivu. Hawakuwa
marafiki wa mfalme. Kwa dhahiri
hawakutaka kuja harusini kwa sababu
waliwatendea vibaya watumwa wake.)
G. Rafiki, vipi kuhusu wewe? Je,
una shughuli nyingi sana, maisha
yamekusonga sana kiasi cha kushindwa
kushughulikia mwaliko wa kumpokea na
kumkubali Yesu kama Bwana na Mwokozi
wako? Au, je, u miongoni mwa watu
wachache wanaodhani kwamba haki yao
inatosha kabisa? Kwa nini usiwe msikivu,
ukatubu na kulipokea vazi la haki ya Yesu
sasa hivi?

Lessoni juma hili

Utangulizi: Jeffrey Brauch, aliyekuwa Mkuu
wa Shule ya Sheria katika Chuo Kikuu cha
Regent, ni mmojawapo wa watu wa pekee
sana niliowahi kukutana nao. Mara zote
alionekana kuyaelekeza mawazo yake yote
kwangu tulipokuwa tukizungumza.
Ninapokuwa ninazungumza na watu
wengine, ninasikitika kwamba kwa ujumla
huwa ninawaza mambo yangu. Nina
uhakika anaenenda vivyo hivyo kwa kila
mtu – kwamba anayaelekeza mawazo yake
yote kwa watu anaozungumza nao. Jeff
anayaishi yale ambayo Mathayo
anayafundisha juma hili: kuishi maisha ya
kuwajali watu wengine. Hebu tuchimbue
somo letu ili tujifunze zaidi!
I. Watoto
A. Soma Mathayo 18:1-4. Nani
aliye na mawazo yenye msimamo thabiti
kuhusu malezi ya watoto: wazazi wenye
watoto kadhaa au watu wasio na watoto?
1. Je, watoto unaowafahamu ni
wabinafsi kwa asili? Je, huwa
wanajipendelea wao wenyewe kuliko watu
wengine? (Kutokana na kile nilichokiona,
watoto wanafanana nasi tu – wamezaliwa
dhambini.)
2. ikiwa hilo ni kweli, je, Yesu
anazungumzia jambo gani?
B. Soma tena Mathayo 18:1. Kwa
nini mtu atake kuwa mkuu katika ufalme
wa mbinguni? (Ili aweze kuwatawala watu
wengine.)
1. Je, watoto hawako hivyo?
(Watoto wadogo ni tegemezi kwa kiwango
cha juu sana. Hata kama wana tabia
nyingine mbaya, kwa mfano kuwa wachoyo/
wabinafsi, bado wanahitaji msaada na
wanalitambua hilo.)
C. Angalia tena Mathayo 18:4.
Yesu anatuambia nini basi kuhusu tabia
njema? (Kwamba tunatakiwa
kujinyenyekeza kwake na kumtegemea yeye
– kama mtoto anavyowategemea wazazi
wake.)
D. Soma Mathayo 18:5-6. Hili
linahusianaje na alichokimaanisha Yesu
kuhusu watoto kuwa tegemezi? (Kwa kuwa
watoto ni tegemezi, watu wazima wana
wajibu wa kuhakikisha kwamba
wanawafundisha vizuri na kuwatendea
watoto vyema kwa mujibu wa ushawishi
wetu mzuri.)
II. Dhambi
A. Soma Mathayo 18:7. Je,
umewahi kumsikia mtu anayenufaika
kutokana na msemo wa kiovu kwamba,
“Nisingefanya hivyo mtu mwingine
angefanya. Nami pia naweza kuwa
mmojawapo wa watu wanaopata fedha
kutokana na kitendo hicho.”
1. Jibu la Yesu kwa swali hilo ni
lipi? (“Ole wako!” uovu utakuja, lakini
ingekuwa heri uovu huo usitokane nawe
(usipitie kwako).)
B. Soma Mathayo 18:8-9. Je,
dhambi inaanzia mkononi mwako, mguuni
mwako au kwenye jicho lako? (Hapana.
Dhambi inaanzia akilini (mawazoni).)
1. Unakielewa kile anachokisema
Yesu? (Yesu anabainisha madhara ya
dhambi. Watu wanatenda dhambi kutokana
na wanachodhani ni manufaa yatokanayo
na vitendo hivyo vya dhambi. Yesu anasema
ni heri kupoteza kitu cha muhimu kuliko
kutenda dhambi.)
C. Soma Mathayo 18:10. Je, Yesu
anazuga kwa kuyazungukazunguka maoni
yake, na amerukia tena kuwazungumzia
watoto? (Yesu yupo kwenye mada ile ile.
Hatimaye watoto watakabiliana na dhambi,
lakini ni heri dhambi hiyo isipitie kwako.)
D. Soma Mathayo 18:12-14.
Yumkini umewahi kusikia kisa cha kondoo
tisini na kenda na kondoo mmoja
aliyepotea. Yesu anamaanisha nini kwenye
huo mfano wa watoto? (Katika tamaduni
nyingi watoto hawathaminiwi. Katika baadhi
ya tamaduni watoto wanatumikishwa. Yesu
anatufundisha kuwa watoto wana thamani
kubwa sana – kila mmoja wao.)
E. Soma Mathayo 18:15-17. Lengo
la kushugulikia tofauti zetu na matatizo kwa
kutumia njia hii ni lipi? (Lengo ni kumfanya
mtu huyo asikilize na kutafakari.)
1. Inamaanisha nini
kumchukulia mtu kama “mpagani au mtoza
ushuru?”
a. Je, ni sahihi kuwatendea
wapagani tofauti?
III. Kanisa
A. Soma Mathayo 18:18.
Tumejadili suala la kupeleka mashauri ya
watu kanisani. Uamuzi wa kanisa ni wa
muhimu kwa kiasi gani?
B. Hebu turejee nyuma na
tusome Mathayo 16:18-19. Tulipojifunza
suala hilo kitambo kifupi kilichopita
nililifanya kuwa jambo la kiroho kwa
kusema kuwa wale wanaoelewa kwamba
Yesu ni Mungu na kumpokea
“wanafunguliwa” na wale wanaomkataa
“wanazuiliwa” mbingui. Je, sikuwa sahihi?
(Huu muktadha mpya unaonesha kuwa
sikuingia kwa kina zaidi kwenye suala la
matumizi ya dhana hiyo kivitendo. Yesu
anatuambia kuwa kanisa limepewa
mamlaka ya kiroho hapa duniani.)
1. Mamlaka haya yana ukomo
gani? Je, kanisa linaweza kubadili siku ya
ibada? Je, kanisa linaweza kumbadilisha
Yesu na kutupatia mwombezi/mpatanishi
mbadala? (Muktadha uliopo katika Mathayo
18 unazungumzia mfarakano kati ya
washiriki wa kanisa.)
C. Soma Mathayo 18:19-20.
Kanisa linatakiwa kuwa kubwa kiasi gani ili
liweze kuwa na aina ya mamlaka ambayo
tumekuwa tukiyajadili? Je, kanisa la watu
wawili linatosha?
1. Unapokaa na kuyatafakari
mafungu haya, unadhani ni jambo gani la
msingi analolimaanisha Yesu? (Mbingu
zinafanya kazi kupitia kwetu. Mungu
anatupatia mamlaka.)
2. Je, hili linahusiana kwa
vyovyote vile na mjadala wa Yesu uliopita
kuhusu watoto? (Yesu anatufundisha kuwa
wanyenyekevu na kumtegemea. Hiyo
inabainisha kiwango cha “mamlaka” yetu
hapa. Mamlaka yetu yanatakiwa kuendana
na mapenzi ya Yesu yaliyobainishwa. Hii
inamaanisha kwamba kanisa halipaswi
kuweka sheria zinazokinzana na
mafundisho makuu ya Mungu. Kwa kuwa
tunayo haya mamlaka, tunatakiwa kuwa
makini sana jinsi tunavyoyatumia.)
IV. Msamaha
A. Soma Mathayo 18:21-22.
Namna pekee ya kuwa na uhakika kwamba
tunazo mara sabini na saba ni kwa
kuandika. Je, haya ndio maelekezo ya Yesu
kwetu?
B. Soma Mathayo 18:23-30.
Unamchukuliaje mtu ambaye alikuwa
anadaiwa mamilioni kutomsamehe mdeni
wake aliyekuwa akimdai kiasi kidogo?
C. Soma Mathayo 18:31.
Mashuhuda walisikitika, kama jinsi
ulivyosikitika! Je, ni kwa sababu mtu
aliyewiwa deni dogo hakusamehewa mara
saba, achilia mbali mara sabini na saba?
D. Soma Mathayo 18:32-33.
Bwana anasema kuwa tatizo ni lipi?
(Rehema. Sio kuendeleza kile
anachokiamrisha Yesu, bali ni kuwa na
rehema kwa wale wanaoomba msamaha.)
1. Kipimo cha msahama
maishani mwako ni kipi? (Yesu alikufia kwa
ajili ya dhambi zako. Dhambi yako i
kinyume na Mungu. Tunaathiriwa na
dhambi, lakini kuvunja sheria ya Mungu ni
dhambi dhidi yake. Sisi ndio yule mtumwa
aliyesamehewa “mamilioni.”)
E. Soma Mathayo 18:34-35. Yesu
anatoa onyo gani?
1. Inamaanisha nini “kusamehe
… kutoka moyoni?”
V. Ndoa
A. Soma Mathayo 19:3-6. Je, Yesu
anaamini maelezo ya uumbaji? (Anayaamini
kwa uthabiti mkubwa kiasi kwamba
anajenga hitimisho la kiroho kutokana na
maelezo ya uumbaji.)
B. Soma Mathayo 19:7-9. Je,
unadhani ni kama ajali tu kwamba huu
mjadala wa ndoa mara moja unaufuatia
mjadala kuhusu msamaha?
1. Je, mjadala wa ndoa
unaboreshaje uelewa wetu wa suala la
msamaha? (Ikiwa mara zote mwenzi
anatakiwa kumsamehe mwenzi wake, basi
hatupaswi kuwa na talaka. Hii inatuonesha
kuwa rehema inatokana na mpango wa
Mungu kwa ajili ya ndoa na maisha.)
2. Je, mwenzi anaweza kusamehe
“kutoka moyoni” kitendo cha mwenzi wake
kutokuwa mwaminifu, na bado akataliki
kutokana na kutokuwepo kwa uaminifu?
(Ndiyo. Msamaha haumaanishi kutelekeza
(kutotumia) akili ya kawaida.)
C. Soma Mathayo 19:10. Baadaye
katika sura hii ya kitabu cha Mathayo Yesu
anasema kuwa ni vigumu kwa tajiri
kuokolewa. Soma Mathayo 19:25. Wanafunzi
wa Yesu wanayachukuliaje mafundisho
yake? (Wanashangaa. Kwao kitendo hicho
hakionekani kuwa sahihi. Haiwaingii akilini
kutokana na uelewa wao juu ya mapenzi ya
Mungu.)
D. Soma Mathayo 19:11-12 (ndoa)
na Mathayo 19:26 (utajiri). Yesu anatoa
maoni gani kuhusu mafundisho ambayo ni
magumu kuyaelewa na kuyafuata? (Kwamba
Mungu atatenda kazi pamoja nasi ili
kuyafanya mambo yanayoonekana kuwa
hayawezekani yawezekane.)
VI. Ujira
A. Soma Mathayo 20:1-12. Je,
unakubaliana na wale wanaonung’unika?
Jiweke kwenye nafasi ya wale waliofanya
kazi kutwa nzima!
B. Soma Mathayo 20:13-16. Ikiwa
Yesu anatufundisha somo kuhusu Ufalme wa
Mbinguni, na sio ujira, je, kuna kipi cha
kujifunza? (Mungu haangalii usawa tu. Yeye
ndiye usawa. Lakini, yeye ni zaidi ya usawa.
Anatupatia kile tunachostahili, na anatupatia
zaidi ya tunachostahili. Anafanya mambo
yasiyowezekana yawezekane.
C. Rafiki, Mungu anakujali.
Anawajali watoto tegemezi. Anatutaka tuwe
mbaraka kwa watu wengine, badala ya
kutafuta tu kile tunachodhani kuwa ni
usawa.
VII. Juma lijalo: Yesu Akiwa
Yerusalemu.

Ijumaa, 27 Mei 2016

Kanuni za Kanisa la Sda

Waadventista wasabato huipokea Biblia kama
kanuni yao pekee na hushika baadhi ya
misingi ya imani kuwa ndiyo mafundisho ya
mabadiliko matakatifu . Imani hizi , kama
zilivyoorodheshwa hapa , hufanya welekevu
wa kanisa na udhihirisho wa mafundisho ya
mabadiliko. Masahihisho ya kauli hizi
yanaweza kutegemewa katika kikao cha
Halmashauri
kuu wakati kanisa likiongozwa na Roho
Mtakatifu kwenye ufahamu ulio kamili zaidi
ya
ukweli wa Biblia au linapopata lugha iliyo
bora zaidi ya kuelezea mafundisho ya Neno
Takatifu la Mungu.
1. Maandiliko Matakatifu
Maandiko Matakatifu , yaani Agano la kale na
Jipya ndiyo Neno la Mungu lililoandikwa,
likatolewa kwa uvuvio wa Mungu, kupitia
kwa watu watakatifu walionena na kuandika
kama
walivyoagizwa na Roho Mtakatifu. Ndani ya
neno hili , Mungu amemkabidhi mwanadamu
maarifa yaliyo lazima kwa ajili ya wokovu.
Maandiko matakatifu ni ufunuo usioweza
kukosa
wa mapenzi yake . Ndiyo upeo wa tabia ,
kipimo cha uzoefu , ufunuo thabiti wenye
mamlaka
wa mafundisho ya imani, na kumbukumbu
aminifu ya matendo ya mungu katika historia.
( 2 Petro 1 : 20 ,21 . 2 Timotheo 3: 16 , 17 . Zaburi
119: 105. Mithal 30 : 5, 6. Isaya 8: 20 . Yoh
17 : 17 . 1Wathe 2: 13 . Waeb 4 : 12 . )
2. Utatu Mtakatifu
Kuna Mungu mmoja : Baba , Mwana, na Roho
Mtakatifu, umoja wa nafsi tatu za milele.
Mungu hapatikani na mauti , mwenye nguvu
zote , ajuaye yote, zaidi ya yote, na aliyeko
daima . Yeye hana mwisho na ni zaidi ya
ufahamu wa kibinadamu , hata hivyo
anafahamika
kupitia kujifunua kwake binafsi . Milele zote
yu astahili kuabudiwa , kusujudiwa ,
kutumikiwa
na viumbe vyote . ( kumb 6 : 4 . Mith 28 : 19 . 2 kor
13 : 14 . Waef 4 : 4 -6 . 1Petr 1 : 2 1 Tim 1: 17
Ufunuo 14 : 7 )
3. Baba
Mungu Baba wa milele ndiye muumbaji ,
Chimbuko , Mtengenezaji , na Mfalme wa
viumbe
wote . Ni mwenye haki na Mtakatifu , Mwingi
wa rehema ,, mwenye fadhili , si mwepesi wa
hasira, na mwingi wa uthabiti wa upendo na
uaminifu . Tabia na uwezo vilivyodhihirishwa
ndani ya Mwana na Roho Mtakatifu pia ni
ufunuo wa Baba . ( Mwanzo 1 : 1 Ufu 4: 11 .
1wakor 15 : 28 . Yoh 3 : 16 . 1 Yoh 4: 8. 1 Tim 1: 17 .
Kut 34 : 6 ,7 . Yoh 14 : 9) .
4. Mwana
Mungu Mwana wa milele alifanya mwili
katika Yesu Kristo. Kupitia kwake vitu vyote
viliumbwa , tabia ya mungu imefunuliwa ,
wokovu wa wanadamu unakaribishwa na
ulimwengu unahukumiwa . Milele zote Mungu
kweli, Alifanyika mwanadamu kweli, Yesu
aliye kristo. Alichukuliwa mimba kwa uwezo
wa Roho Mtakatifu na kuzaliwa na bikira
Mariamu . Akaishi na kupitia uzoefu majaribu
kama mwanadamu , lakini kwa ukamilifu
alioonyesha kwa mfano wa haki na u [ endo
wa Mungu. Kwa miujiza yake alidhihirisha
uwezo wa Mungu na alithibitishwa kama
Masihi aliyeahidiwa. Aliteseka na kufa kwa
hiari
msalabani kwa ajili ya dhambi zetu , na kama
mbadala wetu , Alifufuliwa kutoka kwa wafu ,
na akapaa kuhudumu katika hekalu la
mbinguni kwa niaba yetu. Atakuja tena katika
utukufukwa ajili ya ukombozi wa mwisho wa
watu wake na urejeshwaji wa vitu vyote . ( Yoh
1: 1 -3 ,14 . Wakol 1: 15 - 19 , . Wafil 2 : 5 -11 . Yoh
10 : 30 , 14 : 9 Warum 6 : 23 . 2Wakor 5: 17 -19 .
Yoh 5 : 22 . 1Wakor 15 : 3 ,4 . Luka 1 : 35 . Yoh
14 : 1 - 3)
5. Roho Mtakatifu
Mungu Roho wa milele alikuwa mtendaji
pamoja na Baba na Mwana katika uumbaji ,
kufanyika mwili , na katika ukombozi .
Aliwavuvia waandishi wa mabadiliko
matakatifu .
Alijaza maisha ya kristo na uwezo . Huwavuta
na kuwasadikisha wanadamu , na wale
wanaoitikia huwafanya upya na
kuwabadilisha katika sura ya Mungu.
Akipelekwa na Baba
na Mwana ili kuwa siku zote pamoja na
watoto wake, hutoa karama za kiroho kwa
kanisa ,
huliwezesha kumshuhudia kristo, na kwa
upatano wa maandiko uliongoza kwenye
ukweli
wote . ( Mwa 1 ,2 . Luka 1: 35 , 4 : 18 . Mdo 10 : 38 .
2Petr 1 : 21 . 2 Wakor 3 : 18 . Yoh 14 : 16 -18 , 26 ,
15 : 26 ,27 , 16 : 7 -13 )
6. Uumbaji
Mungu ni muumba wa vitu vyote , na
amefunua katika maandiko uhalisi wa tukio
la
shughuli zake za uumbaji . Katika siku sita
Bwana alizifanya “ Mbingu na Nchi ” na vitu
vyote
vilivyoko hai juu ya nchi, akastarehe siku ya
saba ya juma lile la kwanza . Na hivyo
akaanzisha sabato kama kumbukumbu ya
milele ya kukamilika kwa kazi yake ya
uumbaji.
Mwanaume na Mwanamke wa kwanza
walifanywa kwa mfano wa Mungu kama upeo
wa
kazi yake ya Uumbaji , wakapewa utawala juu
ya ulimwengu , na wakaagizwa kuajibika na
utunzaji wake. Wakati ulimwengu
ulipomalizika kila kitu kilikuwa “ ni chema
sana ”
ukitangaza utukufu wa Mungu. ( Mwa 1 ,2 .
Kut20 : 8 - 11 . Zab 19 : 1 -6 , 33 : 6 -9 , 104. Waebr
11 : 3 )
7. Asili ya Mwanadamu
Mwanaume na Mwanamke walifanyawa kwa
mfano wa Munguwakiwa kila mmoja na nafsi
yake, uwezo na uhuru wa kufikirina kutenda .
Ingawa waliumbwa viumbe huru , kila mmoja
ni umoja wa nafsi isiyogawanyika ya mwili ,
akili na roho, akimtegemea Mungu kwa uhai
na
pumzi na mengine yote. Wakati wazazi wetu
wa kwanza walipomwasi Mungu, walikana
utegemezi wao kwa Mungu na wakaanguka
kutoka hadhi yao ya juuchini ya Mungu. Sura
ya Mungu iliyopo ndani yao ikaharibika na
wakawa chini ya mauti . Wazao wao hushiriki
asili hii ya kuanguka na matokeo yake.
Wanazaliwa wakiwa na udhaifu na mivuto ya
kuelekea kwenye uovu . Lakini Mungu katika
kristo aliupatanisha ulimwengu na nafsi yake ,
na kwa Roho wake hurejesha ndani ya
mwanadamuwatubuo sura ya muumba wao .
Wakiwa wameumbwa kwa ajili ya utukufu
wa Mungu, wanaitwa kumpenda na
kupendana
wao kwa wao na kutunza mazingira yao.
( Mwa 1 : 26 -28 , 2 : 7 . Zab 8 : 4- 8. Mdo 17 : 24 - 28 .
Mwa
3. Zab 51 : 5 War 5 : 12 : 17 . 1Yoh 4 : 7 ,8 ,11 , 20 .
Mwa 2 : 15
8. Pambano kuu
Jamii yote ya wanadamu sasa inahusika
katika pambano kuu baina ya kristo na
shetani
kuhusu tabia ya Mungu, sheria yake , na
utawala wake juu ya ulimwengu . Ugomvi huu
ulianza mbinguni wakati kiumbe aliyeumbwa
na kutunukiwa uhuru wa kuchagua , katika
kujiinua akawa shetani , mpinzani wa Mungu,
na kupelekea sehemu ya Malaika kwenye
uasi . Akaiagiza Roho ya uasi katika
ulimwengu huu pale alipowaongoza Adamu
na Hawa
kingia dhambini. Dhambi hii ya mwanadamu
ilileta matokeo ya upotoshaji ya sura ya
Mungukatika wanadamu , Uvurugaji wa
ulimwengu ulioumbwa , na mwishowe
kuteketea
wakati wa gharika iliyokumba ulimwengu
wote . Ukitazamwa na viumbe wote
ulimwengu
huu ukawa uwanja wa vita ya ulimwengu,
ambao kutokana nao Mungu wa upendo
hatimaye akathibitika kuwa mwenye haki .
Katika kuwasaidia watu wake katika pambano
hili , kristo anamtuma Roho Mtakatifu na
malaika watiifu kuongoza , kulinda , na
kutegemeza katika njia ya wokovu . ( Ufu
12 : 4 - 9, Isa 14 : 12 - 14 , Eze 28 : 12 - 18 , War
1: 19 - 32 ,
5: 12 - 21 , 8: 19 - 22 , 1Wakor 4: 9, Waeb 1 : 14 )
9. Maisha, Mauti na Ufufuo wa kristo
Katika maisha ya kristo ya utii mtakatifu kwa
mapenzi ya Mungu, mateso yake , mauti na
ufufuo , Mungu alitoa njia pekee ya kafara
kwa ajili ya dhambi ya mwanadamu , ili
kwamba
wale ambao kwa imani wanapokea
upatanisho huu waweza kuwa na uzima wa
milele, na
ulimwengu wote uweze kuelewa vizuri
upendo mtakatifu usio na kikomo wa
muumba.
Kafara hii kamilifu huthibitisha haki ya
sheria ya mungu na fadhili za tabia yake , kwa
sababu hufanya vyote viwili kuhukumu
dhambi zetu na kutupatia msamaha . Kifo cha
kristo
ni cha badala na cha kulipia, kupatanisha na
chenye kubadilisha . Ufufuo wa Yesu kristo
hutangaza ushindi wa Mungu dhidi ya nguvu
za uovu , na kwa wale wanaopokea kafara
huakikisha ushindi wao wa mwisho dhidi ya
dhambi na mauti . Kinatangaza ukuu wa Yesu
Kristo, ambaye mbele zake kila goti mbinguni
na duniani litapigwa . ( Yoh 3 : 16 , Isa 13 : 1,
1Petr 2 : 21 , 22 ,1 Wakor 15 : 3 , 4 , 20 -22 , 2Wakor
5: 14 , 19 - 21 . War1 : 4 , 3 : 25 , 4 : 25 , 8 : 3 , 4,
Wafil2: 6 -11 )
10 . Uzoefu wa Wokovu
Katika upendo usio na mwisho na rehema
zake Mungu alimfanya Kristo , asiyejua
dhamdi
kuwa dhambi kwa ajili yetu , ili kwambakatika
yeye tuweze kufanywa haki ya Mungu.
Tukiongozwa na Roho mtakatifu tunatambua
hitaji letu, tunakili hali yetu ya kuwa wenye
dhambi , tunatubu maasi yetu , na kuonyesha
imani katika Yesu kama Bwana na Kristo ,
kama mbadala na kielelezo. Imani hii
inayopokea wokovu huja kupitia katika uwezo
wa
kimbingu wan a ni karama ya neema ya
Mungu. Kupitia kwa kristo tunahesabiwa
haki ,
tunafanywa kuwa wana wa binti za Mungu,
na kukomesabiwa haki kutoka katika hali ya
kuwa chini ya dhambi . Kupitia kwa Roho
tunazaliwa upyana kutakaswa , Roho
hufanywa
upya nia zetu , huandika sheria ya Mungu ya
upendo katika mioyo yetu , na tunapewa
uwezo
wa kuishi maisha matakatifu . Tukikaa ndani
yake tunakuwa washiriki wa asili ya uungu
na
tuna hakika ya wokovu sasa na katika
hukumu . ( 2 Wakor 5 : 17 - 21 , Yoh 3 : 16 , Wag 1 : 4 ,
4: 4-
7, Tito3 : 3 -7 , Yoh 16 : 8 , Wag 3 : 13 , 14 . 1 Petr
2: 21 ,22 . Warumi 10 : 17 , 3 : 21 -26 , 8 : 14 -17 , 12 : 2 .
Warumi 8 : 1- 4, 5: 6- 10 , 2 Petr 1 : 3, 4)
11 . Kukua katika kristo
Kwa kifo chake msalabani Yesu alizishinda
nguvu za uovu . Yeye aliyewatiisha pepo
wachafu wakati wa huduma yake hapa
duniani amezivunja nguvu zao na
kuthibitisha
mwisho wao ni uangamivu usioepukika .
Ushindi wa Yesu utupatia ushindi dhidi ya
nguvu
za uovu ambazo bado zinatafuta kututawala ,
tunapo tembea naye kwa amani, fyraha , na
uhakika wa upendo wake. Sasa Roho Mtakatifu
anakaa ndani yetu na kututia nguvu .
Tukidumu kujikabidhi kwa Yesu kama Bwana
na mwokozi wa maisha yetu tunawekwa
huru kutoka katika mzigo wa matendo yetu
yaliyopita . Hatuishi tena gizani , katika hofu
ya
nguvu za uovu , ujinga , na katika kukosa
maana kwa namna ya maisha yetu ya awali, .
Katika
uhuru huu mpya ndani ya kristo, tumeitwa
kukua katika kufanana na tabia yake ,
tukiongea
naye kila siku katika sala , na kujilisha neno
lake kikamilifu , tukikusanyika pamoja kwa
ajili
ya ibada , na kushiriki katika utume wa
kanisa . Tukijitoa katika kuwahudumia kwa
upendo
wale wanaotuzunguka na kuwashuhudia
wokovu wake, kuwepo kwake nasi daima kwa
njia
ya Roho hugeuza kila wasaa na kazi kuwa
uzoefu wa kiroho . ( Zab. 1: 1, 2. 23 : 4 , 77 : 11 ,12 ,
Kol 1: 13 -14 , 2: 6, 14 - 15 , Luka 10 : 17 -20 ,
Efe5 : 19 -20 , 6 : 12 -18 , 1 Theo 5 : 23 , 2Petr 2 : 9 ,
3: 18 .
Fil3 : 7 -14 , Math 20 : 25 -28 , Yoh 20 : 21 ,
Gal 5: 22 - 25 , Rum 8 : 38 - 39 , 1Yoh 4: 4, Ebr10
12 . Kanisa
Kanisa ni jamii ya waumini wanaomkiri Yesu
kristo kuwa bwana na mwokozi katika
mfululizo wa kufungamana na watu wa
Mungu katika nyakati za agano la kale,
tunaitwa
kutoka katika ulimwengu, na tunajiunga
pamoja kwa ajili ya ibada , kwa ajili ya
ushirika, kwa
ajili ya mafundisho katika neno , na kwa ajili
ya maadhimisho ya meza ya bwana , kwa ajili
ya
huduma kwa wanadamu wote , na kwa ajili ya
tangazo la injili ulimwenguni kote , kanisa
linapata mamlaka yake kutoka kwa kristo,
aliye neno lililofanyika mwili , na kutoka
katika
maandiko, ambayo ndiyo neno lililoandikwa.
Kanisa ni jamaa ya Mungu, waliofanywa nay
eye kuwa watoto wake, washiriki wake huishi
katika misingi ya agano jipya . Kanisa ni mwili
wa Kristo, jamii ya weny imani ambayo kristo
mwenyewe ndiye kichwa. Kanisa ni bibi arusi
ambaye kwa ajili yake kristo apate kulisafisha
na kulitakasa . Wakati wa kurudi kwake kwa
ushindi, ataliwasilisha kwake mwenyewew
kanisa lenye utukufu , waaminifu wa karne
zote ,
walionunuliwa kwa damu yake , lisilo na waa
au kunyanzi , lakini takatifu na lisilo na
ila . ( Mwa 12 : 3, Mdo : 7 : 38 , Waef 4 : 11 -15 , 3 : 8 -11 ,
Math 28 : 19 ,20 , 16 : 13 - 20 , 18 : 18 ,
Waef 19 : 22 ,23 , 5 : 23 -27 , Wakol 1 : 17 - 18 ) .
13 . Masalio na Utume Wake
Kanisa la ulimwengu lijumuisha wale wote
ambao kwa kweli wanamwamini kristo, lakini
katika siku za mwisho , kipindi cha kuenea
kwa ukengeufu , masalio wameitwa kuzishika
amri za Mungu na imani ya Yesu kristo .
Masalio hawa hutangaza kuwadia kwa saa ya
hukumu , hutangaza wokovu kupitia kristo, na
hupiga mbiu ya kukarinia kwa marejeo yake .
Tangazo hili huwakilishwa katika mfano wa
malaika watatu wa ufunuo 14 , juambatana na
kazi ya hukumu mbinguni na kuwa na
matokeo ya kazi ya toba na matengenezo
duniani .
Kila muumini anatakiwa kuwa na sehemu
binafsi katika ushuhuda huu wa ulimwenguni
kote . ( Ufu 12 : 17 , 14 : 6 -12 , 18 : 1 -4 , 2Wakor 5: 10 ,
Yuda 3, 14 , 1Petro1 : 16 -19 , 3 : 10 -14 ,
Ufu 21 : 1- 14 )
14 . Umoja katika Mwili wa Kristo
Kanisa ni mwili mmoja ulio na washiriki
wengi, walioitwa kutoka katika taifa , kabila ,
lugha,
na watu. Katika kristo tu viumbe wapya ,
ubainishi wa rangi, tamaduni , elimu , na taifa ,
na tofauti kati ya tabaka ya juu nay a chini ,
tajiri na maskini , mwanaume na
mwanamke , havipaswi kuleta mgawanyiko
miongoni mwetu . Sote tu sawa katika kristo,
ambaye kwa roho mmoja ametufunga katika
ushirika mmoja pamoja nay eye na sisi
wenyewe kwa wenyewe, tunapaswa kutumika
na kutumikiwa pasipo kupendelea au kusita.
Kupitia kwa Yesu kristo katika maandiko
tunashiriki imani na tumaini moja , na
tunawafikia
wote kwa ushuhuda mmoja . Umoja huu una
chimbuko lake katika umoja wa Mungu
mmoja mwenye nafsi tatu , ambaye
ametufanya sisi tu watoto wake. ( War12 : 4 ,5 ,
1Wakor 12 : 12 - 14 , Math 28 : 19 ,20 , Zabr133: 1,
2Wakor 5 : 16 ,17 , Mdo 17 : 26 ,27 , Waef 4 : 14 -16 ,
4: 1- 6 , Yoh 17 : 20 -23 )
15 . Ubatizo
Kwa njia ya ubatizo tunakiri imani yetu
katika kifo na ufufuo wa Yesu kristo, na
kushuhudia kufia kwetu dhambi na kusudi
letu la kuenenda katika upya wa maisha.
Hivyo
tunamkubali kristo kuwa Bwana na Mwokozi ,
tunakuwa watu wake, na tunapokelewa kama
washiriki wa kanisa lake. Ubatizo ni mfano
wa muungano wetu na kristo , msamaha wa
dhambi zetu na kupokea kwetu Roho
Mtakatifu. Ni kwa kuzamishwa najini na
unategemea
uthibitisho wa imani katika yesu na ushindi
wa toba ya dhambi . Unafuata mafunzo katika
maandiko matakatifu na ukubali wa
mafundisho yake . ( Warum 6 : 1 -6 ,
Wakol2 : 12 ,13 ,
Mdo16 : 30 - 33 , 22 : 16 , 2: 38 , Math 28 : 19 -20 )
16 . Meza ya Bwana
Meza ya Bwana ni ushiriki katika mfano wa
mwili na damu ya Yesu kama udhihirisho wa
imani katika yeye , Bwana na mwokozi wetu .
Katika ushirika huu kristo anakuwepo
kukutana na kuwaimarisha watu wake. Kadri
tunavyoshiriki , kwa furaha tunatangaza mauti
ya Bwana mpaka arudipo tena. Maandalizi
kwa ajili ya meza ya Bwana hujumuisha
kujihoji
nafsi, toba na ungamo . Bwana aliamua
huduma ya kutawadhana miguu kumaanisha
kutakaswa upya , kuonyesha nia ya
kutumiana wenyewe kwa wenyewe katika
unyenyekevu
ufananao na wa kristo , na kuungana mioyo
yetu katika upendo . Huduma ya Meza ya
Bwana wazi kwa waumini wote wakristo .
( 1 Wakor 10 : 16 ,17 . 11 : 23 -30 , Math 26 : 17 -30 ,
Ufu 3: 20 , Yoh 6 : 48 -63 , 13 : 1 -17 )
17 . Karamu za Roho na Huduma
Mungu huwakirimia washiriki wote wa kanisa
lake katika kila kizazi karama za kiroho
ambazo kila mshiriki atatumia katika huduma
ya upendo kwa ajili ya mema ya kawaida ya
kanisa na wanadamu . Zikitolewa kwa wakala
wa Roho Mtakatifu , ambaye humgawia kila
mshiriki kama apendavyo yeye , karama hizo
hutoa uwezo wote na huduma zinazohitajiwa
na kanisa katika kuytekeleza shughuli zake
zilizoamuriwa na Mungu. Kulingana na
maandiko huduma hizi hujumuisha huduma
kama : Imani , uponyaji, unabii , mahubiri ,
mafundisho, utawala , upatanisho , huruma , na
huduma ya kujinyima na ufadhili kwa ajili ya
msaada na faraja kwa watu . Baadhi ya
washiriki huitwa na mungu na kukirimiwa na
Roho
kwa ajili ya shughuli zinazotambuliwa na
kanisa katika uchungaji , uinjilisti , na utume,
na
huduma za kufundisha zinahitajika hasa
katika kuwapatia zana washiriki kwa ajili ya
huduma kulijenga kanisa hadi ukomavu wa
kiroho, na kukuza umoja wa imani na
maarifa
ya Mungu. Pale washiriki wanapozitumia
karama hizi za kiroho kama mawakili
waaminifu wa neema mbalimbali za Mungu,
kanisa hulindwa dhidi ya mivuto miharibifu
ya
mafundisho ya uwongo, na hukua kwa ukuaji
unaotoka kwa Mungu, nakujengeka imara
katika imani na upendo . ( Warumi 12 : 4 -8 ,
1Wakor 12 : 9 -11 , 27 ,28 . Waef 4 : 8 ,11 , Mdo 6 : 1 -7 ,
1Petr 4: 10 - 11 )
18 . Karama ya Unabii
Mojawapo ya karama za Roho Mtakatifu ni
unabii, karama hii ni alama -kitambulisho cha
kanisa la masalio na ilidhihirishwa katika
huduma ya Ellen G . White . Kama mjumbe wa
Bwana , maandishi yake ni chanzo kiendelezi
na yenye mamlaka ya ukweli yanayolipatia
kanisa faraja, uongozi, mafundisho , na
maonyo . Pia yanaweka wazi kuwa Biblia
ndiyo
kanuni ambayo kwa hayo mafundisho yote na
uzoefu lazima vipimwe . ( Yoeli 2 : 28 ,29 ,
Mdo2 : 14 -21 , Waeb 1 : 1- 3, Ufu 12 : 17 , 19 : 10 )
19 . Sheria ya Mungu
Kanuni kuu za sheria ya Mungu zimetiwa
pamoja katika Amri kumi na mfano wake
ulidhihirishwa katika maisha ya kristo,. Nazo
zinadhihirisha upendo wa Mungu, mapenzi
yake, na makusudi yake kuhusu mwenendo
wa binadamu na mahusiano nazo ni sharti
kwa
watu wote katika kila kizazi. Amri hizi ndiyo
msingi wa agano la Mungu na watu wake na
kanuni katika hukumu ya Mungu. Kupitia
uwakala wa Roho Mtakatifu zinasonda
dhambi
na kuhamsha hisia za hitaji la mwokozi .
Wokovu wote ni katika neema, na si kwa
matendo ,
lakini tunda lake ni utii wa amri kumi . Hutii
huu hukuza tabia ya kikristo na huwa na
matokeo ya ustawi . Ni ushuhuda wa upendo
wetu kwa Bwana na wajibu kwa ajili ya
wanadamu wenzetu . Utii wa imani
udhihirisha uwezo wa kristokubadilisha
maisha, na
hivyo huimarisha ushuhuda wa kristo. ( Kut
20 : 1 - 17 , Zab40 : 7, 8 Math 22 : 36 -40 Kumb28 : 1 -
14 Math 5 : 17 -20 , War 8 : 3 ,4 Zab 19 : 7 - 14 )
20 . Sabato
Muumbaji mkarimu, baada ya siku sita za
uumbaji, alipumzika siku ya saba na
kuanzisha
sabato kwa ajili ya watu wote kama
kumbukumbu ya uumbaji . Amri ya nne ya
sheria za
Mungu zisizobadilika inaagiza adhimisho la
sabato hii ya siku ya saba kama siku ya
mapumziko , ibada , na huduma kulingana na
mafundisho na uzoefu wa Yesu , Bwana wa
sabato. Sabato ni siku ya mawasiliano yenye
furaha pamoja na Mungu na sisi kwa sisi . Ni
mfano wa ukombozi wetu katika kristo ,
ishara ya utakaso wetu , ishara ya utii wetu ,
na
mwonjo wa umilele wetu wa siku zijazo
katika ufalme wa Mungu. Sabato na ishara ya
daima
ya mungu ya agano la milele la Mungu kati
yake na watu wake. Utunzaji wa furaha wa
wakati huu mtakatifu toka jioni hadi jioni, jua
kuchwa hadi jua kuchwa, ni adhimishola
matendoya Mungu ya uumbaji na ukombozi .
( Mwa 2 : 1 - 3, Kut20 : 8- 11 , Luka 4 : 16 , Isay56 : 5 -
6, 58 : 13 - 14 , Math 12 : 1- 12 , Ezek20 : 12 -20 ,
Kumb5 : 12 -15 , Wal23 : 32 , Marko 1 : 32 ) .
21 . Uwakili
Sisi tu mawakili wa Mungu, tuliokabidhiwa
nay eye wakati na fursa , uwezo na mali , na
mibaraka ya dunia na raslikamali zake .
Tunawajibika kwake kwa matumizi yake
sahihi.
Tunakiri umilikaji wa Mungu kwa huduma ya
uaminifu kwake na kwa wanadamu wenzetu ,
na kwa kurudisha Dhaka na kutoa sadaka
kwa ajili ya utangazaji wa injili yake na kwa
utegemezaji na ukuaji wa kanisa lake .
Uwakili ni fursa iliyotolewa kwetu na Mungu
kwa ajili
ya malezi katika upendo na ushindi dhidi yao
choyo na tama . Wakili kufurahia mibaraka
inayowajia wengine kama matokeo ya
uaminifu wake. ( Mwa 1 : 26 -28 , 2 : 15 ,
1Nyak 29 : 14 ,
Hagai 1 : 3 - 11 , Malak 3 : 8 -12 , 1Wakor 9: 9- 14 ,
Math 23 : 23 , 2Wakor 8 : 1 -15 Warumi 15 : 26 - 27 . ) .
22 . Mwenendo wa kikristo
Tumeitwa kuwa watauwa wanaofikiri ,
kujisikia , na kutenda kutenda kulingana na
kanuni za
mbinguni. Ili Roho aumba ndani upya ndini
yetu tabia ya Bwana wetu tunajihusisha tu
katika mambo yale ambayo yatazaa katika
maisha yetu usafi unaofanana na kristo , afya ,
na
furaha katika maisha yetu . Hii inamaanisha
kwamba maraha na maburudisho yetu
yanapaswa kufikia viwango vikuu vya maonji
na uzuri wa kikristo . Huku tukitambua
tofauti
za kitamaduni , mavazi yetu yanapaswa yawe
ya kawaida , si ya anasa , na safi, yanayostahili
wale ambao uzuri wao wa asili yake si
mapambo ya nje, bali asili yake ni mapambo
yasiyoharibika , yenye roho ya upole na
utulivu . Pia inamaanisha kwamba kwa kuwa
miili
yetu ni maekalu ya Roho mtakatifu,
tunapaswa kuitunza kwa akili . Pamoja na
mazoezi
tosha na mapumziko , yatupasa kuchagua lishe
yenye afya sana kadiri inavyowezekana na
kuepuka vyakula visivyo najisi , vilivyotajwa
katika maandiko matakatifu . Kwa vile
vinywaji
vya vileo , tumbaku na matumizi mabaya ya
madawa hudhuru miili yetu, yatupasa
kuepukana nayo pia. Badala yake yatupasa
kujishughulisha na chochote kile
kitakacholeta
mawazo yetu na miili yetu yawe katika
nidhamu ya kistro, ambaye hutamani uzima
wetu ,
furaha , na wema . ( Warumi 12 : 1 -2 , 1 Yoh 2: 6,
Waef 5: 1; 21 , Wafil 4 : 8 , 2 Wakor 10 : 5, 6 : 14 ,
7: 1, 1 Pet 3: 1- 4 , Walawi 11 : 1 -47 , 3 Yoh . 2)
23 . Ndoa na Familia
Ndoa ilianzishwa Edeni na Mungu na
ikasibitishwa na Yesu kuwa muungano wa
maisha
yote kati ya mwanaume na mwanamke katika
wenzi wenye upendo . Kwa mkristo kifungo
cha ndoa ni kwa Mungu na pia kwa mwenzi ,
na kishirikiwe tu na wenzi wenye imani
moja .
Upendo wa hiari, heshma , staha , na
uwajibikaji ndizo fito za { kujenga } uhusiano
huu,
ambao utaakisi upendo , utakatifu , ukaribu ,
uthabiti wa uhusiano kati ya kristo na kanisa
lake. Kuhusu talaka , Yesu alifundisha
kwamba mtu anayemwacha mwenza ,
isipokuwa kwa
sababu ya uasherati, na akaoa { au kuolewa }
na mwingine azini . Ingawa baadhi ya
mahusiano ya kifamilia huenda yakashindwa
kufikia lengo , wenzi katika ndoa ambazo
wamejitoa kikamilifu kila mmoja kwa
mwenzake katika kristo wanaweza kufaulu
kufikilia
katika umoja wenye upendo kupitia uongozi
wa Roho na malezi ya kanisa . Mungu
hubariki
familia na anakusaidia kwamba washirika
wake watasaidiana wao kwa wao kufikia
upevu
kamili . Wazazi wawalee watoto wao katika
kumpendeza na kumtii Bwana . Kwa kielelezo
chao na maneno yao wawafundishe kwamba
kristo ni mtiishaji mwenye upendo , daima
mpole na mwenye kujali, anayetaka wawe
kiungo katika mwili wake, familia ya Mungu.
Kukuza ukaribu wa mahusiano wa kifamilia
ni moja wapo ya alama{ ya kujulisha } ujumbe
wa
mwisho wa injil. ( Mwa 2 : 18 -25 , Math 19 : 3- 9,
Yoh 2 : 1 -11 , 2Wakor 6 : 14 , Waef 5 : 21 -33 , Luka
16 : 18 , 1Wakor 7 : 10 -11 , Kut20 : 12 , Kumb6 : 5- 9,
Mith22 : 6 , Mal 4 : 5 -6 )
24 . Huduma ya Kristo katika Hekalu la
Mbinguni
Kuna hekalu mbinguni , hema la kweli
lililosimamishwa na Bwana na siyo
mwanadamu .
Ndani yake kristo anahudumu kwa niaba
yetu, akiwezesha kupatikana kwa ajili ya
waumini
fanaka za kafara yake ya upatanisho
iliyotolewa mara moja msalabani kwa ajili ya
wote .
Alizinduliwa kuwa kuhani wetu mkuu na
akaanza huduma yake ya uombezi wakati wa
kupaa kwake mbinguni. Mnamo mwaka 1884 ,
mwishoni mwa kipindi cha unabii wa siku
2300, aliingia katika awamu ya pili nay a
mwisho katika huduma yake ya upatanisho .
Ni
kazi ya hukumu ya upelelezi ambaya ni
sehemu ya mwisho ambayo hatimaye
itakomesha
dhambi yote , iliyokuwa mfano wa kutakaswa
kwa hekalu la kale la waebrania katika siku
ya
upatanisho . Katika huduma hiyo kielelezo
hekalu lilitakaswa kwa damu ya wanyama wa
kafara , likini mambo ya mbinguni hutakaswa
kwa kafara kamilifu ya damu ya Yesu .
Hukumu ya upelelezi kufunua kwa viumbe
wa mbinguni ni nani miongoni mwa wafu
wamelala katika kristo na hivyo , katika yeye
wanahesabiwa kustahili kuwa na sehemu
katika
ufunuo wa kwanza . Pia inadhihirisha zazi ni
nani miongoni mwa walio hai wanakaa ndani
ya kristo , wakishika amri za Mungu na imani
ya Yesu , na katika yeye, hivyo basi, wako
tayari kwa ajili ya kuhamasishwa kuingia
katika ufalme wa milele . Hukumu hii
huthibitisha
haki ya Mungu, katika kuwokoa wale
wanaomwamini Yesu . Hutangaza kwamba
wale
waliohudumu kuwa watiifu kwa Mungu
watapokea ufalme . Hitimisho ya huduma hii
ya
kristo itakuwa ndiyo mwisho wa kufunga
mlango wa rehema ya mwanadamu kabla ya
marejeo ya Yesu . ( Waebr 8 : 1 -5 , 4 : 14 -16 ,
9: 11 - 28 , 10 : 19 -22 , 1 : 3 , 2 : 16 - 17 . Dan 7: 9- 27 ,
8: 13 -
14 , 9: 24 - 27 . Hes 14 : 34 . Ezekl 4 : 6 Ufu 14 : 6 -7 ,
20 : 12 , 14 : 12 , 22 : 12 . )
25 . Kuja kwa Kristo mara ya pili
Kuja kwa kristo mara ya pili ndilo tumaini
lenye baraka la kanisa , hitimisho kuu la injili.
Kuja kwa mwokozi kutakuwa halisi, binafsi ,
kutaonekana kwa dunia mzima . Atakaporudi
wenye haki waliokufa watafufuliwa na
pamoja na wenye haki walio hai watavikwa
utukufu
na kuchukuliwa kwenda mbinguni , lakini
waovu watakufa . Kutimizwa karibu kabisa
kwa
sehemu nyingi za unabii , pamoja na hakli ya
sasa ya ulimwengu , huonyeshe kwamba kuja
kwa kristo ku karibu sana . Wakati wa tukio
hilo hakukufunuliwa , na hivyo basi
tunahimizwa kuwa tayari kwa nyakati zote . .
( Tito 2: 13 , Math 24 , Mdo 1 : 9 -11 , Math 24 : 14 ,
Ufu 1: 7 , 14 : 14 - 20 , Math 24 : 43 - 43 ,
Wakor 15 : 51 -50 , 1 Wathes 1 : 7 , 4: 13 - 18 , 5: 1 -6 ,
Marko 13 ,
Luka 21 : 2, Tim 3: 1 -5 ) .
26 . Mauti na Ufunuo
Mshahara wa dhambi ni mauti . Lakini
Mungu, ambaye peke yakehapatwi na mauti ,
atawapa uzima wa milelewaliokombolewa
wake. Mpaka siku hiyo mauti ni hali ya
kutokuwa na fahamukwa watu wote . Wakati
kristo, aliye uzima wetu , atakapotokea , wenye
haki waliofufuliwa na walio hai watafikwa
utukufu na kunyakuliwa juu ili kumlaki
Bwana
wao . Ufufuo wa pili ambao ni ufufuo wa
waovu, utatokea miaka elfu moja baadaye .
( Warum 6 : 23 , 1Tim 6 : 15 -16 , Mhu 9 : 5 -6 , Zab
149: 3 -4 , Yoh 11 : 11 - 14 , 1 Wakor 15 : 51 -54 ,
1Wathes 4 : 13 -17 , Ufu 20 : 1 -10 )
.
27 . Milenia { Miaka Elfu} na Mwisho wa
Dhambi
Milenia ni miaka elfu moja ya utawala wa
kristo pamoja na watakatifu wake mbinguni
kati
ya ufufuo wa kwanza na pili . Wakati huo
waovu waliokufa watahukumiwa , dunia
itakuwa
ukiwa na utupu , bila wanadamu wakazi walio
hai , lakini ikikaliwa na shetani na malaika
zake . Mwishowe kristo na watakatifu wake na
Mji Mtakatifu watashuka kutoka Mbinguni.
Ndipo waovu waliokufa watafufuliwa, nao
pamoja na shetani na malika zake
watauzingira
mji , Lakini moto kutoka mbinguni
utawateketeza ili kuitakasa dunia. Na hivyo
ulimwengu
utakuwa huru bila dhambi na wenye dhambi
milele. ( Ufu 20 , 1 Wakor 6 : 2 -3 , Yer 4 : 23 -26 ,
Ufu 21 : 1 -5 ,Mal 4: 1, Ezekl 28 : 18 -19 )
28 . Dunia Mpya
Katika dunia mpya , ambamo haki
hukaa, Mungu ataweka tayari makao ya milele
waliokombolewa na mazingira makamilifu
kwa maisha ya milele, upendo , furaha na
kujifunza mbele zake . Kwa hapa Mungu
mwenyewe atakaa pamoja na watu wake, na
taabu
na mauti vitakuwa vimepita . Pambano kuu
litakuwa limemalizika, na dhambi
haitakuwepo
tena. Vitu vyote vyenye uhai na visivyo na
uhai vitatangaza kwamba Mungu ni pendo,
naye
atatawala milele. Amina . ( 2 Pet 3 : 13 , Isa 35 ,
65 : 17 -25 , Math 5: 5 , Ufu 21 : 1 -7 , 22 : 1 -5 , 11 : 5) .

ABC!

Welcome to amazing mathematics & lifestyle for everybody

Very interesting & meaningful msg to share:

If:
A B C D E F G H I J K LM N O P Q R S T U V W X Y Z
is equal to:
1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14 15 16 17 18 19 20 21 22 23 24 25 26

Then,

H+A+R+D+W+O+R+K ;
8+1+18+4+23+15+18+11=98%

K+N+O+W+L+E+D+G+E ;
11+14+15+23+12+5+4+7+5=96%

L+O+V+E;
12+15+22+5 = 54%

L+U+C+K ;
12+21+3+11 = 47%

None of them makes 100%. Then what makes 100%?

Is it Money? NO!

M+O+N+E+Y= 13+15+14+5+25=72%

Leadership? NO!

L+E+A+D+E+R+S+H+I+P= 12+5+1+4+5+18+19+8+9+16=97%

Every problem has a solution, only if we perhaps change our "ATTITUDE"...

A+T+T+I+T+U+D+E ;
1+20+20+9+20+21+4+5 = 100%

It is therefore OUR ATTITUDE towards Life and Work that makes
OUR Life 100% Successful.

Amazing mathematics

Beautiful msg to share:

Muziki wa Kikristo

Katika sehemu hii tutajielekeza kwenye
uelewa wa Kanisa la Waadventista Wasabato,
kuhusiana na nafasi na usimamizi wa muziki
kwenye huduma za ibada. Tutaiangalia
Kanuni ya Kanisa, ambacho ni kitabu cha
msingi cha sera chenye viwango na kawaida
za kanisa zinazotumika kusimamia makanisa
yote mawili; lile la mahalia na yale ya ngazi
za juu.
Kanuni hizi zilizopo kwenye kanuni za
kanisa, zilizojengwa kwenye Biblia na
zilizojikita kwa Kristo zinawakilisha uelewa
wa kanisa wa wakati huu, kuhusiana na
maswala mbalimbali ya kanisa yanayoathiri
mahusiano yetu, kama mwili wa waumini, na
kama mtu mmoja mmoja. Tunawasihi
watumiaji wote wa muziki na viongozi wa
kanisa kuwa na hamasa kubwa ya kuelewa
kanuni hizi na kuzisimamia kama walinzi
waaminifu wa kuta za Zayuni.
Kile Kanuni ya Kanisa inachosema kuhusu
Muziki
Angalizo : Nukuu imechukuliwa kutoka
“Kanuni ya Kanisa la Waadventista Wasabato
ya 2010, toleo la Kiingereza. Kupigiwa mistari,
kukolezwa kwa wino na mlalo wa maandishi
vimeongezwa. Maoni ni mapendekezo na
maelekezo yetu ya uongozi.
“Muziki ulitengenezwa kutumikia makusudi
matakatifu, kuyainua mawazo hadi kuwa kitu
safi, bora na kilicho juu, na kuamsha rohoni
hali ya ibada na shukrani kwa Mungu.” – DA
73, (CM, 143)
“Muziki ni mojawapo ya sanaa ya kiwango
cha juu sana. Muziki mzuri si tu unatupatia
maburudisho bali pia huyainua mawazo yetu
na kukuza viwango vyetu bora. Mungu mara
nyingi ametumia nyimbo za kiroho kugusa
mioyo ya wadhambi na kuwaongoza kwenye
toba. Kinyume chake, muziki duni unashusha
hali ya kiroho na kutupeleka mbali na
mahusiano yetu na Mungu.” – (CM, 143)
“Ni lazima tutumie uangalifu mkubwa katika
uchaguzi wa nyimbo majumbani mwetu,
kwenye mikusanyiko ya kijamii, mashuleni,
na makanisani. Mrindimo wowote wenye
vionjo vya jazz, rock, au mtindo
uliochanganya hayo, au lugha yoyote
inayooonesha hisia za kipumbavu au zisizo na
maana itaepukwa.” – (Angalia CM, pp. 92, 96,
143.)
MAONI:
“Kuimba, kama sehemu ya huduma ya kidini,
ni tendo la ibada kama lilivyo ombi.”
Patriachs and Prophets Uk. 594. Maombi
hukuza tabia kwa sababu kupitia maombi
tunauona uso wa Yesu, na kwa kumwangali
tunabadilishwa na kufanana naye. Muziki
mzuri ni wakala wa ujenzi wa tabia. (2
Wakorintho 3:18).
Muziki wa Jazz, Rock au mtindo
uliochanganya hayo mawili haipaswi
kuruhusiwa makanisani.
Angalia kwa makini tuni, mwafaka, na
mrindimo; haya yote hayapaswi kufuata
muziki wa kidunia.
Nguvu ya muziki – “Muziki unaweza kuwa
nguvu kubwa kwa mema, na bado hatulitumii
vya kutosha tawi hili la ibada. Uimbaji kwa
ujumla unafanyika kwa misisimko au kwa
kukidhi jambo maalumu, na kwa nyakati
zingine wale waimbao huachwa waendelee
kukosea, na muziki hupoteza athari yake
stahiki kwenye akili za wale waliopo. Muziki
ni lazima uwe na uzuri, uchungu, na nguvu.
Hebu sauti ziinuliwe katika nyimbo za sifa na
za kujitoa. Vitumie kama nyenzo pale
inapowezekana vifaa vya muziki, na uachilie
muafaka wa utukufu upande kwa Mungu,
zawadi inayokubalika.” – 4T 71 (CM, 114).
MAONI
Mwongozaji wa nyimbo ongoza vema. Epuke
makosa ya kawaida.
Mwongozaji anahitaji kuwa na yafuatayo:
Kitabu cha nyimbo chenye alama za muziki za
tonic sol-fa au staff notation, chombo cha
kuchagulia key kiitwacho Pitch pipe, na
kipande cha fimbo kwa kuongozea
kunakoonekana na wote.
Matumizi ya ala za muziki yameruhusiwa.
Matumizi mabaya yamekatazwa. Ni afadhali
kutotumia ala kabisa kuliko kutumia vibaya
na kuwa mtego na laana kwenye ibada kwako
mwenyewe na waabuduo wengine.
Imba kwa roho na uelewa – “Katika jitihada
zao za kuwafikia watu, watumishi wa Bwana
hawapaswi kufuata njia za dunia. Katika
mikutano inayofanyika wasitegemee waimbaji
wa kidunia na maonesho ya kwenye
majukwaa kuamsha usikivu. Wanawezaje
wale wasio na hamu ya Neno la Mungu,
ambao kamwe hawajawahi kusoma Neno lake
kwa nia ya dhati ya kutamani kuelewa ukweli
wake, kutegemewa kuimba kwa roho na kwa
kuelewa?... Kwaya ya mbnguni inawezaje
kujiunga na muziki ulio wa mtindo tu?...
“Uimbaji haupaswi daima kufanywa na
wachache. Mara nyingi kwa kadri
inavyowezekana, hebu na tuache kusanyiko
lote liimbe.” – 9T 143, 144 (CM, 114).
MAONI
Huduma zetu za ibada hazipaswi kuongozwa
au kuhudumiwa na waimbaji wasiomwabudu
Mungu wa kweli katika njia ya kweli.
Muda mwingi unahitaji kutumika kwa
uimbaji wa wote, na muda mchache
unapaswa kutumika kwa kwaya na vikundi
vya uimbaji. Kila Sabato kabla ya vipindi vya
Shule ya Sabato, hebu kuwe na angalau
dakika za kuimba na kujifunza nyimbo mpya.
Dakika 15 zingine zinapaswa kuwa baada ya
Shule ya Sabato na kabla ya huduma kuu.
Hebu dakika 15 zitengwe baada ya shule ya
sabato na kabla ya ibada kuu kwa ajili ya
uimbaji wa pamoja. Ratiba ya kwaya na
vikundi vya nyimbo iendelezwe ili kuzipa
kwaya fursa ya kuimba pamoja na nyimbo
nyingine zilizoandaliwa. Ratiba ihusishe ibada
za maombi ya katikati ya juma na ufunguzi
wa Sabato. Kwaya zinapokuwa nyingi,
usiendekeze maombi mengi ya kutaka nyimbo
zilizoimbwa au zile zinazopendwa sana
zirudiwe. Hii itumike kunapokuwa na kwaya
nyingi zinazosubiri zamu yao ya kuimba.
Kila idara inaweza kuwa na viongozi wa
muziki. Viongozi wawili wanaosisitizwa sana
ni hawa:
Shule ya Sabato:
“Baraza linaweza kumteua Mkurugenzi wa
Muziki wa Shue ya Sabato kwa kushauriana
na viongozi wa vitengo. Kama namna ya
kuonyesha ibada, muziki unapaswa
kumtukuza Mungu. Waimbaji na wanamuziki
wengine wanapaswa kuchaguliwa kwa
uangalifu kama viongozi wa maeneo mengine
ya huduma za Shule ya Sabato na wanapaswa
kupimwa kwa viwango vilevile. (Angalia uk.
92, 144). Baraza pia linaweza kumteua mpiga
kinanda wa vitengo vingine”. (CM, uk. 96)
Vijana Waadventista:
Maafisa wa AYS – “Kanisa huwachagua
maafisa hawa wa AYS: Kiongozi wa Vijana,
msaidizi wa kiongozi wa vijana, Katibu-
mtunza hazina, msaidizi wa Katibu-mtunza
hazina, mwongozaji wa nyimbo, mpiga
kinanda, na mdhamini (ambaye anaweza
kuwa mzee). Kwa kuwa muziki unachukua
nafasi muhimu katika kuunda tabia za vijana,
waimbaji hawana budi wachaguliwe kwa
uangalifu kama maafisa wengine wa AYS”.
(Angalia uk. 92, 96.) (CM, 102)
Kuchagua Waratibu wa Muziki – “Kanisa ni
lazima lichukue uangalifu mkubwa katika
kuwachagua viongozi wa kwaya, ikiwachagua
wale tu waliojitoa kabisa na wanaotoa nyimbo
sahihi kwa huduma zote za ibada za kanisa
na mikutano. Muziki wa kidunia au ule
wenye asili iletayo maswali, kamwe
usiingizwe kwenye huduma zetu.” (CM, 92).
“Viongozi wa nyimbo ni lazima wafanye kazi
kwa ukaribu sana na wachungaji na wazee
wa makanisa ili kwamba uchaguzi wa nyimbo
uoane na wazo kuu la hubiri. Kiongozi huyu
wa nyimbo yupo chini ya usimamizi wa
mchungaji au wazee wa kanisa na hafanyi
kazi kwa kujitegemea. Kiongozi wa nyimbo
anapaswa kushauriana nao kuhusu nyimbo
zitakazoimbwa na uteuzi wa waimbaji na
wanamuziki.” – (CM, uk. 92)
Idara na Huduma zinatakiwa kuteua
Wakurugenzi wa muziki, na kulitaarifu
baraza la kanisa ili liwapitishe wale
waliochaguliwa. Uchaguzi wa viongozi wa
muziki wa idara za Shule ya Sabato na Vijana
umefafanuliwa na kusisitizwa.
Uangalifu mkubwa utumike katika kuchagua
viongozi wa muziki makanisani. Baraza la
kanisa ni lazima libatilishe/liidhinishe
viongozi wote wa vikundi/kwaya zote ambazo
kanisa limevisajili. Kila idara ichague kiongozi
wake na kupeleka kwenye baraza la Kanisa ili
kubatilisha au kuidhinisha..
Kanisa linaweza kuwa na viongozi kadhaa wa
muziki wanaoongoza nyimbo kwenye idara
zao, huduma, au makundi. Lakini kanisa ni
lazima lichague mkurugenzi mmoja wa
muziki, msaidizi/wasaidizi, kutegemeana na
mahitaji ya kanisa, watakaoratibu viongozi
wengine wote wa muziki kutoka idara
mbalimbali za kanisa, huduma au vikundi.
(CM, 171).
Mratibu wa muziki ni mjumbe wa baraza la
kanisa. – (CM, 125). Huchaguliwa na kibaraza
cha uchaguzi. (CM, uk. 171)
Mkurugenzi/Mratibu/Kiongozi (Mratibu
Mkuu) wa muziki wa kanisa):
Ni mjumbe wa baraza la kanisa.
Ni lazima apimwe na kiwango kile kile cha
juu kilichotumika kuwachagua viongozi
wengine wa kanisa.
Ni kiongozi muhimu asaidiaye maandalizi ya
ibada. Hufanya kazi chini ya “Msimamizi wa
Mimbari/Ibada”. – (Wachungaji na Wazee wa
Kanisa)
Ndiye anayepaswa kuchagua nyimbo na
waimbaji watakaoendana na wazo kuu la
hubiri la siku hiyo.
Ndiye atakayeandaa ratiba ya Kwaya
(waimbaji)/Vikundi vya Waimbaji,
Waimbishaji, na Ala za muziki ikiwa
zitakuwepo.
Ndiye atakayehamasisha na kusimamia
filosofia ya Biblia/Kanisa kuhusu muziki.
Makanisa yaweza kuunda Kamati ya Muziki
itakazoongozwa na Mratibu wa Muziki wa
Kanisa itakayosimamia huduma za muziki
kanisani. Wajumbe wa baraza hili wanaweza
kuwa wasaidizi wa Mratibu mkuu (anaweza
pia kutumika kama katibu wa kamati),
waratibu wa muziki kutoka kwenye maidara,
na viongozi wakuu wa kwaya. Wajumbe
wengine wanaweza kuwa viongozi wa Chama
cha Vijana, Mkurugenzi wa Huduma za
Watoto, na Mkurugenzi wa Huma za
Washiriki. Mzee wa kanisa na mchungaji ni
maafisa wa kamati hii.
Ukubwa wa kamati utategemea ukubwa na
mahitaji ya kanisa. Kamati itafanya vizuri
kazi yake kama itakutana walau mara moja
kwa mwezi. Baraza la kanisa linaweza
kukasimu baadhi ya mambo mepesi
yahusianayo na muziki kwa kamati hii.
Kuwachagua Waimbaji – “Muziki mtakatifu ni
sehemu muhimu ya ibada ya hadhara. Kanisa
ni lazima litumie uangalifu katika kuchagua
wanakwaya na wanamuziki wengine
watakaowakilisha vizuri kanuni za kanisa. Ni
lazima wawe washiriki wa Kanisa, au
washiriki wa Shule ya Sabato, au wanachama
wa Chama cha Vijana Waadventista. Kwa
kuwa wanachukua nafasi inayooneka na watu
katika huduma za kanisani, wanatakiwa kuwa
kielelezo cha unyenyekevu na tabia njema,
katika mwonekano na mavazi yao. Mavazi ya
kwaya yatategemea uchaguzi wao. (CM, uk.
92).
Makanisa yanaweza kuwa na kwaya nyingi.
Kuwa na kwaya ya watoto ni njia ya
kuwasaidia kuwalea kiroho, kuwaunganisha
na familia ya kanisa, na kuwashirikisha
kwenye ushuhudiaji. (CM, uk. 92)
MAONI
1. Waimbaji ni lazima wachaguliwe na kanisa
2. Kanisa ni lazima lisajili kwaya/vikundi vya
uimbaji kwa kuwachagua waimbaji na
kuwabatilisha/kuwaidhinisha viongozi.
3. Kwa kuwa waimbaji ni wahubiri, ni lazima
wawe kielelezo, hasa katika mwonekano na
mavazi.
4. Waimbaji ni lazima wawe waongofu wa
kweli. Kwaya na Vikundi vingi vya uimbaji ni
maskani ya Mwovu. Vimejaa wivu, majivuno,
migogoro, mashindano, uzinzi, uasherati,
ubinafsi n.k.
5. Hebu na wajiundie sheria na kanuni zao
wenyewe. Kanisa lijiepusha kutunga na
kusimamia sheria kwa waimbaji. Kanuni ya
kanisa imetoa viwango vya kutosha, hebu
kanisa livitumie hivyo.
Kanisa linaweza kuwa na zaidi ya kwaya
moja, ikiwemo na kwaya ya Watoto. Zote hizo
ni kwaya za Kanisa. Epukeni kupendelea
kwaya au kikundo kimoja cha uimbaji na
kuvipuuza vingine. Kanisa linapaswa
kuvipenda vikundi na kwaya zote na kuvitia
moyo.

Jumapili, 8 Mei 2016

Lessoni juma hili

Somo limetafsiriwa na Mgune Masatu
             
(Mathayo 14 & 15)

Utangulizi:
Watu wanaamini kwamba
wanaume hawawaelewi wanawake kwa
undani. Inawezekana wazo hili lilianzishwa
na wanawake! Je, kuna watu ambao
huwaelewi? Kwa wale unaowaelewa, je,
huwa unawaelewa mara zote? Mojawapo ya
sababu za kujifunza Biblia ni kumwelewa
Mungu vizuri zaidi. Nadhani sababu
mojawapo iliyomfanya Mathayo aandike
waraka tunaojifunza katika somo la juma
hili ni kutufundisha kumtumaini Mungu,
hata pale ambapo hatuelewi maamuzi yake.
Hebu tuzame kwenye somo letu ili tujifunze
zaidi!

I. Kifo cha Yohana Mbatizaji
A. Soma Mathayo 14:6-11. Jambo
gani lilisababisha kifo cha Yohana? (Herode
kutaka kuonekana shujaa, kutokupevuka
(uchanga) kwa Herode, na wasiwasi wake
wa kupata aibu. Hila ya Herodia, hasira
kutokana na kukemewa (na Yohana kwa
ndoa yake isiyo halali – angalia Mathayo
14:3-5). Yote haya yanafungamanishwa na
binti wa Herodia kucheza dansi ya kifisadi.)

1. Ikiwa unampenda Yohana,
endapo ungekuwa mwanafunzi wake, kifo
chake kilikuwa cha kutisha sana na kuacha
pengo kubwa. Mazingira yanaongezea nini
kwenye mwitiko (reaction) wako?
B. Soma Mathayo 14:12. Kwa nini
wanafunzi wa Yohana walimwendea Yesu?
1. Je, walidhani kwamba Yesu
alipaswa kumwokoa Yohana? (Majuma
mawili yaliyopita tulijadili kwamba huenda
Yohana Mbatizaji alikuwa anashangaa kwa
nini Yesu hakumwokoa.)
C. Soma Mathayo 14:13. Kwa nini
Yesu alitafuta muda kuwa faraghani baada
ya kusikia habari za kifo cha Yohana?
(Aliathiriwa sana na habari hizo. Yumkini
alikuwa anatafakari kwamba tukio hili
lilithibitisha kuwa atakuwa mikononi mwa
Warumi. Huenda alikuwa tu na masikitiko
kwamba binamu yake alikuwa amefariki.)
D. Soma Mathayo 14:14. Je,
ungefanya hivi endapo ungekuwa Yesu?
(Nahisi ningekuwa ninajiliwaza huzuni
yangu na kujiponya hisia zangu. Lakini,
tunaona kwamba Yesu anajali zaidi kuhusu
kuwasaidia watu wengine.)
II. Kuwalisha Watu
A. Soma Mathayo 14:15-17. Je, hili
ndilo jibu ambalo ungelitoa?
1. Soma tena Mathayo 14:14.
Katika muktadha huu, je, hilo ndilo jibu
ambalo wanafunzi walipaswa kulitoa?
(Walikuwa hawaangalii taswira pana.
Walikuwa hawautegemei uwezo wa Yesu.
Walikuwa wanategemea kile
wanachokimiliki.)
B. Soma Mathayo 14:18-21.
Wanafunzi ni wa muhimu kiasi gani katika
huu muujiza?
1. Je, unahitajika kuwa na imani
kamilifu ili kushirikishwa kwenye muujiza?
(Kwa dhahiri hapana. Ama kwa hakika hii
ni habari njema.)
2. Soma tena Mathayo 14:16-17.
Je, Yesu alitarajia wanafunzi watende huu
muujiza?
3. Yesu alitendaje huu muujiza –
kuwalisha watu 15,000 kutokana na mikate
mitano na samaki wawili? (Angalia tena
Mathayo 14:19. Alitazama mbinguni,
akashukuru na kuanza kuimega ile mikate.)
C. Soma Mathayo 14:22. Hii
inashangaza – “Yesu aliwalazimisha
wanafunzi kupanda chomboni.” Kwa nini
hawakutaka kuondoka? (Soma Yohana
6:14-16. Hii inatupatia jibu. Mtiririko wa
matukio uliobainishwa na Yohana
unabainisha kuwa watu, baada ya kuona
huu muujiza mkuu, waliamua kumfanya
Yesu kuwa mfalme wao. Bila shaka
wanafunzi walisema, “Naam, hebu tufanye
hivi! Tutakuwa wasaidizi wa Yesu katika
ufalme mpya!”)
III. Upepo
A. Soma Mathayo 14:23-24. Je,
tatizo la wanafunzi kukabiliana na upepo
liliakisi mtazamo wao – kwamba walikuwa
tu hawaendelei maishani?
B. Soma Mathayo 14:25. “Zamu
ya nne” ni kitu gani? (Hii ni kati ya saa 9
na 12 za asubuhi kwa mujibu wa maoni ya
Adam Clarke.)
1. Hiyo inakuambia nini kuhusu
kiwango cha ugumu ambao wanafunzi
walikabiliana na upepo? (Walikuwa
wakienda pole pole sana tangu walipopata
chakula cha usiku.)
2. Una maoni gani kuhusu
usununu (hali) wa wanafunzi?
(Hawakufurahia kitendo cha kushindwa
kumfanya Yesu kuwa mfalme. Walikuwa
wamekatishwa tamaa na upepo.)
3. Kwa nini Yesu alitembea juu
ya maji kwenda kuwaona?
C. Soma Mathayo 14:26.
Unadhani Yesu alitarajia mwitiko (reaction)
huu? (Sidhani. Alikwenda kuwafariji, sio
kuwatisha.)
D. Soma Mathayo 14:27-31. Je,
unaweza kusema kuwa Petro alikuwa na
“imani ndogo?”
1. Kwa kumlinganisha na nani?
Wanafunzi chomboni?
2. Kwa nini Mathayo
anajumuisha kisa hiki kwenye mfululizo wa
hivi visa? (Kifo cha Yohana kinaonekana
kama kushindwa kwa watu wa nje.
Wanafunzi wa Yesu wamekata tamaa.
Mathayo anaelezea visa hivi ili kujenga hoja
dhidi ya kukatishwa tamaa. Anatuonesha
kwamba Yesu ana uwezo wa kutenda
miujiza, uwezo wa kuwashawishi watu
wengine kumfanya yeye kuwa mfalme, na
mamlaka juu ya nguvu za mvutano na vitu
vingine. Nadhani jambo la muhimu ni
kwamba Yesu anachagua muda wa kuingilia
kati, hapungukiwi mamlaka ya kuingilia
kati.
E. Soma Mathayo 14:32. Kwa nini
asitembee ufukweni? (Yesu amejikita zaidi
kwa wale waliopo chomboni.)
F. Soma Mathayo 14:33. Sasa
wanafunzi wanaonesha imani. Yesu
amewaendea na kubadilisha kabisa usununu
(hali) wao. Je, Yesu atakutendea hivyo? Je,
atakuja nyakati ambazo umekata tamaa na
kuvunjika moyo na kukudhihirishia uwezo
wake?
1. Watu wengi wanakana
kwamba Yesu si Mungu. Wanasema kuwa
Yesu ni “mtu mwema tu.” Hii inasema nini
kuwahusu watu hao? (Hawajui chochote
kuhusu Biblia. Biblia inabainisha wazi
kabisa kwamba Yesu ni Mungu.)
G. Soma Mathayo 14:34-36. Je,
Yesu alikuwa anaamua juu ya watu
watakaoponywa na wale ambao
hawataponywa? (Hapana.)
1. Kwa nini hafanyi hivyo?
(Tulianza sura hii ya kitabu cha Mathayo
kwa Yesu kufanya uamuzi wa ama
kumwokoa Yohana au la. Tumeishia na
uponyaji mkuu (wa watu wengi) kwa wote
waliomwendea Yesu.)
IV. Utamaduni
A. Soma Mathayo 15:1-6. Huu ni
mfano mwingine ambapo inaonekana Yesu
anajibu mashtaka ya kutenda kosa kwa
kusema “Nanyi pia mnatenda makosa!” Je,
kweli hicho ndicho anachokisema Yesu?
(Viongozi wa dini wanadai ukiukwaji wa
“utamaduni” wao. Yesu anajibu kwa kusema
kuwa utamaduni wao ni jambo lenye
mashaka. Linabatilisha neno la Mungu
angalao kwenye baadhi ya vipengele.)
B. Soma Mathayo 15:7-9. Isaya
anatabiri nini kuhusu matatizo waliyonayo
watu wa Mungu? (Kwamba wanafuata
sheria za mwanadamu badala ya kufuata
sheria za Mungu. Hawana ibada ya “kweli
kutoka moyoni.”)
1. Kusema kweli, nadhani
wanafunzi wanapaswa kunawa mikono yao
kabla ya kula. Kwa nini kuna pingamizi la
aina hiyo kutoka kwa Yesu? (Hili ni jambo
la muhimu. Kuna mawazo mazuri mengi
sana. Suala lililopo ni endapo tunajikita
kwenye “mawazo mazuri” au kwenye
matakwa ya Mungu.)
C. Soma Mathayo 15:10-11. Je,
Yesu amebadili mada? (Hapana. Anatoa wito
kwa makutano ili waweze kuelewa ujumbe
wake kuhusu mjadala juu ya kunawa
mikono.)
1. Ujumbe wa Yesu ni upi?
(Kilichotoka kinywani mwa viongozi wa dini
kilikuwa ni ukosoaji. Kitendo hiki ni kibaya
zaidi kuliko kunawa mikono yako.)
D. Soma Mathayo 15:12. Je,
unachukizwa na wazo hili kwamba
kiingiacho kinywani hakikutii unajisi?
E. Soma Mathayo 15:13-20.
Unauelewaje ujumbe wa Yesu – je,
anazungumzia tu kuhusu unawaji wa
mikono? (Inaonekana ujumbe wake ni
mpana zaidi. Vitu tuvilavyo na tunywavyo,
kama ilivyo kwa unawaji wa mikono,
vinaendana na suala la kuishi maisha bora.
Vinaakisi mawazo mazuri. Hata hivyo,
tunayoyasema yanaakisi tunayoyafikiria, na
kwenye mawazo ndipo tunapopata pambano
la kweli dhidi ya dhambi.)
V. Mataifa
A. Soma Mathayo 15:22-27.
Unaelezeaje kitendo cha Yesu kumwita huyu
mwanamke masikini “mbwa?” (Soma
Mathayo 15:28. Yesu alikuwa anamjaribu.)
B. Soma tena Mathayo 14:36. Je,
hii ni haki? Wote wanaomgusa Yesu
wanaponywa. Mwanamke huyu ilimpasa
kustahimili matusi na fedheha ili mwanaye
aweze kuponywa. Jambo gani linaendelea
hapa? (Nadhani hii ni kwa faida ya
wanafunzi (angalia Mathayo 15:23). Yesu
anataka kuwaonesha kuwa watu wa mataifa
wanaweza kuwa na imani kubwa. Jifunze
kutokana na fundisho hili kwa ajili ya
nyakati ambazo Mungu anaonekana
kukataa/kujizuia kukusaidia.)
C. Rafiki, tunaona kwamba Yesu
anafanya maamuzi ya kusaidia na kuponya,
maamuzi ambayo mara nyingine ni magumu
sana kuyaelewa. Je, utadhamiria leo, kwa
uwezo wa Roho Mtakatifu, kuamua tu
kumtumaini Mungu?
VI. Juma lijalo: Petro na Mwamba.

Jumanne, 3 Mei 2016

Lessoni juma hili

        (Mathayo 12)
Somo limetafsiriwa na Mgune Masatu.
Utangulizi: Kama mwanasheria, ninaamini
katika sheria. Kuwa na sheria sahihi
husaidia kuwa na uhuru kamili, ikiwemo
uhuru wa dini. Mungu anaamini katika
utawala wa sheria, vinginevyo Yesu
asingekuja kutimiza matakwa ya sheria kwa
niaba (ajili) yetu. Kinachowafanya
wanasheria wawe na kazi ni mgongano kati
ya sheria na mitazamo tofauti juu ya sheria
hizo. Somo letu juma hili linahusu
kuzichanganua sheria za Mungu. Hebu
tuzame kwenye somo letu la Mathayo ili
tuone kile tunachoweza kujifunza kuhusu
asili ya sheria za Mungu!
I. Sheria (Kanuni) ya Nira
A. Soma Mathayo 11:28-30. Juma
lililopita tuliyaangalia mafungu haya. Hebu
tuangalie kipengele kimoja cha ziada. Yesu
anatupatia “nira.” Je, hicho ni kitu kizuri au
kibaya?
1. Je, nira inafanana na sheria,
kwamba inatufunga? (Nira ni kikwazo,
lakini jambo jema ni kwamba Yesu ndiye
mtu mwingine aliyepo kwenye hiyo nira. Hii
inamaanisha kuwa katika kila jambo, kila
changamoto, kila tatizo, Yesu anakuinua.
Hiki ni kizuizi chenye manufaa. Kinaonesha
rehema.)
B. Soma Mathayo 12:1-2. Kwa
nini si halali kuvunja masuke? (Tatizo
halikuwa kuiba masuke (Kumbukumbu la
Torati 23:25), shtaka lilikuwa ni kufanya
kazi siku ya Sabato (Kutoka 20:8-11).)
C. Soma Mathayo 12:3-4.
Unalichukuliaje jibu la Yesu? Je, hilo silo
jibu wakujibulo wanao – kwamba watu
wengine pia wanafanya vivyo hivyo? “Huyu
anatenda hivyo hivyo, Yule pia anafanya
hivyo hivyo!”
1. Unadhani jibu gani litakuwa
zuri zaidi kuliko “watu wengine pia
wanafanya jambo hilo hilo?” (Ningejibu
kwamba hii sio kazi.)
D. Soma 1 Samweli 21:1-6. Je,
Daudi anasema ukweli kwa Mfalme Sauli
kuhusu kuwa kwenye safari ya kazi ya
utume? (Hapana. Ukisoma sura iliyotangulia
utaona kwamba Yonathani alimwonya Daudi
kuwa Mfalme Sauli anataka kumwua. Daudi
anamkimbia Sauli.)
1. Jambo gani linafanana kati ya
mustakabali wa Daudi na wanafunzi wa
Yesu? (Wana njaa.)
2. Je, hicho ndicho tunachopaswa
kujifunza kuhusu Sabato – kwamba ni sahihi
kuvunja sheria ikiwa una njaa?
a. Ikiwa hicho sicho cha
kujifunza, je, Yesu anafundisha juu ya
jambo gani?
(1) Kuwasaidia watu wengine ni
muhimu zaidi kuliko sheria?
b. Vipi ikiwa kuwasaidia watu
wengine ndio sheria kuu?
(1) Je, hicho ndicho kipimo? Je,
hiyo ndio kanuni (sheria)?
E. Soma Mathayo 12:5-8. Yesu
anamaanisha nini anaposema kwamba yeye
ndiye “Bwana wa Sabato?” (Yeye ndiye
anayeamua kilicho sahihi kufanyika siku ya
Sabato.)
1. Yesu anamaanisha nini
anaposema, “Nataka rehema, wala si
sadaka?” (Hosea 6:6) (Ikiwa wanafunzi wa
Yesu pamoja na Daudi wangejizuia kula,
hiyo ingekuwa sadaka. Hivyo, Yesu anasema
kuwa katika amri ya Sabato (na kwa
dhahiri, kwenye amri nyingine pia), lengo ni
kuonesha rehema.)
2. Je, hiyo ni sheria? (Nadhani ni
sheria. Angalia mtazamo wako kwenye nusu
ya pili ya Amri Kumi na kila sheria nyingine
inayofanana na hizo katika Biblia. Je, sheria
hizo zipo kwa ajili ya kutukwaza na
kutuangusha, na kututia dhambini? Au, zipo
hapo kwa kuwa Yesu anatupenda na
anatutaka tuishi maisha huru dhidi ya
matatizo yasiyo ya lazima? Nadhani sheria
zipo ili kutuonesha rehema – na hicho
ndicho anachokimaanisha Yesu. “Nira” yake
ni rehema kwetu.)
3. Utagundua kwamba amri ya
Sabato haipo kwenye “nusu ya pili” ya Amri
Kumi. Je, amri hiyo inahusu kumwabudu
Mungu au inahusu kuwa na maisha bora?
(Amri ya Nne ni kiunganishi cha amri
zinazomhusu Mungu na zile zinazowahusu
wanadamu wenzetu. Soma Marko 2:27-28.
Sabato ni siku ya pumziko kwa wanadamu,
lakini pia ni muda wa pekee wa kutafakari
kile ambacho Mungu amekifanya kwa ajili
yetu.)
II. Sheria (Kanuni) ya Mkono
Uliopooza
A. Soma Mathayo 12:9-10.
Ungejibuje swali hili ikiwa unaelewa
kwamba rehema ndilo lengo lililopo nyuma
ya sheria za Mungu? (Jibu ni dhahiri kabisa,
“ndiyo.”)
B. Soma Mathayo 12:11-13. Kisa
hiki kinakazia vipi visa vilivyotangulia
kuhusu kuvunja masuke na Daudi kula
mikate ya wonyesho? (Hii inaonesha
kwamba rehema ndio sheria kiongozi.)
1. Hebu tujikite kwenye kisa cha
Daudi kuhusu mikate ya wonyesho. Lengo la
hekalu na sherehe (taratibu) za hekalu
lilikuwa ni lipi? (Kuelezea ujio wa Yesu na
kufa kwa ajili yetu.)
a. Je, hiyo ilikuwa ni
kutuonesha rehema? (Ndiyo! Kuzipa
kipaumbele sheria zinazohusu mikate ya
wonyesho dhidi ya mahitaji ya Daudi
kungepuuzia maana yote ya taratibu za
hekalu – kwamba Mungu alikuwa anakuja
ili kutuonesha rehema!)
C. Je, unadhani Mungu ana
tabaka la sheria (kanuni)? Je, baadhi ya
sheria ni muhimu zaidi kuliko nyingine?
1. Katika sheria za Marekani,
kuna sheria inayotawala inayosema kwamba
hakuna sheria inayoizidi nyingine isipokuwa
tu kama kuna ukinzani wa moja kwa moja.
Kwenye visa tulivyoviangalia hadi sasa
(kuvunja masuke na uponyaji siku ya
Sabato/Daudi kula mikate ya wonyesho), je,
palikuwepo na ukinzani wa moja kwa moja
kati ya sheria ya rehema na Sabato au
sheria za hekalu? (Mambo ya Walawi 24:8-9
inakinzana moja kwa moja na Daudi kula
mikate ya wonyesho. Na kwa kuongezea,
Yesu anakiri kuwa kuna ukinzani (Mathayo
12:4). Ingawa sioni ukinzani kwenye
kuvunja masuke, Yesu alijizuia kujenga hoja
kwamba wanafunzi wake hawakuwa
wakifanya kazi. Nadhani anachokimaanisha
Yesu ni kwamba kuna tabaka la sheria.)
2. Je, kuna maelezo ya ziada
kuhusu mbadala wa tabaka la sheria
mbalimbali? (Kwamba sheria zote zina
maana moja – kuonesha rehema.)
D. Soma Mathayo 12:14. Viongozi
wa dini wanaonesha nini? (Hawadhihirishi
rehema. Wanaonesha chuki. Huu ni
ukiukwaji wa dhahiri wa sheria.)
III. Sheria (Kanuni) ya Rehema
A. Soma Mathayo 12:15-16. Baada
ya Yesu kufahamu njama ya kutaka
kumwua, anaondoka. Je, ilikuwa hatari
kwake kufanya uponyaji? (Ndiyo,
ingewachochea zaidi viongozi wa dini
kutaka kumwua Yesu.)
1. Pamoja na hayo kwa nini Yesu
anafanya hivi? (Rehema!)
B. Soma Mathayo 12:17-21.
Tunaambiwa kuwa Yesu atafanya nini?
(Kwa uwezo wa Roho Mtakatifu atatangaza
hukumu, na ataiongoza “hukumu
kushinda.” Ataleta tumaini.)
1. Yesu hatafanya nini? (Hatazua
wala kushiriki kwenye ugomvi au kulia.
Hatainua sauti yake. Hatawajeruhi zaidi
wale ambao tayari wameshajeruhiwa.)
C. Soma tena Mathayo 12:20.
“Utambi utokao moshi” umezimika.
“Mwanzi wenye mchubuko” uko hatarini
kuvunjika kwa sababu tayari una
mchubuko. Vitu hivi vinawaelezea watu wa
aina gani? Wagonjwa? Waliokata tamaa?
Waliopoteza moto wa imani?
1. Je, watu wanaohamasisha
mtindo wa maisha uliojaa dhambi, na wana
uhasama na dini, pia wanastahili kuwa
kwenye kundi la mianzi (matete) yenye
mchubuko na tambi zitokazo moshi?
IV. Sheria ya Hatari
A. Soma Mathayo 12:22-23. Watu
hawa wanaonekana kufikiri juu ya jambo
gani? (Wanaashiria kwamba Yesu ni
Masihi.)
B. Soma Mathayo 12:24. Viongozi
wa dini wanatoa madai gani? (Kwamba Yesu
anapewa uwezo na Shetani.)
C. Katika Mathayo 12:25-29 Yesu
anajenga mfululizo wa hoja zenye mantiki
akibainisha kwamba hatumii uwezo wa
Shetani. Soma Mathayo 12:30-32. Kwa nini
Yesu anazungumzia kunena “dhidi ya Roho
Mtakatifu” na kusema kwamba hiyo ni
dhambi isiyoweza kusamehewa? (Kuihusisha
kazi ya Roho Mtakatifu na Shetani ndio
dhambi isiyoweza kusamehewa.)
1. Asubuhi hii nilibadilishana
mawazo na mtu aliyekuwa anajenga hoja
kwamba muziki wa kisasa wa kumsifu
Mungu wenye mdundo ni wa kishetani.
Ninaamini kwamba muziki wa kisasa wenye
kusifu unahusisha, kwa kiasi fulani, Roho
Mtakatifu kuyaelekeza mawazo yangu kwa
Mungu moja kwa moja. Angalia 1
Wakorintho 14:14-17. Hata hivyo, suala
ninalotaka ulitafakari sio muziki, bali shtaka
la uwezo (nguvu) wa kishetani. Hatari ni
ipi? (Hatari iliyopo ni dhambi
isiyosamehewa! Wakristo wanaowatuhumu
Wakristo wengine kwamba wanatumia
uwezo wa Shetani wako kwenye hatari hiyo
hiyo ya dhambi isiyosamehewa. Wanatakiwa
kuwa na uhakika na mashtaka haya,
vinginevyo wasiwatuhumu.)
2. Je, yule mtu ambaye
hakukubaliana nami ametenda dhambi
isiyosamehewa? (Hii si sawa na mtego wa
waya. Tatizo ni kwamba Roho Mtakatifu
anatugusa na kutufanya tutambue dhambi
zetu. Yohana 16:8-9. Tunapoanza kuupinga
uwezo wa Roho Mtakatifu kwa kudai
kwamba uwezo huo ni wa kishetani,
tunaufukuzilia mbali uwezo huo wenye
mguso maishani mwetu. Ni mchakato, sio
shtaka moja.)
D. Rafiki, je, unaamini kwamba
rehema iko nyuma ya sheria za Mungu kwa
ajili ya maisha yetu? Je, utafanya uamuzi
leo, kuwaonesha watu wengine rehema ya
Mungu? Kupata pumziko kwenye rehema ya
Mungu kwako?
V. Juma lijalo: Bwana wa
Wayahudi na Mataifa.