Jumatatu :usomaji wa Biblia :1Nyakati 14 juni 27
🙊ANGUKO NA MATOKEO YAKE 🙈
✍🏾Biblia haisemi kuwa ulipita muda gani toka Uumbaji ulipokamilika na Anguko. Hatujui ni muda gani ulipita, siku, majuma, au miaka.
✍🏾 Hata hivyo, kile tunachofahamu ni kwamba, kulikuwa na Anguko, na matokeo yake yalikuwa ya mara moja na yalikuwa dhahiri.
✍🏾Matokeo yaliotajwa mwanzoni ya Adamu na Hawa kula tunda la mti wa ujuzi wa mema na mabaya yalikuwa ni utambuzi wao wa ghafla kuwa walikuwa uchi (Mwa. 3:7). Walitafuta kujificha kutoka mbele za Mungu. Mavazi yao ya nuru sasa yakiwa yametoweka. (angalia patriarchs and prophets cha Ellen G. White uk. 57). Uhusiano wao wa karibu waliokuwa nao kwa Mungu wao ulivurugwa kwa sababu ya uhusiano wa karibu mpya waliougundua kwa ubinafsi wa uovu. Kwa hiyo Mungu akatafuta kuwaelimisha wanandoa hawa wa kwanza kuhusiana na matokeo yaliosababishwa kwao na Dhambi yao.
SOMA aya zifuatazo na utambue matokeo ya mara moja ya dhambi ya Adamu na Hawa kama inavyoonekana katika kila fungu la maneno.
Vile vile ni kwa namna gani matokeo yake Yale yanadhihirika leo?
Mwa. 3:8-10......................
Mwa. 3:12..............................
Mwa. 3:13.................................
Mwa. 3:16................................
Mwa. 3:17-19..........................
----------------------—
✍🏾Hakuna shaka, Anguko lilikuwa halisi, Anguko lilikuwa kitu kibaya, Anguko lilikuwa na matokeo mabaya na ya kusikitisha kwa jamaa ya wanadamu. Kisa kirefu na cha kusikitisha cha historia ya mwanadamu tangu wakati huo hadi kwenye matukio ya wakati huu, yanafunua matokeo mabaya na ya kusikitisha ya dhambi.
✍🏾Inatupasa kuwa na shukrani kiasi gani kwa ahadi kuwa siku moja msiba wa dhambi utamalizika na kutokomezwa usijirudie kamwe.
🌑Ni kwa namna gani tunaishi kila siku kwenye matokeo ya dhambi zetu?
✅✅✅✅✅✅✅✅✅✅✅
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni