Jumamosi, 25 Juni 2016

Somo la 13: Msulubiwa na Mfufuka

Utangulizi:
Somo letu la Mathayo juma hili
linawamulika wasaliti wawili na mwanamke
mmoja aliyejitoa kikamilifu kwa Yesu. Je,
inamaanisha nini hasa kumsaliti Yesu?
Inamaanisha nini kujitoa kikamilifu kwa
Yesu? Kwa nini matokeo ni tofauti sana kwa
msaliti mmoja kuliko mwingine? Hebu
tuzame kwenye somo letu la Biblia ili
tujifunze zaidi!
I. Wapanga Njama na
Mwanamke
A. Soma Mathayo 26:1-2. Kwa
dhahiri hizi ni habari zenye kukatisha
tamaa sana. Kwa nini uwaambie wanafunzi?
(Yesu alitaka kuwaonya (kwa mara nyingine
tena).)
1. Hiyo inaashiria nini kuhusu
umuhimu wa matukio ya siku za mwisho?
(Yesu atatuonya kuhusu matukio ya
muhimu na yale yenye changamoto.)
B. Soma Mathayo 26:3-7. Tunazo
taswira mbili kinzani. Taswira ya kwanza ni
ya kundi linalopanga kumwua Yesu na
nyingine ni ya mwanamke ambaye anajitoa
kwa hali ya juu kwa ajili ya Yesu. Kutokana
na Yesu kuelewa mustakabali wa mauti
yanayomkabili kitambo kifupi kijacho,
unadhani alijisikiaje kuhusu huyu
mwanamke? (Hii ni nyota inayong’aa
kwenye mazingira ya giza. Ningemshukuru
sana mwanamke huyu.)
C. Soma Mathayo 26:8-9.
Unauelezeaje mwitiko wa wanafunzi?
Wameambiwa kwamba Yesu anakaribia
kufa, je, hawapaswi kushiriki katika
kumfanyia jambo la pekee? (Nadhani
wanafunzi walipingana na uhalisia kwa
kutokubali kuamini kile alichowaambia
Yesu. Hawakutaka kuamini kuwa atakufa.)
1. Je, ungekuwa na mwitiko gani
endapo wewe ndiye ungekuwa huyu
mwanamke na kusikia ukosoaji huu?
Umejitoa kwa kununua hii marhamu, na
sasa wanafunzi wanakukosoa!
2. Kuna dhana katika fungu hili
ambayo nataka uiangalie. Wanafunzi
hawakusema kwamba mwanamke alipaswa
kutoa fedha kwa masikini badala ya
kununua marhamu, bali walisema kuwa
angeweza kuiuza hiyo marhamu. Hii
inatuambia nini kuhusu jinsi mwanamke
huyu alivyoipata hii marhamu? (Ilikuwa ni
zawadi. Kwa uthibitisho, hakikuwa kitu
ambacho angeweza kumudu kukinunua.)
D. Soma Mathayo 26:10-13. Hii
ilikuwa ni zawadi, kuna mtu alidhamiria
mwanamke huyu aweze kuitumia zawadi
hiyo. Badala yake, alichagua kujikana nafsi
kwa kutoitumia kama walivyopendekeza
wanafunzi. Je, wanafunzi walikuwa na haki
ya kumwambia kufanya matumizi
anayopaswa kujikana nafsi ili kutoyafanya?
(Hawana ushauri sahihi. Yesu anasema
kuwa alichokifanya mwanamke huyu
kitaongelewa katika kumbukumbu lake na
historia yote.)
1. Je, zipo fursa
zinazokuzunguka kuinua mioyo ya watu
waliokata tamaa kwa kuwatendea wema?
2. Je, pia watazungumzia
duniani kote kuhusu habari ya wanafunzi
kumkosoa mwanamke huyu aliyejikana
nafsi?
3. Kuna tofauti gani kati ya
mtazamo wa mwanamke na ule wa
wanafunzi? (Alikuwa amejitoa kwa Yesu
kikamilifu. Wanafunzi walijitoa kufanya
uamuzi wa matumizi bora ya marhamu
yake.)
II. Yuda
A. Soma Mathayo 26:14-16. Je,
Yuda ndiye aliyemkosoa mwanamke?
1. Unadhani kwa nini Yuda
alimsaliti Yesu? Je, sasa aliamua kumchukia
Yesu? (Ninazo nadharia mbili. Kwanza,
hakuamini kwamba Yesu angeweza kuuawa
– na kwamba angeweza pia kupokea fedha
kama thawabu kwa kumlazimisha Yesu
kujitangaza kuwa Mfalme. Pili, kwamba
Yesu alimaanisha sana juu ya kifo chake,
kiasi kwamba alistahili fedha kwa muda
alioupoteza kwa kuzunguka kwake kote kwa
muda wa miaka mitatu. Katika nadharia
zote mbili, alijitumainia yeye mwenyewe na
wala hakumtumaini Yesu.)
2. Soma Mathayo 18:7. Je,
maelezo haya yanazungumzia hali aliyo
nayo Yuda?
B. Soma Mathayo 26:17-22.
Wanafunzi walichukulia kwamba bado
usaliti ulikuwa haujaanza kufanyika. Kwa
nini? (Kwa sababu wote, isipokuwa Yuda,
walikuwa hawajamsaliti Yesu.)
1. Tumejadili mawazo yangu
kuhusu njama ya Yuda. Wanafunzi wengine
walikuwa wanafikiria nini – je, mawazoni
mwao waliwaza kwamba wangeweza
kutengeneza fedha kiasi katika hiki
kizungumkuti cha kubadilika kwa matukio?
(Walikuwa na masikitiko kuhusiana na
habari hii, na walikuwa na wasiwasi
kwamba wanaweza wasiwe watu wa
kutegemewa.)
2. Kwa nini Yesu alibainisha
ukweli kwamba atasalitiwa? Unadhani
alitaka kumfanya Yuda ajisikie hatia, au
alitaka Yuda aachane na mpango wake, au
Yesu alikuwa na wazo jingine mawazoni
mwake?
C. Soma Mathayo 26:23-25. Hili
ni tukio kubwa sana mawazoni mwa
wanafunzi. Je, unadhani walielewa kwamba
Yuda alikuwa anamsaliti Yesu?
1. Ikiwa ndivyo, kwa nini
hawakumshambulia Yuda? Kwa nini
wasimtishe ili asiweze kumsaliti? Kwa nini
wasimzuie (wasimweke kizuizini) ili asiweze
kumsaliti Yesu?
2. Yuda aliposema, “Ni mimi,
Rabi?,” je, hiyo inatuambia nini kuhusu
utayari wake wa kuachana na mpango
wake? (Yuda alikuwa ameshafanya uamuzi.
Sasa alisema uongo ili kuuficha uamuzi
wake.)
III. Mlo Wake wa Mwisho
A. Soma Mathayo 26:26-30. Jiweke
kwenye nafasi ya wanafunzi. Je, ungeweza
kufahamu chochote ya kile ambacho Yesu
alikuwa anakizungumzia? Kwanza anasema
anakaribia kuuawa, na sasa kiishara
anazungumzia kuhusu kuula mwili wake na
kuinywa damu yake.
B. Angalia kile tulichojifunza hadi
sasa. Wanafunzi wanadhani kuwa wana
mawazo mazuri zaidi kuliko ya mwanamke.
Yuda anadhani ana mawazo bora kuliko
mawazo ya Yesu. Unadhani Mathayo
anamaanisha nini kwa kuandika hapa haya
maelezo ya Mlo Wake wa Mwisho?
IV. Petro
A. Soma Mathayo 26:31-35.
Unadhani Petro anasema ukweli? (Soma
Yohana 18:10-11. Katika maelezo ya Yohana
juu ya kukamatwa kwa Yesu, Petro
anachomoa upanga wake, yuko radhi kufa
kwa ajili ya Yesu. Anasema ukweli.)
1. Petro anatofautianaje na
Yohana? (Yesu haenendi ili kujinufaisha
yeye mwenyewe.)
B. Hebu turuke mafungu kadhaa
baada ya kukamatwa kwa Yesu. Soma
Mathayo 26:57-58. Je, bado Petro
anadhihirisha ujasiri mkubwa?
C. Soma Mathayo 26:69-75. Jana,
nilimsikiliza mtu aliyekuwa na dhamira
njema akisimulia jinsi ambavyo tunatakiwa
kutia bidii kujiepusha na dhambi, kwamba
tunakabiliana na Shetani, na kwamba bora
tuwe tayari kwa ajili ya pambano dhidi ya
dhambi (huku Yesu akitusaidia). Anguko la
Petro ni lipi? Anadhihirisha kasoro gani
kitabia? Kuna dosari gani kwenye haiba
yake ni tatizo kubwa? (Petro alikuwa na
Yesu muda wote tena kwa ukamilifu.
Alikuwa radhi kupambana hadi kufa.
Lakini, alichanganyikiwa kwa kitendo cha
Yesu kutopambana na kitendo cha Yesu
kuzungumzia kuhusu kuula mwili wake na
kuinywa damu yake. Yesu hakujua nini cha
kufikiri.)
1. Ni jambo gani basi ambalo
Petro alipaswa kulifanya? (Kumtumaini Yesu
tu.)
D. Hebu turejee kwenye somo
letu. Kwenye mjadala kati ya wanafunzi na
mwanamke juu ya matumizi bora ya
marhamu, nani alikuwa anamtumaini Yesu
na nani alikuwa anayatumaini mawazo yake
mwenyewe? (Wanafunzi walikuwa
wanayatumaini mawazo yao wenyewe.)
E. Katika maelezo ya usaliti wa
Yuda, je, Yuda anamtumaini nani?
(Anajitumainia mwenyewe. Anadhani ana
ufahamu (anajua) zaidi ya Yesu.)
F. Kwenye kumbukumbu ya Mlo
Wake wa Mwisho, Yesu anamaanisha nini
kuhusu kuula mwili wake na kuinywa damu
yake? (Wokovu unapatikana kwa njia ya
Yesu pekee. Yeye ndiye Kondoo wa kafara
wa huduma ya patakatifu (hekalu). Yeye
ndiye njia pekee ya kuufikia wokovu.)
G. Petro hadhani kwamba yeye ni
mwerevu zaidi ya Yesu. Ingawa yu radhi
kufa, kwa namna fulani ameharibu mambo
na kumkana (kumsaliti) Yesu. Je, Petro
alipaswa kufanya nini ili kuepuka matokeo
haya? (Soma tena Mathayo 26:31-33. Petro
angeweka kando majivuno yake na
kumwuliza Yesu, “Nawezaje kuepuka
kufanya hivyo? Niambie ninachotakiwa
kukifanya ili niweze kukusaidia kikamilifu
badala ya kukukana.”)
H. Rafiki, sidhani kama ni wazo
jema kujiandaa kwa ngumi ili kupambana
na Shetani. Sidhani kama ni wazo zuri
kujikita kwenye kuchunguza na kukomesha
kila dhambi maishani mwako. Kiini cha
maisha yako lazima kiwe ni kumtumaini
Mungu, hata pale dunia yote inapoonekana
kuwa nje kabisa ya udhibiti. Unaweza
kuanza kufanya hivyo sasa hivi kwa
kumwomba Roho Mtakatifu kila siku,
kuongoza kila uamuzi wako na kila wazo
lako ili iweze kuwa tabia yako kumtumaini
Mungu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni