Jumamosi, 28 Mei 2016

Lessoni juma hili

Utangulizi: Jeffrey Brauch, aliyekuwa Mkuu
wa Shule ya Sheria katika Chuo Kikuu cha
Regent, ni mmojawapo wa watu wa pekee
sana niliowahi kukutana nao. Mara zote
alionekana kuyaelekeza mawazo yake yote
kwangu tulipokuwa tukizungumza.
Ninapokuwa ninazungumza na watu
wengine, ninasikitika kwamba kwa ujumla
huwa ninawaza mambo yangu. Nina
uhakika anaenenda vivyo hivyo kwa kila
mtu – kwamba anayaelekeza mawazo yake
yote kwa watu anaozungumza nao. Jeff
anayaishi yale ambayo Mathayo
anayafundisha juma hili: kuishi maisha ya
kuwajali watu wengine. Hebu tuchimbue
somo letu ili tujifunze zaidi!
I. Watoto
A. Soma Mathayo 18:1-4. Nani
aliye na mawazo yenye msimamo thabiti
kuhusu malezi ya watoto: wazazi wenye
watoto kadhaa au watu wasio na watoto?
1. Je, watoto unaowafahamu ni
wabinafsi kwa asili? Je, huwa
wanajipendelea wao wenyewe kuliko watu
wengine? (Kutokana na kile nilichokiona,
watoto wanafanana nasi tu – wamezaliwa
dhambini.)
2. ikiwa hilo ni kweli, je, Yesu
anazungumzia jambo gani?
B. Soma tena Mathayo 18:1. Kwa
nini mtu atake kuwa mkuu katika ufalme
wa mbinguni? (Ili aweze kuwatawala watu
wengine.)
1. Je, watoto hawako hivyo?
(Watoto wadogo ni tegemezi kwa kiwango
cha juu sana. Hata kama wana tabia
nyingine mbaya, kwa mfano kuwa wachoyo/
wabinafsi, bado wanahitaji msaada na
wanalitambua hilo.)
C. Angalia tena Mathayo 18:4.
Yesu anatuambia nini basi kuhusu tabia
njema? (Kwamba tunatakiwa
kujinyenyekeza kwake na kumtegemea yeye
– kama mtoto anavyowategemea wazazi
wake.)
D. Soma Mathayo 18:5-6. Hili
linahusianaje na alichokimaanisha Yesu
kuhusu watoto kuwa tegemezi? (Kwa kuwa
watoto ni tegemezi, watu wazima wana
wajibu wa kuhakikisha kwamba
wanawafundisha vizuri na kuwatendea
watoto vyema kwa mujibu wa ushawishi
wetu mzuri.)
II. Dhambi
A. Soma Mathayo 18:7. Je,
umewahi kumsikia mtu anayenufaika
kutokana na msemo wa kiovu kwamba,
“Nisingefanya hivyo mtu mwingine
angefanya. Nami pia naweza kuwa
mmojawapo wa watu wanaopata fedha
kutokana na kitendo hicho.”
1. Jibu la Yesu kwa swali hilo ni
lipi? (“Ole wako!” uovu utakuja, lakini
ingekuwa heri uovu huo usitokane nawe
(usipitie kwako).)
B. Soma Mathayo 18:8-9. Je,
dhambi inaanzia mkononi mwako, mguuni
mwako au kwenye jicho lako? (Hapana.
Dhambi inaanzia akilini (mawazoni).)
1. Unakielewa kile anachokisema
Yesu? (Yesu anabainisha madhara ya
dhambi. Watu wanatenda dhambi kutokana
na wanachodhani ni manufaa yatokanayo
na vitendo hivyo vya dhambi. Yesu anasema
ni heri kupoteza kitu cha muhimu kuliko
kutenda dhambi.)
C. Soma Mathayo 18:10. Je, Yesu
anazuga kwa kuyazungukazunguka maoni
yake, na amerukia tena kuwazungumzia
watoto? (Yesu yupo kwenye mada ile ile.
Hatimaye watoto watakabiliana na dhambi,
lakini ni heri dhambi hiyo isipitie kwako.)
D. Soma Mathayo 18:12-14.
Yumkini umewahi kusikia kisa cha kondoo
tisini na kenda na kondoo mmoja
aliyepotea. Yesu anamaanisha nini kwenye
huo mfano wa watoto? (Katika tamaduni
nyingi watoto hawathaminiwi. Katika baadhi
ya tamaduni watoto wanatumikishwa. Yesu
anatufundisha kuwa watoto wana thamani
kubwa sana – kila mmoja wao.)
E. Soma Mathayo 18:15-17. Lengo
la kushugulikia tofauti zetu na matatizo kwa
kutumia njia hii ni lipi? (Lengo ni kumfanya
mtu huyo asikilize na kutafakari.)
1. Inamaanisha nini
kumchukulia mtu kama “mpagani au mtoza
ushuru?”
a. Je, ni sahihi kuwatendea
wapagani tofauti?
III. Kanisa
A. Soma Mathayo 18:18.
Tumejadili suala la kupeleka mashauri ya
watu kanisani. Uamuzi wa kanisa ni wa
muhimu kwa kiasi gani?
B. Hebu turejee nyuma na
tusome Mathayo 16:18-19. Tulipojifunza
suala hilo kitambo kifupi kilichopita
nililifanya kuwa jambo la kiroho kwa
kusema kuwa wale wanaoelewa kwamba
Yesu ni Mungu na kumpokea
“wanafunguliwa” na wale wanaomkataa
“wanazuiliwa” mbingui. Je, sikuwa sahihi?
(Huu muktadha mpya unaonesha kuwa
sikuingia kwa kina zaidi kwenye suala la
matumizi ya dhana hiyo kivitendo. Yesu
anatuambia kuwa kanisa limepewa
mamlaka ya kiroho hapa duniani.)
1. Mamlaka haya yana ukomo
gani? Je, kanisa linaweza kubadili siku ya
ibada? Je, kanisa linaweza kumbadilisha
Yesu na kutupatia mwombezi/mpatanishi
mbadala? (Muktadha uliopo katika Mathayo
18 unazungumzia mfarakano kati ya
washiriki wa kanisa.)
C. Soma Mathayo 18:19-20.
Kanisa linatakiwa kuwa kubwa kiasi gani ili
liweze kuwa na aina ya mamlaka ambayo
tumekuwa tukiyajadili? Je, kanisa la watu
wawili linatosha?
1. Unapokaa na kuyatafakari
mafungu haya, unadhani ni jambo gani la
msingi analolimaanisha Yesu? (Mbingu
zinafanya kazi kupitia kwetu. Mungu
anatupatia mamlaka.)
2. Je, hili linahusiana kwa
vyovyote vile na mjadala wa Yesu uliopita
kuhusu watoto? (Yesu anatufundisha kuwa
wanyenyekevu na kumtegemea. Hiyo
inabainisha kiwango cha “mamlaka” yetu
hapa. Mamlaka yetu yanatakiwa kuendana
na mapenzi ya Yesu yaliyobainishwa. Hii
inamaanisha kwamba kanisa halipaswi
kuweka sheria zinazokinzana na
mafundisho makuu ya Mungu. Kwa kuwa
tunayo haya mamlaka, tunatakiwa kuwa
makini sana jinsi tunavyoyatumia.)
IV. Msamaha
A. Soma Mathayo 18:21-22.
Namna pekee ya kuwa na uhakika kwamba
tunazo mara sabini na saba ni kwa
kuandika. Je, haya ndio maelekezo ya Yesu
kwetu?
B. Soma Mathayo 18:23-30.
Unamchukuliaje mtu ambaye alikuwa
anadaiwa mamilioni kutomsamehe mdeni
wake aliyekuwa akimdai kiasi kidogo?
C. Soma Mathayo 18:31.
Mashuhuda walisikitika, kama jinsi
ulivyosikitika! Je, ni kwa sababu mtu
aliyewiwa deni dogo hakusamehewa mara
saba, achilia mbali mara sabini na saba?
D. Soma Mathayo 18:32-33.
Bwana anasema kuwa tatizo ni lipi?
(Rehema. Sio kuendeleza kile
anachokiamrisha Yesu, bali ni kuwa na
rehema kwa wale wanaoomba msamaha.)
1. Kipimo cha msahama
maishani mwako ni kipi? (Yesu alikufia kwa
ajili ya dhambi zako. Dhambi yako i
kinyume na Mungu. Tunaathiriwa na
dhambi, lakini kuvunja sheria ya Mungu ni
dhambi dhidi yake. Sisi ndio yule mtumwa
aliyesamehewa “mamilioni.”)
E. Soma Mathayo 18:34-35. Yesu
anatoa onyo gani?
1. Inamaanisha nini “kusamehe
… kutoka moyoni?”
V. Ndoa
A. Soma Mathayo 19:3-6. Je, Yesu
anaamini maelezo ya uumbaji? (Anayaamini
kwa uthabiti mkubwa kiasi kwamba
anajenga hitimisho la kiroho kutokana na
maelezo ya uumbaji.)
B. Soma Mathayo 19:7-9. Je,
unadhani ni kama ajali tu kwamba huu
mjadala wa ndoa mara moja unaufuatia
mjadala kuhusu msamaha?
1. Je, mjadala wa ndoa
unaboreshaje uelewa wetu wa suala la
msamaha? (Ikiwa mara zote mwenzi
anatakiwa kumsamehe mwenzi wake, basi
hatupaswi kuwa na talaka. Hii inatuonesha
kuwa rehema inatokana na mpango wa
Mungu kwa ajili ya ndoa na maisha.)
2. Je, mwenzi anaweza kusamehe
“kutoka moyoni” kitendo cha mwenzi wake
kutokuwa mwaminifu, na bado akataliki
kutokana na kutokuwepo kwa uaminifu?
(Ndiyo. Msamaha haumaanishi kutelekeza
(kutotumia) akili ya kawaida.)
C. Soma Mathayo 19:10. Baadaye
katika sura hii ya kitabu cha Mathayo Yesu
anasema kuwa ni vigumu kwa tajiri
kuokolewa. Soma Mathayo 19:25. Wanafunzi
wa Yesu wanayachukuliaje mafundisho
yake? (Wanashangaa. Kwao kitendo hicho
hakionekani kuwa sahihi. Haiwaingii akilini
kutokana na uelewa wao juu ya mapenzi ya
Mungu.)
D. Soma Mathayo 19:11-12 (ndoa)
na Mathayo 19:26 (utajiri). Yesu anatoa
maoni gani kuhusu mafundisho ambayo ni
magumu kuyaelewa na kuyafuata? (Kwamba
Mungu atatenda kazi pamoja nasi ili
kuyafanya mambo yanayoonekana kuwa
hayawezekani yawezekane.)
VI. Ujira
A. Soma Mathayo 20:1-12. Je,
unakubaliana na wale wanaonung’unika?
Jiweke kwenye nafasi ya wale waliofanya
kazi kutwa nzima!
B. Soma Mathayo 20:13-16. Ikiwa
Yesu anatufundisha somo kuhusu Ufalme wa
Mbinguni, na sio ujira, je, kuna kipi cha
kujifunza? (Mungu haangalii usawa tu. Yeye
ndiye usawa. Lakini, yeye ni zaidi ya usawa.
Anatupatia kile tunachostahili, na anatupatia
zaidi ya tunachostahili. Anafanya mambo
yasiyowezekana yawezekane.
C. Rafiki, Mungu anakujali.
Anawajali watoto tegemezi. Anatutaka tuwe
mbaraka kwa watu wengine, badala ya
kutafuta tu kile tunachodhani kuwa ni
usawa.
VII. Juma lijalo: Yesu Akiwa
Yerusalemu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni