Jumatano, 29 Juni 2016

Lessoni j5 UREJESHWAJI KATIKA KRISTO.

🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻
☂☂☂☂☂☂☂☂☂☂☂
   Lesson ya leo Jumatano,  Jun 29.

Somo!!  UREJESHWAJI KATIKA KRISTO.

'' 👉🏾 Vitoto vyangu, ambao kwamba nawaonea utungu tena mpka Kristo aumbike ndani yenu'' (Gal. 4:19).👈🏽

--------------------------------
✍🏽⏩ Kwa asili, tuliumbwa tukiwa viumve wakamilifu na watimilifu kwenye Ulimwengu mkamilifu na mtimilifu. Kwa bahati mbaya, paradiso hii ya kabla ya Anguko ilipotezwa kwa njia ya dhambi, na ulimwengu huu tunavyoufahamu kwa sasa,  Umejaa vifo, vurugu, mateso, hofu, na ujinga. Mpango wa wokovu uliasisiwa ili kuurudisha ulimwengu huu katika ukamilifu wake wa Asili.
Kristo alikuja ili kukirejesha kilichokuwa kimepotezwa wakati wa Anguko.

✍🏽⏩ '' Hapo mwanzo Mungu alimuumba mtu kwa mfano wake mwenyewe.
Alimjalia kwa sifa au tabia zilizo bora. Akili yake ilikuwa katika ulinganifu mkubwa, na uwezo wake wote uliokuwa ndani yake  ulikuwa katika upatanifu.  Lakini Anguko na madhara yake vimepotosha  vipawa hivi.

✍🏽 Dhambi imeharibu na ilikuwa karibu kabsa kuifuta sura ya Mungu kutoka kwa mwanadamu. Ilikuwa ni katika kuirejeaha upya  ndipo mpango wa wokovu ulibuniwa,,  na mwanadamu alipewa maisha ya majaribio. Kumrejesha upya katika ukamilifu aliokuwa ame7mbwa nao hapo mwanzo na hili ndilo kusudi kubwa la maisha - kusudi lililo la msingi kwa mengine yote.'' E.G White, patriarchs  and prophets, Uk 595.
Ingawa urejeshwaji upya huu hautakamilika  mpaka wakati wa mbingu mpya na nchi mpya, mchakato huo umekwisha  kuanza ndani yetu sasa!!.

Soma👉🏾 Wagalatia 4:19. Chochote kile alichokuwa anataka kujihusisha  nacho wakati huo, ni wazo gani muhimu la Kiroho Paulo analilenga hapa?
--------------------------------
✍🏽 Katika vitabu vya Waebrania 1:3 Yesu anatambulishwa kama sura ya Mungu, '' Yeye ni mng'ao wa utukufu wa Mungu, na mfano kamili wa hali ya Mungu mwenyewe '' (BHN)

(Linganisha na Yn 14:9; 2Kor:4:4; Kol.1:15). Anatamani kulingana nasi ili kuirejesha upya sura ya Mungu ndani yetu. Ikiwa tutakubali, Kristo aliye Sura ya Mungu atakuwa ndani yetu; ''Kristo yuko ndani yenu, na jambo hilo linamaanisha kwamba, ninyi mtaushiriki utukufu wa Mungu. (Kol. 1:27 BHN).

✍🏽⏩ Uzoefu wa mwisho wa kurejeshwa upya katika sura yake utatokea wakati wa ujio wa pili wa Yesu.  (Soma 👉🏾1kor. 15:49, 1Yoh. 3:2). Hata hivyo, Kristo anapokuwa ndani yetu, nasi ndani yake, mchakato wa Kurejeshwa upya katika Sura ya Mungu unaanza tukiwa upande huu wa kurejeshwa upya katika sura ya Mungu unaanza tukiwa upande huu wa mbingu. Na jambo hilo linapotokea, tutakuwa na shauku ya kuwaleta wale walio katika jamii zetu kwake yeye anayeweza kuwarejesha upya na wao pia.

(MATUMIZI MAISHANI )

👉🏾 Ingawa kazi hiyo, ya kuturejesha upya, inaanza ndani yetu sasa, kwa nini siku zote inatupasa kukumbuka kuwa urejeshwaji upya hautakamilika hadi ujio wa pili wa Yesu?
            '' MWISHO''

🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻
☂☂☂☂☂☂☂☂☂☂☂

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni