(Mathayo 12)
Somo limetafsiriwa na Mgune Masatu.
Utangulizi: Kama mwanasheria, ninaamini
katika sheria. Kuwa na sheria sahihi
husaidia kuwa na uhuru kamili, ikiwemo
uhuru wa dini. Mungu anaamini katika
utawala wa sheria, vinginevyo Yesu
asingekuja kutimiza matakwa ya sheria kwa
niaba (ajili) yetu. Kinachowafanya
wanasheria wawe na kazi ni mgongano kati
ya sheria na mitazamo tofauti juu ya sheria
hizo. Somo letu juma hili linahusu
kuzichanganua sheria za Mungu. Hebu
tuzame kwenye somo letu la Mathayo ili
tuone kile tunachoweza kujifunza kuhusu
asili ya sheria za Mungu!
I. Sheria (Kanuni) ya Nira
A. Soma Mathayo 11:28-30. Juma
lililopita tuliyaangalia mafungu haya. Hebu
tuangalie kipengele kimoja cha ziada. Yesu
anatupatia “nira.” Je, hicho ni kitu kizuri au
kibaya?
1. Je, nira inafanana na sheria,
kwamba inatufunga? (Nira ni kikwazo,
lakini jambo jema ni kwamba Yesu ndiye
mtu mwingine aliyepo kwenye hiyo nira. Hii
inamaanisha kuwa katika kila jambo, kila
changamoto, kila tatizo, Yesu anakuinua.
Hiki ni kizuizi chenye manufaa. Kinaonesha
rehema.)
B. Soma Mathayo 12:1-2. Kwa
nini si halali kuvunja masuke? (Tatizo
halikuwa kuiba masuke (Kumbukumbu la
Torati 23:25), shtaka lilikuwa ni kufanya
kazi siku ya Sabato (Kutoka 20:8-11).)
C. Soma Mathayo 12:3-4.
Unalichukuliaje jibu la Yesu? Je, hilo silo
jibu wakujibulo wanao – kwamba watu
wengine pia wanafanya vivyo hivyo? “Huyu
anatenda hivyo hivyo, Yule pia anafanya
hivyo hivyo!”
1. Unadhani jibu gani litakuwa
zuri zaidi kuliko “watu wengine pia
wanafanya jambo hilo hilo?” (Ningejibu
kwamba hii sio kazi.)
D. Soma 1 Samweli 21:1-6. Je,
Daudi anasema ukweli kwa Mfalme Sauli
kuhusu kuwa kwenye safari ya kazi ya
utume? (Hapana. Ukisoma sura iliyotangulia
utaona kwamba Yonathani alimwonya Daudi
kuwa Mfalme Sauli anataka kumwua. Daudi
anamkimbia Sauli.)
1. Jambo gani linafanana kati ya
mustakabali wa Daudi na wanafunzi wa
Yesu? (Wana njaa.)
2. Je, hicho ndicho tunachopaswa
kujifunza kuhusu Sabato – kwamba ni sahihi
kuvunja sheria ikiwa una njaa?
a. Ikiwa hicho sicho cha
kujifunza, je, Yesu anafundisha juu ya
jambo gani?
(1) Kuwasaidia watu wengine ni
muhimu zaidi kuliko sheria?
b. Vipi ikiwa kuwasaidia watu
wengine ndio sheria kuu?
(1) Je, hicho ndicho kipimo? Je,
hiyo ndio kanuni (sheria)?
E. Soma Mathayo 12:5-8. Yesu
anamaanisha nini anaposema kwamba yeye
ndiye “Bwana wa Sabato?” (Yeye ndiye
anayeamua kilicho sahihi kufanyika siku ya
Sabato.)
1. Yesu anamaanisha nini
anaposema, “Nataka rehema, wala si
sadaka?” (Hosea 6:6) (Ikiwa wanafunzi wa
Yesu pamoja na Daudi wangejizuia kula,
hiyo ingekuwa sadaka. Hivyo, Yesu anasema
kuwa katika amri ya Sabato (na kwa
dhahiri, kwenye amri nyingine pia), lengo ni
kuonesha rehema.)
2. Je, hiyo ni sheria? (Nadhani ni
sheria. Angalia mtazamo wako kwenye nusu
ya pili ya Amri Kumi na kila sheria nyingine
inayofanana na hizo katika Biblia. Je, sheria
hizo zipo kwa ajili ya kutukwaza na
kutuangusha, na kututia dhambini? Au, zipo
hapo kwa kuwa Yesu anatupenda na
anatutaka tuishi maisha huru dhidi ya
matatizo yasiyo ya lazima? Nadhani sheria
zipo ili kutuonesha rehema – na hicho
ndicho anachokimaanisha Yesu. “Nira” yake
ni rehema kwetu.)
3. Utagundua kwamba amri ya
Sabato haipo kwenye “nusu ya pili” ya Amri
Kumi. Je, amri hiyo inahusu kumwabudu
Mungu au inahusu kuwa na maisha bora?
(Amri ya Nne ni kiunganishi cha amri
zinazomhusu Mungu na zile zinazowahusu
wanadamu wenzetu. Soma Marko 2:27-28.
Sabato ni siku ya pumziko kwa wanadamu,
lakini pia ni muda wa pekee wa kutafakari
kile ambacho Mungu amekifanya kwa ajili
yetu.)
II. Sheria (Kanuni) ya Mkono
Uliopooza
A. Soma Mathayo 12:9-10.
Ungejibuje swali hili ikiwa unaelewa
kwamba rehema ndilo lengo lililopo nyuma
ya sheria za Mungu? (Jibu ni dhahiri kabisa,
“ndiyo.”)
B. Soma Mathayo 12:11-13. Kisa
hiki kinakazia vipi visa vilivyotangulia
kuhusu kuvunja masuke na Daudi kula
mikate ya wonyesho? (Hii inaonesha
kwamba rehema ndio sheria kiongozi.)
1. Hebu tujikite kwenye kisa cha
Daudi kuhusu mikate ya wonyesho. Lengo la
hekalu na sherehe (taratibu) za hekalu
lilikuwa ni lipi? (Kuelezea ujio wa Yesu na
kufa kwa ajili yetu.)
a. Je, hiyo ilikuwa ni
kutuonesha rehema? (Ndiyo! Kuzipa
kipaumbele sheria zinazohusu mikate ya
wonyesho dhidi ya mahitaji ya Daudi
kungepuuzia maana yote ya taratibu za
hekalu – kwamba Mungu alikuwa anakuja
ili kutuonesha rehema!)
C. Je, unadhani Mungu ana
tabaka la sheria (kanuni)? Je, baadhi ya
sheria ni muhimu zaidi kuliko nyingine?
1. Katika sheria za Marekani,
kuna sheria inayotawala inayosema kwamba
hakuna sheria inayoizidi nyingine isipokuwa
tu kama kuna ukinzani wa moja kwa moja.
Kwenye visa tulivyoviangalia hadi sasa
(kuvunja masuke na uponyaji siku ya
Sabato/Daudi kula mikate ya wonyesho), je,
palikuwepo na ukinzani wa moja kwa moja
kati ya sheria ya rehema na Sabato au
sheria za hekalu? (Mambo ya Walawi 24:8-9
inakinzana moja kwa moja na Daudi kula
mikate ya wonyesho. Na kwa kuongezea,
Yesu anakiri kuwa kuna ukinzani (Mathayo
12:4). Ingawa sioni ukinzani kwenye
kuvunja masuke, Yesu alijizuia kujenga hoja
kwamba wanafunzi wake hawakuwa
wakifanya kazi. Nadhani anachokimaanisha
Yesu ni kwamba kuna tabaka la sheria.)
2. Je, kuna maelezo ya ziada
kuhusu mbadala wa tabaka la sheria
mbalimbali? (Kwamba sheria zote zina
maana moja – kuonesha rehema.)
D. Soma Mathayo 12:14. Viongozi
wa dini wanaonesha nini? (Hawadhihirishi
rehema. Wanaonesha chuki. Huu ni
ukiukwaji wa dhahiri wa sheria.)
III. Sheria (Kanuni) ya Rehema
A. Soma Mathayo 12:15-16. Baada
ya Yesu kufahamu njama ya kutaka
kumwua, anaondoka. Je, ilikuwa hatari
kwake kufanya uponyaji? (Ndiyo,
ingewachochea zaidi viongozi wa dini
kutaka kumwua Yesu.)
1. Pamoja na hayo kwa nini Yesu
anafanya hivi? (Rehema!)
B. Soma Mathayo 12:17-21.
Tunaambiwa kuwa Yesu atafanya nini?
(Kwa uwezo wa Roho Mtakatifu atatangaza
hukumu, na ataiongoza “hukumu
kushinda.” Ataleta tumaini.)
1. Yesu hatafanya nini? (Hatazua
wala kushiriki kwenye ugomvi au kulia.
Hatainua sauti yake. Hatawajeruhi zaidi
wale ambao tayari wameshajeruhiwa.)
C. Soma tena Mathayo 12:20.
“Utambi utokao moshi” umezimika.
“Mwanzi wenye mchubuko” uko hatarini
kuvunjika kwa sababu tayari una
mchubuko. Vitu hivi vinawaelezea watu wa
aina gani? Wagonjwa? Waliokata tamaa?
Waliopoteza moto wa imani?
1. Je, watu wanaohamasisha
mtindo wa maisha uliojaa dhambi, na wana
uhasama na dini, pia wanastahili kuwa
kwenye kundi la mianzi (matete) yenye
mchubuko na tambi zitokazo moshi?
IV. Sheria ya Hatari
A. Soma Mathayo 12:22-23. Watu
hawa wanaonekana kufikiri juu ya jambo
gani? (Wanaashiria kwamba Yesu ni
Masihi.)
B. Soma Mathayo 12:24. Viongozi
wa dini wanatoa madai gani? (Kwamba Yesu
anapewa uwezo na Shetani.)
C. Katika Mathayo 12:25-29 Yesu
anajenga mfululizo wa hoja zenye mantiki
akibainisha kwamba hatumii uwezo wa
Shetani. Soma Mathayo 12:30-32. Kwa nini
Yesu anazungumzia kunena “dhidi ya Roho
Mtakatifu” na kusema kwamba hiyo ni
dhambi isiyoweza kusamehewa? (Kuihusisha
kazi ya Roho Mtakatifu na Shetani ndio
dhambi isiyoweza kusamehewa.)
1. Asubuhi hii nilibadilishana
mawazo na mtu aliyekuwa anajenga hoja
kwamba muziki wa kisasa wa kumsifu
Mungu wenye mdundo ni wa kishetani.
Ninaamini kwamba muziki wa kisasa wenye
kusifu unahusisha, kwa kiasi fulani, Roho
Mtakatifu kuyaelekeza mawazo yangu kwa
Mungu moja kwa moja. Angalia 1
Wakorintho 14:14-17. Hata hivyo, suala
ninalotaka ulitafakari sio muziki, bali shtaka
la uwezo (nguvu) wa kishetani. Hatari ni
ipi? (Hatari iliyopo ni dhambi
isiyosamehewa! Wakristo wanaowatuhumu
Wakristo wengine kwamba wanatumia
uwezo wa Shetani wako kwenye hatari hiyo
hiyo ya dhambi isiyosamehewa. Wanatakiwa
kuwa na uhakika na mashtaka haya,
vinginevyo wasiwatuhumu.)
2. Je, yule mtu ambaye
hakukubaliana nami ametenda dhambi
isiyosamehewa? (Hii si sawa na mtego wa
waya. Tatizo ni kwamba Roho Mtakatifu
anatugusa na kutufanya tutambue dhambi
zetu. Yohana 16:8-9. Tunapoanza kuupinga
uwezo wa Roho Mtakatifu kwa kudai
kwamba uwezo huo ni wa kishetani,
tunaufukuzilia mbali uwezo huo wenye
mguso maishani mwetu. Ni mchakato, sio
shtaka moja.)
D. Rafiki, je, unaamini kwamba
rehema iko nyuma ya sheria za Mungu kwa
ajili ya maisha yetu? Je, utafanya uamuzi
leo, kuwaonesha watu wengine rehema ya
Mungu? Kupata pumziko kwenye rehema ya
Mungu kwako?
V. Juma lijalo: Bwana wa
Wayahudi na Mataifa.
Jumanne, 3 Mei 2016
Lessoni juma hili
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni