Katika sehemu hii tutajielekeza kwenye
uelewa wa Kanisa la Waadventista Wasabato,
kuhusiana na nafasi na usimamizi wa muziki
kwenye huduma za ibada. Tutaiangalia
Kanuni ya Kanisa, ambacho ni kitabu cha
msingi cha sera chenye viwango na kawaida
za kanisa zinazotumika kusimamia makanisa
yote mawili; lile la mahalia na yale ya ngazi
za juu.
Kanuni hizi zilizopo kwenye kanuni za
kanisa, zilizojengwa kwenye Biblia na
zilizojikita kwa Kristo zinawakilisha uelewa
wa kanisa wa wakati huu, kuhusiana na
maswala mbalimbali ya kanisa yanayoathiri
mahusiano yetu, kama mwili wa waumini, na
kama mtu mmoja mmoja. Tunawasihi
watumiaji wote wa muziki na viongozi wa
kanisa kuwa na hamasa kubwa ya kuelewa
kanuni hizi na kuzisimamia kama walinzi
waaminifu wa kuta za Zayuni.
Kile Kanuni ya Kanisa inachosema kuhusu
Muziki
Angalizo : Nukuu imechukuliwa kutoka
“Kanuni ya Kanisa la Waadventista Wasabato
ya 2010, toleo la Kiingereza. Kupigiwa mistari,
kukolezwa kwa wino na mlalo wa maandishi
vimeongezwa. Maoni ni mapendekezo na
maelekezo yetu ya uongozi.
“Muziki ulitengenezwa kutumikia makusudi
matakatifu, kuyainua mawazo hadi kuwa kitu
safi, bora na kilicho juu, na kuamsha rohoni
hali ya ibada na shukrani kwa Mungu.” – DA
73, (CM, 143)
“Muziki ni mojawapo ya sanaa ya kiwango
cha juu sana. Muziki mzuri si tu unatupatia
maburudisho bali pia huyainua mawazo yetu
na kukuza viwango vyetu bora. Mungu mara
nyingi ametumia nyimbo za kiroho kugusa
mioyo ya wadhambi na kuwaongoza kwenye
toba. Kinyume chake, muziki duni unashusha
hali ya kiroho na kutupeleka mbali na
mahusiano yetu na Mungu.” – (CM, 143)
“Ni lazima tutumie uangalifu mkubwa katika
uchaguzi wa nyimbo majumbani mwetu,
kwenye mikusanyiko ya kijamii, mashuleni,
na makanisani. Mrindimo wowote wenye
vionjo vya jazz, rock, au mtindo
uliochanganya hayo, au lugha yoyote
inayooonesha hisia za kipumbavu au zisizo na
maana itaepukwa.” – (Angalia CM, pp. 92, 96,
143.)
MAONI:
“Kuimba, kama sehemu ya huduma ya kidini,
ni tendo la ibada kama lilivyo ombi.”
Patriachs and Prophets Uk. 594. Maombi
hukuza tabia kwa sababu kupitia maombi
tunauona uso wa Yesu, na kwa kumwangali
tunabadilishwa na kufanana naye. Muziki
mzuri ni wakala wa ujenzi wa tabia. (2
Wakorintho 3:18).
Muziki wa Jazz, Rock au mtindo
uliochanganya hayo mawili haipaswi
kuruhusiwa makanisani.
Angalia kwa makini tuni, mwafaka, na
mrindimo; haya yote hayapaswi kufuata
muziki wa kidunia.
Nguvu ya muziki – “Muziki unaweza kuwa
nguvu kubwa kwa mema, na bado hatulitumii
vya kutosha tawi hili la ibada. Uimbaji kwa
ujumla unafanyika kwa misisimko au kwa
kukidhi jambo maalumu, na kwa nyakati
zingine wale waimbao huachwa waendelee
kukosea, na muziki hupoteza athari yake
stahiki kwenye akili za wale waliopo. Muziki
ni lazima uwe na uzuri, uchungu, na nguvu.
Hebu sauti ziinuliwe katika nyimbo za sifa na
za kujitoa. Vitumie kama nyenzo pale
inapowezekana vifaa vya muziki, na uachilie
muafaka wa utukufu upande kwa Mungu,
zawadi inayokubalika.” – 4T 71 (CM, 114).
MAONI
Mwongozaji wa nyimbo ongoza vema. Epuke
makosa ya kawaida.
Mwongozaji anahitaji kuwa na yafuatayo:
Kitabu cha nyimbo chenye alama za muziki za
tonic sol-fa au staff notation, chombo cha
kuchagulia key kiitwacho Pitch pipe, na
kipande cha fimbo kwa kuongozea
kunakoonekana na wote.
Matumizi ya ala za muziki yameruhusiwa.
Matumizi mabaya yamekatazwa. Ni afadhali
kutotumia ala kabisa kuliko kutumia vibaya
na kuwa mtego na laana kwenye ibada kwako
mwenyewe na waabuduo wengine.
Imba kwa roho na uelewa – “Katika jitihada
zao za kuwafikia watu, watumishi wa Bwana
hawapaswi kufuata njia za dunia. Katika
mikutano inayofanyika wasitegemee waimbaji
wa kidunia na maonesho ya kwenye
majukwaa kuamsha usikivu. Wanawezaje
wale wasio na hamu ya Neno la Mungu,
ambao kamwe hawajawahi kusoma Neno lake
kwa nia ya dhati ya kutamani kuelewa ukweli
wake, kutegemewa kuimba kwa roho na kwa
kuelewa?... Kwaya ya mbnguni inawezaje
kujiunga na muziki ulio wa mtindo tu?...
“Uimbaji haupaswi daima kufanywa na
wachache. Mara nyingi kwa kadri
inavyowezekana, hebu na tuache kusanyiko
lote liimbe.” – 9T 143, 144 (CM, 114).
MAONI
Huduma zetu za ibada hazipaswi kuongozwa
au kuhudumiwa na waimbaji wasiomwabudu
Mungu wa kweli katika njia ya kweli.
Muda mwingi unahitaji kutumika kwa
uimbaji wa wote, na muda mchache
unapaswa kutumika kwa kwaya na vikundi
vya uimbaji. Kila Sabato kabla ya vipindi vya
Shule ya Sabato, hebu kuwe na angalau
dakika za kuimba na kujifunza nyimbo mpya.
Dakika 15 zingine zinapaswa kuwa baada ya
Shule ya Sabato na kabla ya huduma kuu.
Hebu dakika 15 zitengwe baada ya shule ya
sabato na kabla ya ibada kuu kwa ajili ya
uimbaji wa pamoja. Ratiba ya kwaya na
vikundi vya nyimbo iendelezwe ili kuzipa
kwaya fursa ya kuimba pamoja na nyimbo
nyingine zilizoandaliwa. Ratiba ihusishe ibada
za maombi ya katikati ya juma na ufunguzi
wa Sabato. Kwaya zinapokuwa nyingi,
usiendekeze maombi mengi ya kutaka nyimbo
zilizoimbwa au zile zinazopendwa sana
zirudiwe. Hii itumike kunapokuwa na kwaya
nyingi zinazosubiri zamu yao ya kuimba.
Kila idara inaweza kuwa na viongozi wa
muziki. Viongozi wawili wanaosisitizwa sana
ni hawa:
Shule ya Sabato:
“Baraza linaweza kumteua Mkurugenzi wa
Muziki wa Shue ya Sabato kwa kushauriana
na viongozi wa vitengo. Kama namna ya
kuonyesha ibada, muziki unapaswa
kumtukuza Mungu. Waimbaji na wanamuziki
wengine wanapaswa kuchaguliwa kwa
uangalifu kama viongozi wa maeneo mengine
ya huduma za Shule ya Sabato na wanapaswa
kupimwa kwa viwango vilevile. (Angalia uk.
92, 144). Baraza pia linaweza kumteua mpiga
kinanda wa vitengo vingine”. (CM, uk. 96)
Vijana Waadventista:
Maafisa wa AYS – “Kanisa huwachagua
maafisa hawa wa AYS: Kiongozi wa Vijana,
msaidizi wa kiongozi wa vijana, Katibu-
mtunza hazina, msaidizi wa Katibu-mtunza
hazina, mwongozaji wa nyimbo, mpiga
kinanda, na mdhamini (ambaye anaweza
kuwa mzee). Kwa kuwa muziki unachukua
nafasi muhimu katika kuunda tabia za vijana,
waimbaji hawana budi wachaguliwe kwa
uangalifu kama maafisa wengine wa AYS”.
(Angalia uk. 92, 96.) (CM, 102)
Kuchagua Waratibu wa Muziki – “Kanisa ni
lazima lichukue uangalifu mkubwa katika
kuwachagua viongozi wa kwaya, ikiwachagua
wale tu waliojitoa kabisa na wanaotoa nyimbo
sahihi kwa huduma zote za ibada za kanisa
na mikutano. Muziki wa kidunia au ule
wenye asili iletayo maswali, kamwe
usiingizwe kwenye huduma zetu.” (CM, 92).
“Viongozi wa nyimbo ni lazima wafanye kazi
kwa ukaribu sana na wachungaji na wazee
wa makanisa ili kwamba uchaguzi wa nyimbo
uoane na wazo kuu la hubiri. Kiongozi huyu
wa nyimbo yupo chini ya usimamizi wa
mchungaji au wazee wa kanisa na hafanyi
kazi kwa kujitegemea. Kiongozi wa nyimbo
anapaswa kushauriana nao kuhusu nyimbo
zitakazoimbwa na uteuzi wa waimbaji na
wanamuziki.” – (CM, uk. 92)
Idara na Huduma zinatakiwa kuteua
Wakurugenzi wa muziki, na kulitaarifu
baraza la kanisa ili liwapitishe wale
waliochaguliwa. Uchaguzi wa viongozi wa
muziki wa idara za Shule ya Sabato na Vijana
umefafanuliwa na kusisitizwa.
Uangalifu mkubwa utumike katika kuchagua
viongozi wa muziki makanisani. Baraza la
kanisa ni lazima libatilishe/liidhinishe
viongozi wote wa vikundi/kwaya zote ambazo
kanisa limevisajili. Kila idara ichague kiongozi
wake na kupeleka kwenye baraza la Kanisa ili
kubatilisha au kuidhinisha..
Kanisa linaweza kuwa na viongozi kadhaa wa
muziki wanaoongoza nyimbo kwenye idara
zao, huduma, au makundi. Lakini kanisa ni
lazima lichague mkurugenzi mmoja wa
muziki, msaidizi/wasaidizi, kutegemeana na
mahitaji ya kanisa, watakaoratibu viongozi
wengine wote wa muziki kutoka idara
mbalimbali za kanisa, huduma au vikundi.
(CM, 171).
Mratibu wa muziki ni mjumbe wa baraza la
kanisa. – (CM, 125). Huchaguliwa na kibaraza
cha uchaguzi. (CM, uk. 171)
Mkurugenzi/Mratibu/Kiongozi (Mratibu
Mkuu) wa muziki wa kanisa):
Ni mjumbe wa baraza la kanisa.
Ni lazima apimwe na kiwango kile kile cha
juu kilichotumika kuwachagua viongozi
wengine wa kanisa.
Ni kiongozi muhimu asaidiaye maandalizi ya
ibada. Hufanya kazi chini ya “Msimamizi wa
Mimbari/Ibada”. – (Wachungaji na Wazee wa
Kanisa)
Ndiye anayepaswa kuchagua nyimbo na
waimbaji watakaoendana na wazo kuu la
hubiri la siku hiyo.
Ndiye atakayeandaa ratiba ya Kwaya
(waimbaji)/Vikundi vya Waimbaji,
Waimbishaji, na Ala za muziki ikiwa
zitakuwepo.
Ndiye atakayehamasisha na kusimamia
filosofia ya Biblia/Kanisa kuhusu muziki.
Makanisa yaweza kuunda Kamati ya Muziki
itakazoongozwa na Mratibu wa Muziki wa
Kanisa itakayosimamia huduma za muziki
kanisani. Wajumbe wa baraza hili wanaweza
kuwa wasaidizi wa Mratibu mkuu (anaweza
pia kutumika kama katibu wa kamati),
waratibu wa muziki kutoka kwenye maidara,
na viongozi wakuu wa kwaya. Wajumbe
wengine wanaweza kuwa viongozi wa Chama
cha Vijana, Mkurugenzi wa Huduma za
Watoto, na Mkurugenzi wa Huma za
Washiriki. Mzee wa kanisa na mchungaji ni
maafisa wa kamati hii.
Ukubwa wa kamati utategemea ukubwa na
mahitaji ya kanisa. Kamati itafanya vizuri
kazi yake kama itakutana walau mara moja
kwa mwezi. Baraza la kanisa linaweza
kukasimu baadhi ya mambo mepesi
yahusianayo na muziki kwa kamati hii.
Kuwachagua Waimbaji – “Muziki mtakatifu ni
sehemu muhimu ya ibada ya hadhara. Kanisa
ni lazima litumie uangalifu katika kuchagua
wanakwaya na wanamuziki wengine
watakaowakilisha vizuri kanuni za kanisa. Ni
lazima wawe washiriki wa Kanisa, au
washiriki wa Shule ya Sabato, au wanachama
wa Chama cha Vijana Waadventista. Kwa
kuwa wanachukua nafasi inayooneka na watu
katika huduma za kanisani, wanatakiwa kuwa
kielelezo cha unyenyekevu na tabia njema,
katika mwonekano na mavazi yao. Mavazi ya
kwaya yatategemea uchaguzi wao. (CM, uk.
92).
Makanisa yanaweza kuwa na kwaya nyingi.
Kuwa na kwaya ya watoto ni njia ya
kuwasaidia kuwalea kiroho, kuwaunganisha
na familia ya kanisa, na kuwashirikisha
kwenye ushuhudiaji. (CM, uk. 92)
MAONI
1. Waimbaji ni lazima wachaguliwe na kanisa
2. Kanisa ni lazima lisajili kwaya/vikundi vya
uimbaji kwa kuwachagua waimbaji na
kuwabatilisha/kuwaidhinisha viongozi.
3. Kwa kuwa waimbaji ni wahubiri, ni lazima
wawe kielelezo, hasa katika mwonekano na
mavazi.
4. Waimbaji ni lazima wawe waongofu wa
kweli. Kwaya na Vikundi vingi vya uimbaji ni
maskani ya Mwovu. Vimejaa wivu, majivuno,
migogoro, mashindano, uzinzi, uasherati,
ubinafsi n.k.
5. Hebu na wajiundie sheria na kanuni zao
wenyewe. Kanisa lijiepusha kutunga na
kusimamia sheria kwa waimbaji. Kanuni ya
kanisa imetoa viwango vya kutosha, hebu
kanisa livitumie hivyo.
Kanisa linaweza kuwa na zaidi ya kwaya
moja, ikiwemo na kwaya ya Watoto. Zote hizo
ni kwaya za Kanisa. Epukeni kupendelea
kwaya au kikundo kimoja cha uimbaji na
kuvipuuza vingine. Kanisa linapaswa
kuvipenda vikundi na kwaya zote na kuvitia
moyo.
Ijumaa, 27 Mei 2016
Muziki wa Kikristo
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni