Utangulizi:
Kumkubali kiongozi kuna
matokeo yake. Ukubali wako unamaanisha
kwamba unamkubali mtu huyo aweze
kuongoza na kufanya maamuzi ya msingi.
Mathayo anaendelea na mwendelezo wake
wa kuthibitisha kwamba Yesu ni Masihi,
Yesu ni Bwana. Sasa Mathayo ananukuu
matokeo ya kukataa kumfuata Yesu kwa
dhati. Hebu tuzame kwenye somo letu la
Biblia ili tujifunze zaidi!
I. Kuingia
A. Soma Mathayo 21:1-3. Je,
ungetilia mashaka maelekezo haya endapo
Yesu angekupatia hayo maelekezo?
(Ningepata ugumu sana kuchukua vitu vya
thamani kwa msingi kwamba nitamwambia
mwenye navyo “Bwana anawahitaji.” Hata
hivyo, ikiwa Yesu anaweza kuyaona mambo
yajayo, ninawezaje kutilia shaka jambo
lolote analolisema?)
B. Soma Mathayo 21:4-5.
Mathayo anathibitisha jambo gani hapa?
(Kwa mara nyingine, Mathayo anathibitisha
kuwa Yesu anatimiza unabii kwamba yeye
ni Masihi. Utaona kwamba anakuja kwa
upole.)
C. Soma Mathayo 21:6-9. Soma
Mathayo 16:20. Jambo gani limetokea? (Sasa
ni wakati wa kutangaza kuwa Yesu ni
Masihi.)
1. Makutano wanasema nini
kumhusu Yesu? (Kwamba Yesu ni “Mwana
wa Daudi,” Yeye ajaye “kwa jina la Bwana,”
na “Hosana.”)
2. Soma Zaburi 118:25-26.
“Hosana” maana yake ni “utuokoe sasa” au
“tafadhali tuokoe.” Je, Zaburi 118
inatufundisha jambo gani la ziada kuhusu
makutano kupaza sauti? (Kwamba Yesu
ndiye anayekuja kuwaokoa. Kitendo hiki
kinatangaza kwamba Yesu ni Bwana na
Masihi aliyeahidiwa.)
D. Soma Mathayo 21:10-11. Je,
jibu hili lilisababisha matatizo? (Soma
Mathayo 2:3-6. Ikiwa watu walikuwa wana
ufahamu juu ya unabii wa Masihi, kusema
kwamba Yesu alikuwa anatokea Nazareti
kungesababisha mtafaruku.)
1. Je, ungefanya nini endapo
ungekuwepo mahali pale ukisikiliza jambo
hili? (Natumaini ningefanya uchunguzi
zaidi!)
II. Hekalu
A. Soma Mathayo 21:12-13.
Tulisikia wanachokisema watu wengine
kumhusu Yesu. Tumefuatilia mfululizo wa
uthibitisho wa Mathayo kumhusu Yesu. Yesu
anajizungumziaje hapa? (Analiita hekalu
kuwa ni “nyumba yangu” na anaonesha
mamlaka juu ya kile kinachoendelea
hekaluni.)
B. Soma Mathayo 21:14-15. Je,
viongozi wa dini wanaudhika kutokana na
Yesu kuwaponya watu? (Soma Mathayo
21:16. Walikasirika kuhusu Yesu kuitwa
“Mwana wa Daudi” na yeye (Yesu)
kuenenda kama kiongozi wao.)
C. Soma Zaburi 8:1-2. Hili ndilo
fungu ambalo Yesu analinukuu. Fungu hili
linabainisha jambo gani? (Kwamba Yesu ni
Bwana, Kwamba Mungu anabariki sifa
anazopewa kutoka kwa watoto, na sababu
ya kufanya hivyo ni “kuwanyamazisha,
kuwakomesha adui na mijilipiza kisasi!”)
III. Mtini
A. Soma Mathayo 21:17-19. Je, hili
ni jambo jema au baya? Je, Yesu
anauangamiza mti kutokana na hasira?
1. Mtini umetenda jambo gani
lililosababisha uangamizwe? (Majani yake
yanakudanganya na kukufanya udhani
kuwa una matunda.)
2. Je, hili ni fundisho kwa
Wakristo wanaojiita kuwa ni Wakristo?
B. Soma Mathayo 21:20-22. Hivi
karibuni nilitazama sinema iliyoonesha
miujiza kadhaa isiyo na maana (ya kipuuzi).
Watu waliota meno ya dhahabu, vito vya
bandia vilitengenezwa bila kutumia
rasilimali yoyote, nk. Asili ya kipuuzi ya
miujiza hiyo ilinifanya nishangae na
kutafakari asili yake. Je, tunashughulika na
miujiza isiyo na maana katika Mathayo 21:
kuufanya mtini unyauke na kuhamisha
milima? (Mti ni fundisho kwa wanafiki.
Milima inaweza kuwa inawakilisha
changamoto na matatizo yaliyopo maishani
mwako. Yesu anatuambia kuwa imani ndio
jibu kwa changamoto za maisha.)
IV. Shamba la Mizabibu
A. Soma Mathayo 21:33-36.
Wapangaji wanaweza kujenga hoja gani
kutokana na mwenendo (tabia) wao?
(Hawana kisingizio kwa ajili ya jambo hili.)
B. Soma Mathayo 21:37-39. Nia
ya kumwua mwana wa mwenye shamba ni
ipi? (Mali. Uroho/ulafi. Wizi.)
C. Soma Mathayo 21:40-43. Yesu
anasema huu ni muujiza kuhusu viongozi
wa dini na watu watakaomwua (Yesu).
Walitaka mali gani? Shamba lao la mzabibu
lililoibwa ni lipi? Mungu alitarajia taifa lake
teule kuzaa matunda ya roho. Badala yake,
walijielekezea faida na kujisifu wao
wenyewe.)
D. Fikiria tena kuhusu mtini
ulionyauka. Je, kweli huo ni muujiza wa
kipuuzi? Uangamivu wa kipuuzi? (Hii
ilielezea sababu ya taifa la Kiyahudi
lililomkataa Yesu litakavyoangamizwa hivi
karibuni.)
E. Soma Mathayo 21:44. Je, hizi
ndizo chaguzi zetu mbili maishani?
F. Soma Mathayo 21:45. Je,
walengwa wa mjadala wa Yesu wana
mashaka? (Hapana. Mathayo anabainisha
jambo hili kwa dhahiri kabisa.)
V. Harusi
A. Soma Mathayo 22:1-5. Kwa nini
wale walioalikwa harusini hawaji?
(Wametingwa na shughuli nyingi sana.)
1. Kisingizio chao kinafananaje
na nia ya wale waliotaka kuiba shamba la
mzabibu? (Makundi yote mawili yalikuwa
yanatafuta kujipatia fedha. Walikuwa
wanataka kuongeza mali zao.)
2. Harusi ni ya muhimu kiasi
gani kwa mfalme?
B. Soma Mathayo 22:6-7. Je, hii
ni haki? (Wao ni wauaji! Walimdhihaki na
kumkasirisha mfalme wao.)
1. Je, si kitendo kikubwa kupita
kiasi kuwaua watu kwa sababu
wamekudhihaki na kukukasirisha? (Kwa
mara nyingine, tafakari muktadha uliopo.
Hapo awali Mathayo alielezea kisa cha mtini
na kisa cha shamba la mizabibu. Kuwa
mnafiki, kuipinga injili, kuwatendea vibaya
na kuwaua wafuasi wa Mungu, na
kumkataa Mungu kuna matokeo yake.)
C. Soma Mathayo 22:8-10. Hapa
kigezo cha kuwachagua watu ni kipi? Je,
kuna wanafiki na watu wabaya katika kundi
hili? (Mwaliko ulikuwa kwa ajili ya watu
wote. Watu “wabaya” (pamoja na wema)
waliutikia mwaliko. Kigezo cha kuchaguliwa
ni kuukubali mwaliko.)
D. Soma Mathayo 22:11-12. Kuna
jambo gani la kushangaza kuhusu kutokuwa
na mavazi sahihi? Watu hawa walitolewa
kutoka sehemu mbalimbali za mitaa,
walikuwa wamevaa mavazi ya kuendea
sokoni na kufanya manunuzi mengineyo,
mavazi ya kazini, na mavazi kwa ajili ya
mapumziko ya kawaida!
1. Unadhani kwa nini mtu
mmoja pekee ndiye hakuwa amevaa mavazi
sahihi? (Hii inatusaidia kujaza mashimo
katika kweli zisizoepukika. Lazima kila mtu
alikuwa na upungufu kwenye suala la
mavazi, sio mtu mmoja pekee. Hivyo,
tunajifunza kuwa lazima mfalme atakuwa
aligawa mavazi rasmi ya harusi kwa wageni
wote, lakini mtu huyu aliyakataa.)
a. Hebu tuangalie mantiki hapa.
Mwishoni mwa fungu la 12 linatuambia
kuwa mtu yule “alitekewa.” Je, tunaweza
kuongezea kweli zipi nyingine? (Mfalme
hana makosa. Ikiwa mfalme aliwatoza fedha
kwa ajili ya kupata mavazi maalumu, ikiwa
mavazi hayo hayakuwatosha, ikiwa mtu yule
hakufahamu lolote kuhusu mavazi
maalumu, basi angetoa kisingizio. Kwa
namna fulani alidhani kwamba alikuwa
sahihi kuyakataa mavazi ya mfalme.)
b. Jambo gani linaweza kuwa
lilimfanya mtu huyu adhani kuwa yuko
sahihi kukataa kuvaa vazi maalumu la
harusi lililotolewa na mfalme? (Aliyapenda
mavazi yake zaidi. Hakuhitaji ukarimu wa
mfalme, alikuwa mtu mwenye kujali sana
suala la mavazi.)
(1) Vipi kuhusu wewe? Je,
unajivunia kazi zako?
E. Soma Mathayo 22:13. Jambo
gani linamtokea mtu huyu? (Anafungwa na
kutupwa gizani.)
1. Hebu tujikite mwishoni mwa
fungu hili. Hisia gani zinasababisha kulia
na kusaga meno? (Ilikuwa rahisi sana
kuyakubali mavazi ya mfalme. Anawezaje
kufanya kosa kama hilo katika kufanya
uamuzi?)
F. Soma Mathayo 2:14. Tuliona
kuwa kila aliyetajwa kwenye kisa
alikaribishwa. Yesu anamaanisha nini kwa
kusema “wateule ni wachache?” Mtu mmoja
pekee ndiye anayeonekana kushangaa
kuikosa harusi. (Jibu pekee lenye mantiki ni
kwamba Yesu anarejea (anazungumzia)
uchaguzi binafsi. Wageni wote walioalikwa
waliukataa mwaliko wa mfalme kwa sababu
walikuwa na shughuli nyingi sana kiasi cha
kushindwa kuwa wasikivu. Hawakuwa
marafiki wa mfalme. Kwa dhahiri
hawakutaka kuja harusini kwa sababu
waliwatendea vibaya watumwa wake.)
G. Rafiki, vipi kuhusu wewe? Je,
una shughuli nyingi sana, maisha
yamekusonga sana kiasi cha kushindwa
kushughulikia mwaliko wa kumpokea na
kumkubali Yesu kama Bwana na Mwokozi
wako? Au, je, u miongoni mwa watu
wachache wanaodhani kwamba haki yao
inatosha kabisa? Kwa nini usiwe msikivu,
ukatubu na kulipokea vazi la haki ya Yesu
sasa hivi?
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni