🌳🌳🌳🌳🌳🌳🌳🌳🌳
Juni 25-Julai 1
''UREJESHWAJI UPYA WA VITU VYOTE''
Sabato Mchana.
Somo la Juma Hili: Mwa. 1:26,27; Kum.6:5; Mwa. 3:8-19; Yak.4:4; Gal.4:19; Marko 2:1-12; Yoh. 10:10.
FUNGU LA KUKARIRI:
'' Mungu akamuumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.'' (Mwanzo 1:27).
⏩✍🏽 Kile kinachompasa Mtu kufanya ni kutazama kila upande unaomzunguka,
Kuuangalia Ulimwengu, katika ujirani, kujitazama yeye mwenyewe ili kuliona jambo hili.
⏩ Na jambo hili ni lipi? Jambo fulani limekwenda vibaya sana.
Jambo hili linaitwa Anguko, linaitwa dhambi, linaitwa Uasi, na linaitwa Pambano Kuu.
⏩✍🏽 Hata hivyo, Habari njema ni kwamba, Jambo hili si la kudumu. Halitakuwepo siku zote. Yesu alikuja na kufa kwa ajili ya dhambi za ulimwengu na aliahidi kuja tena,
⏩ na atakapokuja tena,,, hakuna hakuna jambo lolote la dunia hii litakalosalia. Badala yake, Ufalme mpya, Ufalme wake wa milele utaanza. '' Na katika siku za Wafalme hao Mungu wa Mbinguni atausimamisha ufalme ambao hautaangamizwa milele, wala watu wengine hawataachiwa enzi yake; bali utavunja falme hizi zote vipande vipande na kuziharibu, nao utasimama milele na milele'"" (Dan 5:44).
Urejeshwaji upya wa kushangaza kiasi gani!!
⏩✍🏽 Lakini hatutangoja hadi Ujio wa pili kwa ajili ya Urejeshwaji Upya kuanza. Wale walio katika Kristo ni viumbe vipya kwa sasa. (2Kor 5:17). na tumechaguliwa ili tufuatishe na kufananishwa na mfano wa Yesu sasa.
(Rum 8:29). Pia, yeye anatuita na kutuwezesha, kama kanisa lake ili kwamba tuweze kufanya kazi ambayo itawarejesha watu wengine pi.
Mwisho.
Karibuni kwa michango na maswali kwa Lesson ya leo, Kuchangia kwenu ndo kupanuka kwa Maarifa ya Kimbingu.
📖📖📖📖📖📖📖📖📖
🙏🏾🙏🏾🙏🏾🙏🏾🙏🏾🙏🏾🙏🏾🙏🏾🙏🏾
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni