Somo limetafsiriwa na Mgune Masatu
(Mathayo 14 & 15)
Utangulizi:
Watu wanaamini kwamba
wanaume hawawaelewi wanawake kwa
undani. Inawezekana wazo hili lilianzishwa
na wanawake! Je, kuna watu ambao
huwaelewi? Kwa wale unaowaelewa, je,
huwa unawaelewa mara zote? Mojawapo ya
sababu za kujifunza Biblia ni kumwelewa
Mungu vizuri zaidi. Nadhani sababu
mojawapo iliyomfanya Mathayo aandike
waraka tunaojifunza katika somo la juma
hili ni kutufundisha kumtumaini Mungu,
hata pale ambapo hatuelewi maamuzi yake.
Hebu tuzame kwenye somo letu ili tujifunze
zaidi!
I. Kifo cha Yohana Mbatizaji
A. Soma Mathayo 14:6-11. Jambo
gani lilisababisha kifo cha Yohana? (Herode
kutaka kuonekana shujaa, kutokupevuka
(uchanga) kwa Herode, na wasiwasi wake
wa kupata aibu. Hila ya Herodia, hasira
kutokana na kukemewa (na Yohana kwa
ndoa yake isiyo halali – angalia Mathayo
14:3-5). Yote haya yanafungamanishwa na
binti wa Herodia kucheza dansi ya kifisadi.)
1. Ikiwa unampenda Yohana,
endapo ungekuwa mwanafunzi wake, kifo
chake kilikuwa cha kutisha sana na kuacha
pengo kubwa. Mazingira yanaongezea nini
kwenye mwitiko (reaction) wako?
B. Soma Mathayo 14:12. Kwa nini
wanafunzi wa Yohana walimwendea Yesu?
1. Je, walidhani kwamba Yesu
alipaswa kumwokoa Yohana? (Majuma
mawili yaliyopita tulijadili kwamba huenda
Yohana Mbatizaji alikuwa anashangaa kwa
nini Yesu hakumwokoa.)
C. Soma Mathayo 14:13. Kwa nini
Yesu alitafuta muda kuwa faraghani baada
ya kusikia habari za kifo cha Yohana?
(Aliathiriwa sana na habari hizo. Yumkini
alikuwa anatafakari kwamba tukio hili
lilithibitisha kuwa atakuwa mikononi mwa
Warumi. Huenda alikuwa tu na masikitiko
kwamba binamu yake alikuwa amefariki.)
D. Soma Mathayo 14:14. Je,
ungefanya hivi endapo ungekuwa Yesu?
(Nahisi ningekuwa ninajiliwaza huzuni
yangu na kujiponya hisia zangu. Lakini,
tunaona kwamba Yesu anajali zaidi kuhusu
kuwasaidia watu wengine.)
II. Kuwalisha Watu
A. Soma Mathayo 14:15-17. Je, hili
ndilo jibu ambalo ungelitoa?
1. Soma tena Mathayo 14:14.
Katika muktadha huu, je, hilo ndilo jibu
ambalo wanafunzi walipaswa kulitoa?
(Walikuwa hawaangalii taswira pana.
Walikuwa hawautegemei uwezo wa Yesu.
Walikuwa wanategemea kile
wanachokimiliki.)
B. Soma Mathayo 14:18-21.
Wanafunzi ni wa muhimu kiasi gani katika
huu muujiza?
1. Je, unahitajika kuwa na imani
kamilifu ili kushirikishwa kwenye muujiza?
(Kwa dhahiri hapana. Ama kwa hakika hii
ni habari njema.)
2. Soma tena Mathayo 14:16-17.
Je, Yesu alitarajia wanafunzi watende huu
muujiza?
3. Yesu alitendaje huu muujiza –
kuwalisha watu 15,000 kutokana na mikate
mitano na samaki wawili? (Angalia tena
Mathayo 14:19. Alitazama mbinguni,
akashukuru na kuanza kuimega ile mikate.)
C. Soma Mathayo 14:22. Hii
inashangaza – “Yesu aliwalazimisha
wanafunzi kupanda chomboni.” Kwa nini
hawakutaka kuondoka? (Soma Yohana
6:14-16. Hii inatupatia jibu. Mtiririko wa
matukio uliobainishwa na Yohana
unabainisha kuwa watu, baada ya kuona
huu muujiza mkuu, waliamua kumfanya
Yesu kuwa mfalme wao. Bila shaka
wanafunzi walisema, “Naam, hebu tufanye
hivi! Tutakuwa wasaidizi wa Yesu katika
ufalme mpya!”)
III. Upepo
A. Soma Mathayo 14:23-24. Je,
tatizo la wanafunzi kukabiliana na upepo
liliakisi mtazamo wao – kwamba walikuwa
tu hawaendelei maishani?
B. Soma Mathayo 14:25. “Zamu
ya nne” ni kitu gani? (Hii ni kati ya saa 9
na 12 za asubuhi kwa mujibu wa maoni ya
Adam Clarke.)
1. Hiyo inakuambia nini kuhusu
kiwango cha ugumu ambao wanafunzi
walikabiliana na upepo? (Walikuwa
wakienda pole pole sana tangu walipopata
chakula cha usiku.)
2. Una maoni gani kuhusu
usununu (hali) wa wanafunzi?
(Hawakufurahia kitendo cha kushindwa
kumfanya Yesu kuwa mfalme. Walikuwa
wamekatishwa tamaa na upepo.)
3. Kwa nini Yesu alitembea juu
ya maji kwenda kuwaona?
C. Soma Mathayo 14:26.
Unadhani Yesu alitarajia mwitiko (reaction)
huu? (Sidhani. Alikwenda kuwafariji, sio
kuwatisha.)
D. Soma Mathayo 14:27-31. Je,
unaweza kusema kuwa Petro alikuwa na
“imani ndogo?”
1. Kwa kumlinganisha na nani?
Wanafunzi chomboni?
2. Kwa nini Mathayo
anajumuisha kisa hiki kwenye mfululizo wa
hivi visa? (Kifo cha Yohana kinaonekana
kama kushindwa kwa watu wa nje.
Wanafunzi wa Yesu wamekata tamaa.
Mathayo anaelezea visa hivi ili kujenga hoja
dhidi ya kukatishwa tamaa. Anatuonesha
kwamba Yesu ana uwezo wa kutenda
miujiza, uwezo wa kuwashawishi watu
wengine kumfanya yeye kuwa mfalme, na
mamlaka juu ya nguvu za mvutano na vitu
vingine. Nadhani jambo la muhimu ni
kwamba Yesu anachagua muda wa kuingilia
kati, hapungukiwi mamlaka ya kuingilia
kati.
E. Soma Mathayo 14:32. Kwa nini
asitembee ufukweni? (Yesu amejikita zaidi
kwa wale waliopo chomboni.)
F. Soma Mathayo 14:33. Sasa
wanafunzi wanaonesha imani. Yesu
amewaendea na kubadilisha kabisa usununu
(hali) wao. Je, Yesu atakutendea hivyo? Je,
atakuja nyakati ambazo umekata tamaa na
kuvunjika moyo na kukudhihirishia uwezo
wake?
1. Watu wengi wanakana
kwamba Yesu si Mungu. Wanasema kuwa
Yesu ni “mtu mwema tu.” Hii inasema nini
kuwahusu watu hao? (Hawajui chochote
kuhusu Biblia. Biblia inabainisha wazi
kabisa kwamba Yesu ni Mungu.)
G. Soma Mathayo 14:34-36. Je,
Yesu alikuwa anaamua juu ya watu
watakaoponywa na wale ambao
hawataponywa? (Hapana.)
1. Kwa nini hafanyi hivyo?
(Tulianza sura hii ya kitabu cha Mathayo
kwa Yesu kufanya uamuzi wa ama
kumwokoa Yohana au la. Tumeishia na
uponyaji mkuu (wa watu wengi) kwa wote
waliomwendea Yesu.)
IV. Utamaduni
A. Soma Mathayo 15:1-6. Huu ni
mfano mwingine ambapo inaonekana Yesu
anajibu mashtaka ya kutenda kosa kwa
kusema “Nanyi pia mnatenda makosa!” Je,
kweli hicho ndicho anachokisema Yesu?
(Viongozi wa dini wanadai ukiukwaji wa
“utamaduni” wao. Yesu anajibu kwa kusema
kuwa utamaduni wao ni jambo lenye
mashaka. Linabatilisha neno la Mungu
angalao kwenye baadhi ya vipengele.)
B. Soma Mathayo 15:7-9. Isaya
anatabiri nini kuhusu matatizo waliyonayo
watu wa Mungu? (Kwamba wanafuata
sheria za mwanadamu badala ya kufuata
sheria za Mungu. Hawana ibada ya “kweli
kutoka moyoni.”)
1. Kusema kweli, nadhani
wanafunzi wanapaswa kunawa mikono yao
kabla ya kula. Kwa nini kuna pingamizi la
aina hiyo kutoka kwa Yesu? (Hili ni jambo
la muhimu. Kuna mawazo mazuri mengi
sana. Suala lililopo ni endapo tunajikita
kwenye “mawazo mazuri” au kwenye
matakwa ya Mungu.)
C. Soma Mathayo 15:10-11. Je,
Yesu amebadili mada? (Hapana. Anatoa wito
kwa makutano ili waweze kuelewa ujumbe
wake kuhusu mjadala juu ya kunawa
mikono.)
1. Ujumbe wa Yesu ni upi?
(Kilichotoka kinywani mwa viongozi wa dini
kilikuwa ni ukosoaji. Kitendo hiki ni kibaya
zaidi kuliko kunawa mikono yako.)
D. Soma Mathayo 15:12. Je,
unachukizwa na wazo hili kwamba
kiingiacho kinywani hakikutii unajisi?
E. Soma Mathayo 15:13-20.
Unauelewaje ujumbe wa Yesu – je,
anazungumzia tu kuhusu unawaji wa
mikono? (Inaonekana ujumbe wake ni
mpana zaidi. Vitu tuvilavyo na tunywavyo,
kama ilivyo kwa unawaji wa mikono,
vinaendana na suala la kuishi maisha bora.
Vinaakisi mawazo mazuri. Hata hivyo,
tunayoyasema yanaakisi tunayoyafikiria, na
kwenye mawazo ndipo tunapopata pambano
la kweli dhidi ya dhambi.)
V. Mataifa
A. Soma Mathayo 15:22-27.
Unaelezeaje kitendo cha Yesu kumwita huyu
mwanamke masikini “mbwa?” (Soma
Mathayo 15:28. Yesu alikuwa anamjaribu.)
B. Soma tena Mathayo 14:36. Je,
hii ni haki? Wote wanaomgusa Yesu
wanaponywa. Mwanamke huyu ilimpasa
kustahimili matusi na fedheha ili mwanaye
aweze kuponywa. Jambo gani linaendelea
hapa? (Nadhani hii ni kwa faida ya
wanafunzi (angalia Mathayo 15:23). Yesu
anataka kuwaonesha kuwa watu wa mataifa
wanaweza kuwa na imani kubwa. Jifunze
kutokana na fundisho hili kwa ajili ya
nyakati ambazo Mungu anaonekana
kukataa/kujizuia kukusaidia.)
C. Rafiki, tunaona kwamba Yesu
anafanya maamuzi ya kusaidia na kuponya,
maamuzi ambayo mara nyingine ni magumu
sana kuyaelewa. Je, utadhamiria leo, kwa
uwezo wa Roho Mtakatifu, kuamua tu
kumtumaini Mungu?
VI. Juma lijalo: Petro na Mwamba.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni