Alhamisi, 30 Juni 2016

Lessoni Alhamis, Jukumu la kanisa la urejeshaji.

🌳LESSON 🌳

🌲Alhamisi june 30 🌲

Jukumu la kanisa la urejeshaji.


🌲kama tulivyoona, Ulimwengu wetu, ingawa uliumbwa mkamilifu, ulianguka, kwa matokeo yenye kuleta uharibifu mkuu. Lakini mungu hakutuacha katika kile ambacho kingelikuwa hatima yetu, kuangamia milele,(hatima ambayo sayansi inasema inatungojea). Badala yake, hata kabla Ulimwengu haujakuwapo, mpango wa wokovu uliundwa, (angalia 1 pet, 1 :2) na kwa gharama kubwa isiyopimika kwake (Mungu), Yesu alikuja katika Ulimwengu huu na kuteseka msalabani na aliahidi kuwa atarudi. Wakati ambapo kila kitu kitakuwa kimepita na dhambi imeangamizwa, Ulimwengu ule uliokuwa umepotea utarejeshwa upya kikamilifu.

🌲Hata hivyo, kinachoshangaza ni kwamba hata sasa mungu anatuita sisi, kanisa lake, kuwa na sehemu ya kazi ya kufanya katika kuelekea kwenye urejeshwaji huu.

   Soma marko 2:1-12 kisa cha jinsi ambavyo marafiki fulani kwa uthabiti walifanya kazi  kwa   pamoja katika kumpeleka aliyekuwa amepooza kwa Yesu. Ni kwa jinsi gani kisa hiki kinaelezea wajibu wa kanisa katika uponyaji na urejeshaji upya wa watu?



🌲Nyumba ilikuwa imejaa watu kwa sababu Yesu Alikuwa pale. Upendo wake kwa watu uliwavuta makutano. Wale watu wanne waliotoboa tundu kwenye paa ili kumfikisha kwa Yesu huyu mtu aliyekuwa mgonjwa wa kiroho, kiakili, na kimwili. Ndipo Yesu alipomrejesha upya mtu huyo kwa kusamehe dhambi zake, kumpatia amani moyoni na kumwamuru kusimama na kutembea. Yesu alidhihirisha kwamba hakuna mtu anakuwa ameponywa kwa hakika isipokuwa amerejeshwa upya katika kila jambo.

  Mtume Yohana  alielezeaje sababu ya Kristo kuja humu duniani? Tunaweza kupata tumaini gani kutoka kwenye ahadi hizi? Soma yohana. 10:10, 1 yoh. 3:8.



🌲Imeelezwa kuwa yohana 10:10 ni muhtasari wa ujumbe wa waadventista wa sabato. Kwa uwazi hili ndilo lililokuwa tamko la utume la Yesu. Jukumu kuu la mwili wa kristo, kanisa lake, halina budi kufuata nyayo zake na kuziharibu kazi za yule mwovu kwa kubadilisha mauti na mahali pake  kujazwa kwa uzima tele,  (angalia Mdo. 10:38:,1 yoh. 2:6).kanisa limeitwa kufanya kazi kwa ubia na kristo kwa kuwasukuma watu kuelekea kwenye  kurejeshwa upya katika sura ya Mungu-kimwili, kiakili na kiroho.

👫Ni watu gani ambao kwa sasa wanahitaji msaada wako, Msaada ambao kwa namna ya pekee umeandaliwa ili uweze kutoa?

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni