Alhamisi, 30 Juni 2016

Mwenyekiti SHC apata ajari.

Breaking news.  Mwenyekiti wa Conference ya Nyanda za Juu Kusini (STUM) Mchungaji Kenan Mwasomola Amepata Ajali Mida ya Saa 2 Usiku wajana Tarehe 29/06/2016 eneo la Nyandekwa Katikati ya Igunga na Nzega Wakati Akielekea Kirumba Mwanza kwa Sherehe ya Jubilee ya miaka 50 akiwa na Gari la Office.

Kwa Mujibu wa Taarifa ya Shuhuda wa Ajali hii Ambaye pia alikuwa ndani ya Gari hilo Mch. D Bambaganya Amesema Mwenyekiti Ameumia Maeneo ya Mbavu na Mke wa Mwenyekiti Ameumia Shingoni na Begani na Tayari wote wamelazwa  Hospitali ya Mission ya Nkinga Na hali zao Zinaendelea Vizuri.

Sababu ya Ajali inasemekana ni Tuta lililo kuwa katika barabara ambayo lami imekwanguliwa na Kulikuwa hakuna alama yeyote ya kuelekeza. Jambo lililo sababisha Gari kubilingita juu chini na hatimaye kusimama.

Kwa Mujibu wa wenyeji wa eneo hilo wanasema Tuta hilo limesha sababisha Ajali nyingi zilizo poteza maisha ya watu. Tena hata asubuhi hii wakati nikipokea Habari hizi kunagari jingine dogo limeponapona kupata Ajali mbaya.

Tuendelee Kumuombea Mwenyekiti na Majerui wote ili BWANA awaponye na kuendelea na Kazi katika kipindi hiki cha Utume kwanza ni wakati wa mavuno. Amen

By. Mchungaji Haruni Kikiwa - Mbalizi District Pastor SHC

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni