KUPASIMAMISHA UPYA
2014/2015
TUCASA | Southern Tanzania Union Mission 0
KUPAJENGA PALIPOBOMOKA NA KUPASIMAMISHA UPYA
LIMEANDALIWA NA: KAMATI KUU TUCASA UNION YA KUSINI
TUCASA-STUM
SOUTHERN TANZANIA UNION MISSION
2014/2015
KUPAJENGA PALIPOBOMOKA NA KUPASIMAMISHA UPYA 2014/2015
TUCASA | Southern Tanzania Union Mission 1
UTANGULIZI.
Tunaishi katika ulimwengu uliochanganyikiwa, ulimwengu usiotaka hekima za Mbinguni, tunakutana na changamoto nyingi ambazo wakati mwingine zinatukatisha tamaa, Kwa sababu ya changamoto hizo sehemu kubwa ya ukristo wetu imebomoka kukosa ujumla wa uahalisia wake, pamoja na hayo yuko yesu aliyetayari kutuongoza katika KUPAJENGA PALIBOMOKA NA KUPASIMAMISHA UPYA SAWIA NA NGUVU YAKO YA AWALI (WAKATI WA UBATIZO WAKO) Huyu yesu ni mwenye kutusogeza karibu naye daima, mahali ambapo ni patulivu na pana bubujiko la faraja, kituo cha amani, mahali pa joto la kiroho. Karibuni katika somo la juma hili, Fungua Moyo wako, mwambie Mungu akupe masikio ya kusikia, macho ya kuona na moyo wa nyama katika KUPAJENGA PALIPOBOMOKA. BWANA AWABARIKI SANA,
METHUSELA MASUNGA MWENYEKITI TUCASA SOUTHERN TANZANIA UNION MISSION.
KUPAJENGA PALIPOBOMOKA NA KUPASIMAMISHA UPYA 2014/2015
TUCASA |Somo la kwanza
1. TUMEZUNGUKWA NA WINGU KUBWA LA MASHAHIDI
Limeandaliwa na Godfrey J. Machota, Katibu Mkuu TUCASA-STUM
Utangulizi
Je! Hamjui, ya kuwa wale washindanao kwa kupiga mbio, hupiga mbio wote, lakini apokeaye tuzo ni mmoja? Pigeni mbio namna hiyo, ili mpate. Na kila ashindanaye katika michezo hujizuia katika yote; basi hao hufanya hivyo kusudi wapokee taji iharibikayo… {1kor 9:24-25}Paulo katika barua yake kwa wakorinto amefananisha maisha ya kikristo na mashindano ya mbio za riaza yaliyokuwa yanafanyika huko karibu na korinto. Katika michezo yote iliyokuwapo wakati wa wagiriki na warumi, mchezo wa mbio za riaza ulikuwa wa zamani kuliko yote na uliopendwa sana. Ulikuwa ukitazamwa na wafalme, mabalozi na watu wenye cheo serikalini. {AA 309.1}
Mashindano yaliongozwa na sharia kali, ambazo zilikuwa hazina kukata rufaa. Wale waliotamani majina yao yaingie kwenye mashindano hayo, walipaswa kufanya maandalizi ya kutosha. Mazoea mabaya ya ulaji na unywaji au jambo lolote ambalo lingeweza kushusha uwezo wa akili au nguvu za kimwili, yalipingwa vikali mno... {AA 309.2}
Lilikuwa sio jambo la ajaabu mtu kudondoka, kutoka damu mdomoni au puani na wakati mwingine kuzimia kabisa wakati akiwa katika mashindano, lakini washiriki wa michezo hii hawakuangalia uwezekano wao wa kudumu na ulemavu au hata kufa wakilinganisha na heshima kubwa ambayo ingefuata kama wangekuwa washindi. {AA 310.2}
Shindano la Imani
Katika waebrania 12:1 paulo anasema “Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu”
Paulo anayafananisha maisha ya ukristo na mashindano ya riaza, katika sehemu ya kwanza ya fungu anasema tumezungukwa na wingu kubwa la mashahidi, je hawa mashahidi ni kina nani? Ellen G. White anasema “wote wanaotuzunguka na wanaotutaza kwa ukaribu, kuangalia namna tunavyoenenda katika Imani tunayoikiri mbele yao. Katika muda wote na maeneo yote kwa kadiri iwezekanavyo ni lazima tuukuze na kuinua ukweli mbele ya ulimwengu” (MS 61, 1907; 7BC 934.11)
Anachokisema mjumbe wa Mungu ni kwamba katika maisha yetu tunazungukwa na watu wasio wa Imani yetu na wa Imani yetu pia ambao huwa mashahidi wa Imani yetu ya kwamba tunaenenda kama Imani yetu inavyotutaka au tunaishi kinyume na tunacho kihubiri. Kama vile wana riaza wanavyojiepusha na vitu au mambo yanayoweza kupunguza uwezo wao wa kimwili
KUPAJENGA PALIPOBOMOKA NA KUPASIMAMISHA UPYA 2014/2015
TUCASA | Southern Tanzania Union Mission 3
na kiakili na hivyo kuwakwambisha kutwaa taji zao za ushindi, vivyo hivyo wakristo wanavyopaswa kufanya ili washinde katika shindano hili la Imani
Paulo anasema “na tuweke kando kila mzigo mzito” mzigo ni jambo lolote ambalo ni kikwazo ambacho kinaweza kukupunguzia au kukuondolea kabisa nafasi ya kushinda, katika njozi ya ijara ya watakatifu Ellen G. White aliona watakatifu wakiwa katika safari kuelekea mji wa
Mungu na kadiri walivyozidi kuukaribia njia ilizidi kuwa nyembemba na pia walikuwa watua na kuachana na mizigo ambayo ingewachosha na safari, wale ambao waling`ang`ania mizigo yao njia haikuwatosha na hivyo walishindwa na safari.
Kila mzigo ambao unamdalilisha kristo ni lazima uwekwe kando haijalishi utakuletea maumivu kiasi gani kuuacha, lakini ni lazima uuweke kando, Paulo anasema “Hata mimi napiga mbio vivyo hivyo, si kama asitaye; napigana ngumi vivyo hivyo, si kama apigaye hewa; bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiri wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa” (1kor 9:26-27).
Hata kama itakulazimu kuteseka, kukataliwa au pengine kuonekana mshamba ni lazima juhudi zote zifanyike ili kuuweka kando kila mzigo usifaa, Yesu anatoa wito, “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha” (mathayo 11:28)
Je wewe umejitwisha mzigo gani? Je ni mitindo na mavazi ya kidunia, je ni ya mapambo, miziki na maburudisho ya kidunia? Je umejitwisha kiburi, majivuno, dharau, au kupuuzia mambo ya kiroho? Mjumbe wa Mungu anaandika kwa kalamu ya uvuvio akisema “mibaraka ya Mbinguni haiwezi kumfikia mtu anayevunja maagizo ya kweli za milele. Dhambi moja iliyotukuzwa na kutunzwa inatosha kufanya kazi ya kuharibu tabia na kupotosha wengine” {AA 312.1}
Ndio! Tunaweza kuwapotosha wengine, na kuwafanya waukose uzima wa milele kwa kutokuwa waaminifu wa maagizo ya Mungu, wengi wanakosa kuuona uzuri wa mwokozi kwa sababu ya matendo yetu ya giza ambayo hayapatani na Nuru ya Mbinguni.
Paulo pia anazungumza juu ya dhambi zinazotuzinga kwa wepesi, kuna dhambi ambazo kwa sababu tunazitenda mara kwa mara zimetengeneza mazoea sugu (addiction) katika maisha yetu na kitu kibaya Zaidi dhambi hizi hujulikana kwa uwazi kabisa, na hivyo huchafua tabia na sura ya maisha yetu ya Imani kwa wengine, wengi wamenaswa na mazoea ya uzinzi, uongo, utapeli, kukosa uaminifu, wizi wa zaka na sadaka na tamaa mbaya.
Mazoea haya mabaya huchafua akili na kupunguza uwezo wa kufanya maamuzi sahihi na uwezo wa kutofautisha kati ya jema na baya, mazoea haya huleta hali ya uvuguvugu wa kiimani na huyapofua kabisa macho ya kiroho, na ikiwa hatutaamua kwa dhati kuachana nayo, basi shindano litatushinda na tutaipoteza taji ya uzima wa milele,
Inawezekana Kushinda.
Biblia inatupa vielelezo kadhaa vya maisha ya watakatifu na namna walivyoweza kushinda katika shindano hili, sura ya 11 ya kitabu cha waebrania imejaa vielelezo vya mashujaa wa
KUPAJENGA PALIPOBOMOKA NA KUPASIMAMISHA UPYA 2014/2015
TUCASA | Southern Tanzania Union Mission 4
Imani, Paulo mwenyewe alipokaribia kulala usingizi wa mauti roho wa Bwana alimthibitishia ya kwamba amevipiga vyema vita vya Imani na huku akimtukuza Bwana Paulo anaandika “Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda; baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake” (2Tim 4:7-8)
Ni hakika inawezekana kushinda na kuishi maisha yatakayompendeza Mungu na kuwaonyesha wengine uzuri wa mwokozi, nabii Danieli anatuachia kielelezo kingine cha maisha safi, washitaki wake walivyompeleleza kutafuta kosa hawakuona kitu cha kumshitaki kwacho alikuwa mwaminifu na mwadilifu, tena mtu alipendwa sana mbinguni.
Si kwa Nguvu wala Uweza Bali ni kwa Roho.
Hatuwezi kamwe kushinda bila kuutegemea msaada kutoka mbinguni,
Danieli aliweza kwa kuwa roho bora ilikuwa ndani yake (danieli 6:3)
Yufusu alishinda kwasababu Roho wa Mungu alikaa ndani yake (mwanzo 41:38)
Henoko alishinda kwa sababu alitembea na Bwana siku zote (mwanzo 5:22)
Paulo aliweza kwa sababu aliamini anayaweza yote katika Mungu anayemtia nguvu (filipi 4:13)
Na sisi biblia inasema tunaweza kushinda na kumwakilisha Yesu vizuri katika jamii zinazotuzunguka ikiwa “tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu.” (ebra 12:2)
Tazama ukaishi tanzama upate uzima tazama pale kalvari ili ukolewe, sisi ni mabaki ni wateule tuliosalia, watakatifu wa Bwana katika kizazi cha mwisho hivyo tumwakilishe vyema kristo katika maisha yetu, mashahidi ni wengi wanaotuona Tumuombe Mungu aziamshe roho zetu ili tufanye bidii katika kupiga mbio za Imani.
Roho yangu amka sasa, mara jitahidi;
Shindano ni lake Bwana, zawadi ni taji.
Sauti ni yake Mungu inayokuita;
Ndiyo aliyekirimu taji ya uzima.
Mashahidi ndio wengi wanaokuona;
Ya nyuma usifikiri bali mwendo kaza.
Bwana umetuanzisha katika shindano;
Kwa vile tunaposhinda ushindi ni wako.
KUPAJENGA PALIPOBOMOKA NA KUPASIMAMISHA UPYA 2014/2015
TUCASA | Southern Tanzania Union Mission 5
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni