🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻☂☂☂☂☂☂☂☂☂☂☂
LESSON
Somo~2. KUREJESHA UPYA UTAWALA. Julai 2-8
☂☂☂☂☂☂☂☂☂☂☂
Soma la Juma.👉🏾 Mwa.1:26-28; Zab. 8:3-8; Mwa.2:15; Rum. 8:20-22; Kut.20:1-17; Rum. 1-25; 2Thesalonike. 3:10.
Fungu la kukariri.➡ '' Mungu akasema, na tumfanye Mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu, wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi'' (Mwanzo 1:26).
✍🏽 Katika anguko wazazi wetu wa kwanza walipoteza zaidi ya sura yao ya mwanzo iliyokuwa katika mfano wa Mungu.
✍🏽 ''Si mwanadamu peke yake bali pia dunia kwa sababu ya dhambi ilikuwa chini ya udhibiti wa yule mwovu, na ilitakiwa kurejeshwa upya kwenye mpangowa wokovu. Wakati wa kuumbwa kwake, Adamu aliwekwa kuwa mtawala dunia yote.
✍🏽 Lakini kwa kushindwa na jaribu, aliwekwa chini ya utawala wa shetani, na mamlaka ile aliyokuwa anaishikilia iliondoka mikononi mwake na kwenda kwa aliyekuwa mtekaji wake. Na kwa njia hiyo, shetani akawa, ''mungu wa dunia hii.''
✍🏽Alikuwa amenyakua mamlaka hiyo ya kuitawala dunia ambayo kwa asili ilikuwa imewekwa mikononi mwa Adamu.
Lakini Kristo, kwa kafara yake aliyoilipia adhabu ya dhambi, si tu kwamba angemkomboa mwanadamu, lakini pia angerejesha mamlaka aliyokuwa amepoteza. Vyote vilivyokuwa vimepotezwa na Adamu wa kwanza vitarejeshwa na Adamu wa pili. '' Ellen G. White, katika jarida la singns of the Times, Novemba 4, 19088.
✍🏽Hakuna swali, baada Anguko, wanadamu walipoteza vingi sana, hivyo ni pamoja na '' MAMLAKA'' ambayo kwa ssili tulikuwa tumepewa.
✍🏽 Mamlaka hii iliyokuwa imepotezwa ni Ipi? Ingawaje dhana ya '' Mamlaka'' siku hizi 8mekuwa na tafasiri hasi, kwa hakika haikuwa hivyo katika Bustani ya Edeni. Ilikuwa inamaanisha nini kwa mara ya kwanza wanadamubwalipopewa mamlaka ya kuitawala dunia? Na kanisa litafanya nini ili kuwasaidia watu kuvirejesha baadhi ya vitu vilivyopotea baada ya msiba wa Anguko la wazazi wetu wa kwanza pale Edeni?
Mwisho.
Soma somo la juma hili ukijiandaa kwa ajili ya Sabato ya Julai 9.
🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻🌻☂☂☂☂☂☂☂☂☂☂☂. Karibuni kwa michango yenu Waumishi wa Bwana.
🙏🏾🙏🏾🙏🏾🙏🏾🙏🏾🙏🏾🙏🏾🙏🏾🙏🏾🙏🏾🙏🏾.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni