🌴LESONI- ALHAMISI🌴
🌲TAREHE 28/07/2016🌲
🔷KUSIMIKA KANISA🔷
Soma Mathayo 10: 5-10 Kwanini Yesu aliwatuma wanafunzi wake katika miji na vijiji tofauti tofauti bila vitendea kazi?
Linaonekana kuwa jambo gumu sana kwa wanafunzi wa Yesu kupewa maagizo ya kuanza huduma katika maeneo tofauti wakiwa na akiba chache kwaajili yao wenyewe.N I uhakika kwamba Yesu aliwaweka wanafunzi wake katika hali hiyo ili wajifunze kumtegemea Mungu na umuhimu wa kujenga urafiki kupitia hudma kwa wakazi wa maeneo waliopo.Wenyeji wamaeneo haya wangethamini huduma yao kiasi cha kuwasaidia kufanya huduma yao.
Mchungaji Frank alitumwa na konfrensi yake Mahalia kwenda kusimika kanisa katika sehemu ya mji mkubwa ambayo kwa hakika hapa kuwa na Mwadventista hata mmoja. Mwanzoni hakuwa na fedha kabisa kwa ajili ya kazi hiyo.Alitazama ramani na kutafuta mipaka yote ya mji ule na kusoma takwimu ya watu wote katika eneo lile na hali zao.Aliegesha gari lake jirani na eneo lenye biashara nyingi za kila aina,Alianza kutembelea biashara moja baada ya nyingine akiwauliza watu kuhusu hali ya maisha katika eneo lile. Alitembelea maeneo hayo akiongozana na viongozi wa kisiasa,kibiashara na kijamii. Alipata marafiki wenyeji wa eneo lile,ambao walimualika kujumuika pamoja nao katika klabu za kijamii, Katika utaratibu huo aligundua viongozi ambao walikua tayari kumpangishia jengo dogo kando ya jengo kubwa kwaajili ya kanisa Mahalia la Kipresbetarian.Wanachama wa klabu ya kijamii walitoa fedha zao za mbegu,zilizotumika kununulia rangi na vifaa vya kufanyia usafi ili kung’arisha jingo lile kwa ajili ya huduma za kijamii.Mahojiano kati ya viongozi wa kijamii na Mchungaji Frank yalionesha kuwa hutaji la muhimu kwa jamii ile ni suala la afya.Hivyo Mchungaji Frank alitengeneza na kuunganisha timu ya wataalamu wa afya waliojitolea ,walikuja na kuendesha programu mbalimbali na walitozwa bei ndogo sana,jambo lililosaidia kumudu gharama zile. Muda mfupi baadae tawi la Shule ya Sabato lilifunguliwa na baadhi ya wakazi wa eneo lile walihudhuria.
Kwa upesi sana Mchungaji Frank alijifunza kuwa ,Mojawapo ya njia nzuri ya kusimika kanisa ni kwa kuanzisha huduma inayo yafikia mahitaji ya jamii husika,na baada ya hapo pandikiza kanisa kwa kupitia huduma hiyo.Huduma hii inayoihusisha jamii ilizaa waumini wa Waadventista wasabato Zaidi ya 140.Kisa cha Mchungaji Frank,kinaelezea kinachoweza kutokea iwapo tutayafuata mafundisho ya Yesu yakuzifikia jamii,Yesu aliishije kulingana na mafundisho yake ya kuifikia jamii?Juma lijalo tutaanza kuchunguza njia ya huduma ya Yesu,ambayo “itatoa mafanikio ya hakika katika kufikia watu”.Ellen G.White,Ministry of healing,uk.143.
KARIBUNI TUJADILI
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni