Jumatano, 6 Julai 2016

Je unatunza au Unapamba?

SOMO: NI KUPAMBA? AU NI KUTUNZA NYWELE.
Wanawake wanashindwa kutofautisha kati ya “kutunza nywele” na “kupamba nywele “lazima utofautishe kati ya kutunza na kupamba.
Kamusi ya Kiswahili sanifu inatoa maana ya maneno haya:
“Kutunza” maana yake ni kukiweka kitu katika hali nzuri ili kisiharibike.
“Kupamba” maana yake ni kuweka urembo au nakshi zaidi ya kawaida yake.
Wasichana wengi na wanawake kwa ujumla katika ulimwengu huu wa leo wameamua kupamba nywele zao badala ya kuzitunza. Kupamba nywele  kunaweza kuwa na hasara kadha wa kadha ambazo huambatana na matumizi ya vitu vitumikavyo kupambia nywele hizo. Hasara hizo ni za kiuchumi na kiafya lakini hasara nyingine kubwa ni hasara ya kiroho.

(a)  Madhara ya Kiuchumi.

i.             Gharama kubwa katika kupamba nywele. Wanawake wengi wanatumia pesa nyingi kununua mapambo ya nywele, kwenda saluni, na kuwalipa mafundi wa kuzilemba na kuzipamba. Wanadhani kwa kufanya hivyo watapendeza na kuongeza kukubalika kwao, kumbe wanajiweka katika sehemu mbaya mno. Wavulana wazuri japo hawawaambii waziwazi, wanawaogopa wasichana hao kwa sababu wamejiweka katika daraja la watu wa gharama kubwa. Vijana hao wa kiume huwa wanawakwepa kwa kuhofia gharama za kupamba nywele za mwanamke huyo.

ii.           Kupamba nywele kunahitaji muda wa kutosha ili kuzishughulikia. Muda mwingi ambao ungeweza kutumika kwa shughuli nyingine za kimaendeleo, unapotezwa kenye upambaji wa nywele. Kama muda huo ungelitumika kuzalisha au kufanya kazi fuluni ya kiuchumi basi wanawake hao wangepunguza gharama kubwa za maisha na kuongeza uzalishaji kwa matumizi mazuri ya muda.

(b)  Madhara ya kiafya:

MADHARA YA KIAFYA YANAYOTOKANA NA MATUMIZI YA VIPODOZI.
Mamlaka ya madawa na chakula (marekani) imetafsiri vipodozi kama kemikali ambazo hutumika mwilini kwa lengo la kuosha, kuongeza uzuri na mvuto bila kuharibu kiungo cha mwili na kazi yake. Kwa lugha rahisi vipodozi hubadilisha muonekano wa mtumiaji. Vipodozi huhusisha; kemikali za ngozi, “lotion”, poda, marashi (perfumes), mafuta ya mdomo (lip sticks and lip shine), rangi za kucha, kemikali za uso na macho (eye and facial make up), rangi za nywele (hair colours), marashi ya nywele (hair spray and gels), mafuta ya kuogea na michoro ya mwili (tattoos).

Baadhi ya kemikali (ingredients) za vipodozi zenye madhara mwilini ni;
(i)           Rangi za kucha zina kemikali iitwayo “sodium lauryl sulfate” ambayo husababisha ugonjwa wa ngozi (dermatitis).
(ii)           Kutumia “make up” kwa muda mrefu husababisha ugonjwa wa nywele za kope (eyelashes), ambao humfanya mtumiaji awe na hatari ya kupata ugonjwa wa macho (keratitis).
(iii)        Kemikali zinazotumika kutunza vipodozi (preservatives) kama “ureas” zinasababisha ugonjwa wa ngozi (dermatitis). Aidha kemikali zingine kama methyl, propyl na butyl zinaweza kusababisha saratani ya matiti (breast cancer).
(iv)         Vipodozi vinavyotokana na “petrol” au “paraffin” vinaziba vitundu
vidogo vidogo vya ngozi na kufanya ngozi isitoe uchafu vizuri na hivyo kusababisha chunusi.
(v)          Kemikali kama “oxybenzone” na “octylmethoxycinnamate” inaharibu mfumo wa hormone, hivyo kuathiri shughuli za kikemikali za mwili.
(vi)         “propylene glycol” inasababisha matatizo ya macho, saratani, inaathiri uzazi (wajawazito) na pia ni sumu endapo mtu atakunywa kwa bahati mbaya.
(vii)       “sodium lauryl sulphate” inayowekwa kwenye cream nyingi na shampoo inasababisha ngozi kuwasha, huingia mwilini kwa urahisi na hukusanyika kwenye jicho, ubongo, moyo na ini kwa muda mrefu, hivyo kuathiri utendaji wa viungo hivyo.
(viii)     Rangi za vipodozi zinasababisha saratani.
(ix)        Marashi (perfumes). Perfume (1) inaweza kutengenezwa na kemikali  hadi 200. Baadhi ya kemikali hizo husababisha maumivu ya kichwa, kizunguzungu, chunusi, kukohoa, ngozi kuwasha, aleji na kutapika.
(x)          Kemikali nyingi huharibu na kuondoa seli (cells) za ngozi zilizokomaa (melanin) na kuacha seli zilizo changa; hivyo kuathiri ulinzi ambao  ngozi huutoa dhidi ya vimelea vya magonjwa na mionzi ya jua. Kwa hali hii mwili upo hatarini kushambuliwa na vimelea vya magonjwa, saratani ya ngozi na kuumia kwa urahisi.
Kwa ufupi; kemikali (ingredients) zifuatazo ni htari kwa afya yako; methyl, propyl, butyl, ethyl diethanolamine (DEA) or Triethanolamine (TEA), Diazolidinyl urea, sodium lauryl, petrolatum, synthetic colours e.t.c
Lakini pia kemikali ya Methylmercury inoyotumika kwenye vipodozi na kemikali za kukuzia nywele ina madhara yafuatayo;
(a)  Kwa vitoto ambavyo bado viko tumboni (fetus), watoto wachanga waliozaliwa (infants) na watoto wakubwa kidogo (children), hupata madhara ya vipodozi hivyo kupitia mama zao wakiwa tumboni. Madhara hayo ni pamoja na kuadhiri ukuaji wa ubongo wa mtoto na mifumo ya mwili (effects on baby’s growing brain and nevous system).
(b)   It also affects peripheral vision and disturbances in the body, especially sensations (hisia katika) in the hands (mikono), feet (miguu) and around the mouth (maeneo ya midomo).
(c)  Lack of coordination movement (kuharibu mwondoko wa mwili); impairment (madhara katika) of speech (kuogea), hearing (kusikia), walking (kutembea) and muscle weakness (uthaifu wa misuli).
(d)  Husababisha ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi, saratani ya ngozi, saratani ya mifupa, saratani ya damu. Ingawa ugonjwa huchukuwa muda mrefu kudhihirika.
(e)  Disturbances in sensation, (kuharibu mifumo ya hisia ya ngozi).
(f)   Changes in never responses,(mabadiliko katika mwitikio wa neva).
(g)  Performance deficits on tests of cognitive function,(kuharibu uwezo wa kuelewa).
(h) Kidney effects, (madhara ya figo)
(i)   Respiratory failure,(kuathiri mifumo ya upumuaji).
(j)   Death,(hupelekea kifo).
(k)  Skin rashes and dermatitis, (michubuko ya ngozi na muwasho).
(l)   Mood swings, (kubadilika kwa hali ya mtu ovyo bila sababu)
(m)               Memory loss, (kupoteza uwezo wa kumbukumbu).
(n)  Mental disturbances, (kuvurugika akili).
(o)  Muscle weakness.
Walioadhirika na matatizo hayo waonane na wataalam wa Afya kwa msaada zaidi. Makampuni mengi hayaorodheshi kemikali zote zilizotumika kutengeneza vipodozi hususani  zenye madhara makubwa. Bidhaa nyingi zinapambwa kwa majina mazuri kama “natural” ama “organic” wakati zinamadhara makubwa kiafya.

TAARIFA YA WIZARA YA AFYA (2004) KATIKA HOSPITALI ZIFUATAZO:
Hospitali ya Mirembe na Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI).
Hospitali ya Mirembe inahudumia wagonjwa wenye matatizo ya akili, wakati hospitali ya oceanroad inhudumia wagonjwa walioathirika na magonjwa ya saratani. Kumbuka mpendwa hayo ni magonjwa yanayosababishwa kwa kiasi kikubwa na utumiaji wa kemikali katika vipodozi, ambapo athari zake huanza kuathiri mtoto akiwa bado yuko tumboni.

Hospitali ya Mirembe hutoa huduma za rufaa kwa wagonjwa wa magonjwa ya Akili. Katika mwaka 2004 iliweza kutoa huduma ya wagonjwa wa nje 33,067 na waliolazwa 3,010. Idadi ya vifo vilivyotokea katika mwaka 2004 kwa wagonjwa wa magonjwa ya akili ilikuwa asilima 4.4 ya idadi ya wagonjwa waliolazwa.
Magonjwa ya Akili kumi yaliyoongoza kwa wagonjwa waliolazwa mwaka wa 2004 ni Schizophrenia 61%, Epilepsy 229 (8.4)%, Organic brain syndrome 134 (6%), Acute psychosis, Psychoactive substance use disorders 14% Depression, Alcoholic psychosis 2% Manic-depressive psychosis, Mania 0.7%, Senile dementia 1.4%, Acute Psychosis 0.9%, Mental deficiency 0.5% na Anxiety neurosis 0.4%

Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI)
Taasisi ya saratani ocean road ni taasisi maalum ya kutibu magonjwa ya Saratani, kwa mwaka 2004 ilihudumia wagonjwa wa nje (OPD) 6,962 ambapo wagonjwa 2,947 walikuwa wa Saratani ya shingo ya uzazi na kati ya hao wagonjwa wapya walikuwa 992 na waliokuwa wakifuatiliwa ni 1,955. Wagonjwa 4,015 walikuwa na Saratani za aina nyingine ambapo 1,874 kati yao ni wapya na 2,141 walikuwa wakifuatiliwa.

Kuhusu wagonjwa, wagonjwa 2,312 walilazwa mwaka 2004. Jumla ya vifo 187 vilitokea kutokana na magonjwa ya Saratani. Saratani ya shingo ya uzazi iliongoza kwa 34.6% ikifuatiwa na Kaposis Sarcoma 14%, Oesophagial carcinoma 8.1 %, Saratani ya matiti 8.0 % pamoja na Saratani za Head and Neck 7.8% kati ya magonjwa kumi yaliyooongoza kwa magonjwa ya nje (OPD). Tiba ya mionzi ilitolewa kwa wagonjwa 30,045 ambapo Shingo ya uzazi ilioongoza katika viungo vilivyotibiwa kwa 65%, ikifutiwa na Head and Neck 10.5% pamoja na Oesophagus 6.3%. Zingatia idadi ya wagonjwa waliohudumiwa, waliokufa, jumla yao walioadhirika. Tazama pia magonjwa yaliyowafanya wengi kulazwa katika taasisi hizo za Afya. Utagundua kuwa vyanzo vya magonjwa hayo vinapatikana ndani ya vipodozi vinavyoonekana kupendwa na kutumiwa na wanawake wengi. Je, watumiaji watapona kwa hali hii, mabadiliko yasipofanyika?

Wapenzi watu wa Mungu, hata katika nchi ya Tanzania, Mamlaka ya chakula na Dawa (TFDA), imepiga marufuku baadhi ya vipodozi ambavyo vimeonekana kuwa na madhara makubwa kwa binadamu. Ikiwa taasisi hii yaweza kuwa na kitu chema cha kuionya jamii inayotumia vipodozi kumkosoa Mungu katika uumbaji wake, habari gani kwa sisi watu wenye nuru ya Mungu?. Kwanini tusiridhike na jinsi Mungu alivyotuumba? Huko ni kuwaka tamaa na kukosa kuwa na kiasi, ndipo tunafikiria kumkosoa Mungu katika uumbaji wake. Wanawake wanajiwekea makalio yasiyo yao, kupunguza matiti au kuyapandisha, kupaka rangi za kucha, mdomo na sehemu nyingine, kutumia dawa za kuongeza hips, kutumia dawa za kukuza nywele, kuweka nywele za bandia na kukoboa ngozi. Tusipo isikia sauti ya Mungu inayotuita leo kutoka Babeli, tutaangamia kwa magonjwa yaliyotajwa hapo juu, ambayo chanzo chake kikubwa ni matumizi ya hivyo vipodozi.

Soma taarifa ya gazeti hili la Mwananchi hapo chini, iliyoripotiwa 24 May 2012 20:48
MWANANCHI:

Thursday, 24 May 2012 20:48
Daniel Mjema, Moshi
WAKATI Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), ikipiga marufuku matumizi ya vipodozi hatari kwa afya za binadamu, vipodozi hivyo sasa vimetapakaa katika maduka mbalimbali ya vipodozi mkoani Kilimanjaro.
Hali ni mbaya zaidi katika mji wa Moshi na vitongoji vyake ambapo baadhi ya Maofisa wa Afya wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, wamegeuza biashara hiyo kuwa mradi ambapo ‘humalizana’ kiaina na wamiliki wa maduka hayo.
Uchunguzi wa gazeti hili ulibaini baadhi ya maduka hayo kuuza  vipodozi hivyo kwa usiri mkubwa kwa kutazama sura ya mteja ambapo sehemu kubwa ya wale wanaouziwa ni wanawake  huku wanaume wakitiliwa mashaka.

Vipodozi vilivyozagaa kwa wingi ni Carolight, Mekako, Maxi Light, Bio Carote, Carottene na G&G cream, Rico Cream, Princes Cream na Clare Cream ambavyo TFDA ilitangaza vipodozi hivyo kuwa na madhara makubwa kwa binadamu.

Maduka yaliyosheheni vipodozi hivyo yapo katika stendi kuu ya mabasi Moshi Mjini, stendi ya Soweto, Barabara ya Nyerere maarufu kama Double Road, maeneo ya KCMC na baadhi ya maduka ya bidhaa za rejareja yaliyopo kwenye makazi ya watu.

Katika kuthibitisha kuzagaa kwa vipodozi hivyo, mwandishi wa habari hizi aliamua kumkodi  mwanamke mmoja na kuzunguka naye katika maduka sita kununua vipodozi hivyo na akauziwa japo vilikuwa vikichukuliwa nje ya makabati ya bidhaa.

Habari zaidi zilidai kuwa Afisa mmoja wa Afya katika Manispaa ya Moshi(jina tunalo) amekuwa akipita katika maduka hayo mara moja au mbili kwa mwezi na kuchukua hongo ya kati ya sh100,000 na sh200,000 kwa kila duka.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, Dk. Christopher Mtamakaya alipoulizwa jana alisema hana taarifa juu ya kuzagaa kwa vipodozi hivyo na kuahidi kufanya operesheni ya kukagua maduka yote ya vipodozi.

Tayari TFDA ilishatoa taarifa kwa umma juu ya kuwepo kwa vipodozi karibu 200 ambavyo vimetengenezwa kwa madini hatari ya Hydroquinine, Steroids, Bithionol na Zebaki ambayo yana madhara makubwa kwa binadamu.
Taarifa hiyo ya TFDA inasema vipodozi hivyo hatari huweza kusababisha kansa ya ngozi kwa mtumiaji, akina mama kuzaa watoto wenye mtindio wa ubongo na uharibifu wa ini na figo na athari huchukua muda mrefu kutambuliwa.

Historia ya upambaji wa nywele katika Biblia.
Katika bibilia upambaji wa nywele uliambatana na wanawake waovu, wauaji, Malaya na wenye mashetani au waabudu mashetani. Kisa cha Yezebeli katika (2 Falme 9:30), kina onesha kuwa Yezebeli alizaliwa katika Ikulu ya sidoni katika nyumba ya waabudu mashetani au miungu. Miungu yao ilikuwa “ Baali au Bel” mungu mkuu wa kiume aliyeabudiwa kwa kutoa kafara za wanadamu. Bibilia inashuhudia ibada ya namna hiyo. “Nao wamemjengea Baali mahali pake palipo juu ili kuwachoma moto wana wao wawe sadaka za kuteketezwa kwa Baali (yer 19:5)” kando ya ibada hiyo ya kuchoma watoto, ilijumuisha uasharati.

Yezebeli akaolewa na Ahabu mfalme wa Israel. Binti huyu hakuacha ibada ya Baali katika taifa la Israel (1falme 18:4). Hivyo wale wanaooa mabinti wanao jipamba wakidhani watawabadilisha wanajidanganya huko ni kuleta moto wa kigeni katika familia yako na ndipo mtaungana kuabudu miungu mingine.

Lakini Yezebeli alikuwa mwongo na muuaji pia, (1 falme 21:1-16), ndipo baada ya miaka kadhaa, Yehu akaenda kulipiza kisasi, akamkuta huyu mwanamke na tabia yake ya kupamba nywele, Bibilia inasema “Yezebeli akapata habari akatia wanja akapamba kichwa chake ………(2 falme 9: 30), lengo lake la kufanya hivi kwanza aliamini miungu yake itamsaidia lakini pia alitaka Yehu amtamani ili asimuue. Lakini Yehu alipomwona hakumhurumia alimuua (2 Falme 9:33).

Kwahiyo tunaona kuwa upambaji wa nywele si wa wanawake wa kristo. Bali kiasilia ni wa waabudu mashetani ambao huenda sambamba na uovu, uuaji na uasherati. Kuweka nywele za badia zilizo na rasta, kuweka rangi (nyekundu, nyeupe au kahawia na kadhalika) na kuweka wanja, hayo yana kutia hasara kiuchumi, lakini pia yanaharibu sifa yako njema ya kiroho.

Ndugu wapenzi katika kristo nawasihi kwa neema ya Yesu epukeni kupamba nywele maana hayo ni kwa waabudu mashetani. Mungu anachotuagiza kufanya ni kutunza na wala sio kupamba nywele. “kujipamba kwenu kusiwe kujipamba kwa nje, yaani kusuka nywele na kujitia dhahabu na kuvalia mavazi(1peter.3:3).” kumbuka hapa maandiko yanazungumzia kupamba si kutunza. Mapambo yanayo kubaliwa hapa na ndiyo yanayo zungumzwa ni mapambo yasiyo haribika, yaani roho ya utulivu maana ndivyo walivyo jipamba wanawake watakatifu wa zamani (1 pet.3:4).

Katika ufunuo 2:20 anatajwa mwanamke kwa kuhusika na uovu kama uzinzi , “lakini nina neno juu yako  ya kwamba wamridhia Yule mwanamke Yezebeli yeye ajiitaye nabii na kuwafundisha watu wangu na kuwapoteza, ili wazini na kula vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu”. pia mwanamke wa ufunuo 17 naye pia ameonekana amepambwa lakini anatajwa kuwa mzinzi huwakilisha kanisa lililo asi.

Kwa hiyo ili nywele zako zikupatie heshima na kuvutia kukubalika kwako zitunze katika hali ya usafi usiziache zikakuletea usumbufu kichwani kama vile kuwasha na kuwa makao ya chawa na uchafu. Kwa kuziweka nywele katika hali nzuri inakulazimu kuziosha vizuri mara kwa mara kwa sabuni. Baada ya kuziosha zipake mafuta maalum ya nywele, sio madawa. Usiache nywele zako zinasokotana na kufanya zisipendeze, na unapojaribu kuzichana zinauma. Osha, paka mafuta na zichane. Biblia inasema “wala kichwa chako kisikose marhamu (Muhubiri 9:8).” Kwa nini wewe unaacha nywele zako kuwa chafu? Jaribu kutumia nywele zako kujipatia sifa njema, kanisani, nyumbani, shuleni, chuoni, au katika jamii inayokuzunguka. Jiepushe na mitindo isiyompa Mungu utukufu.

HITIMISHO:
MSIMAMO WA KANISA, THISDASO T.U, THISDASO DODOMA ZONE.
1kor.4:1 – Mtu na atuhesabu hivi; kuwa tu watumishi wa Kristo, na mawakili wa siri za Mungu. Hapo tena inayohitajiwa katika mawakili, ndiyo mtu aonekane kuwa mwaminifu.

Kwakweli kama wakristo, tunayo kila sababu ya kuwa kielelezo katika maeneo tunayoishi ili kuwa nuru kwa watu wengine wanaoteseka na mambo ya Dunia hii yasiyo na faida. “Na waende kwa sheria na ushuhuda; ikiwa hawasemi sawasawa na Neno hili, bilishaka kwa hao hakuna asubuhi” (Isaya 8:20). Kama wakristo ikiwa hatuendi sawasawa na Neno sisi kwetu hakuna asubuhi, maana hatutakuwa nuru kwa wtu.

Watu wa Mungu huongozwa na Neno la Mungu, ili liwakinge katika kushindana na mivuto ya walimu wadanganyifu na nguvu za uongo wa pepo za giza. Shetani anatumia kila hila awezayo kuwazuia ili awazuie watu kufahamu maarifa ya Biblia. Katika kila uamsho wa kazi ya Mungu, mkuu wa uovu huamka kufanya bidii zaidi; anajitahidi kupita kiasi kushindana na kristo na wafuasi wake. Angalia sana pepo hili baya la ibilisi la kutaka kukwamisha kazi ya Mungu lisikutumie kwa kazi zake, tumwombe Mungu atupatie uwezo wa kuzipinga hila za shetani, Tule kwa kiasi, Tunywe kwa kiasi, Tuhusiane kwa kiasi, Tuvae kwa kiasi, Tuongee kwa kiasi huku tukijua kuwa sisi ni chumvi ya Dunia.

Hii ni saa ya hatari kubwa.
Kitakacho vumilia mapigo saba ya mwisho ni tabia iliyo takatifu. Hitaji muhimu……Hitaji kubwa la kanisa la masalio si ongezeko la washiriki, wahubiri zaidi, au vifaa zaidi. Zaidi sasa hitaji kubwa leo ni watu waume na wake waliojazwa na Roho Mtakatifu. Kumaliza kazi ya Mungu, yatupasa tupokee kwa upya kila siku ubatizo wa Roho Mtakatifu.

“Hakuna hata mmoja anayedai utakatifu ambaye ni mtakatifu wa kweli. Wale ambao wameandikwa kuwa ni watakatifu katika vitabu vya Mbinguni hawajifahamu, nao huwa ni wa mwisho kujivunia wema wao wenyewe”.

“Wale ambao kwa kweli wanatafuta kukamilisha tabia zao za Kikristo hawatakubali kuwalazimu kuwa hawana dhambi. Maisha yao yanaweza kuwa hayana hatia, wanaweza kuishi maisha yanayowakilisha kweli walioipokea, kwa kadri wanavyoweka mawazo yao kudumu kwenye tabia ya kristo, kwa kadri wanavyokaribia sura yake ya kimungu….”watakamilishwa nao watayachukia mambo ya dunia hii yanayoonekana kuwavutia walio wengi.

Wale wanaojaribiwa kumsaidia Shetani kulaumu viongozi na washiriki katika kanisa la masalio, watafanya vyema kutafakari maonyo ya ujumbe wa Mungu katika mafungu yafuatayo; 6 T 42 – “Hhakuna chochote katika ulimwengu huu kinachopendwa kama Kanisa la Mungu. Mungu ana kanisa ulimwenguni, ambao ni watu wake waliochaguliwa wanaozishika amri zake. Anaongoza, si machipukizi yanayofarakana, si mmoja hapa na pale, lakini watu waliopamoja”. (kutayarisha njia sehemu ya pili, u.k 48).

“Hakuna kinacho mkosea Mungu kama tendo la kudharau mvuto wa wale wanaoifanya kazi yake. Atawahesabia kosa wale wote wanaomsaidia Shetani katika kazi yake ya kulaumu na kukatisha tama” (kutayarisha njia sehemu ya pili, u.k 48). “Yatupasa tuwe na bidii kubwa. Hatuna muda wa kutumia kwa kulaumu na kutoa mashitaka. (kutayarisha njia sehemu ya pili, u.k 48). “Lolote lililo baya, la chuki, kulaumu, kudhulumu, hayo si ya kristo, bali hutoka kwa Shetani” (kutayarisha njia sehemu ya pili uk 48)

“Kuvutwa kuingia katika kulaumu wengine, kungekuwa ni ishara ya hatari kwetu, kwani roho mtakatifu anapotutakasa na kutubadilisha, mioyo yetu itajazwa na upendo kwa ndugu zetu….” “Ijapokuwa ni kweli kwamba wengi wetu katika kanisa la Masalio wako katika hali ya Laodikia, ambao wengi watatikiswa na kutolewa, hata hivyo kanisa wako walio waaminifu ambao watasikia mashauri ya Kristo aliye Shahidi wa kweli…watatayarishwa kwa mvua ya masika, wakishiriki katika kutoa ujumbe pamoja na Kilio Kikuu na kuwa tayari kubadilishwa.

“Hili ni kanisa la Masalio. Mungu hataongoza kanisa lingine. Sasa ni wakati wa kujitayarisha kwa mvua ya masika. Na tungekumbuka kila siku kuwa kazi hii ya kujitayarisha yapasa ianze wakati wa mvua ya vuli” (kutayarisha njia sehemu ya pili uk 48)
Furaha yetu ya baadaye inategemea kuwa ubinadamu wetu, na uwezo wake wote, view katika kumtii Mungu na kuweka chini ya utawala wa Kimungu…” “Kristo anatamani kuwa kila mmoja wetu akate shauri mapema” “Bidii isiyo na kikomo ingekuwa yetu sasa”
Mwisho.
“Ombeni kuwa nguvu ya Roho Mtakatifu, ikiwa na uwezo wake mwenyezi, unaohuisha na kugeuza, uijie roho iliyolemaa kama nguvu ya umeme ikiufanya kila mshipa kuamka kwa uzima mpya, kumhuisha mwanadamu kutoka kwa ufu wake wa kidunia na hali ya kimwili”.
Mungu awabariki mnapojiandaa kila mmoja wetu kufanya mabadiliko kwa yale ambayo Roho amekushuhudia kupitia somo hili ya kwamba ufanye matengenezo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni