Alhamisi, 7 Julai 2016

Kupajenga palipobomoka sehemu ya tatu

Ni mwendelezo wa somo la kupajenga palipobomoka, usisite kutoa maoni yako kupitia sehemu ya maoni hapo chini au wasiliana kwa 0712672894

3. EFFORT NDEFU KULIKO ZOTE
Limeandaliwa na Rwabuhanga Werema M/kiti-Tucasa ETC
 
“Na yakuwa tangu utotoni umeyajua maandiko matakatifu,ambayo yaweza kukuhekimisha hata upate wokovu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu .” 2 Timotheo 3:15.

Jitihada za dhati za wale ambao tayari walishaipokea nuru ya Yesu Kristo na kwa nia ya dhati wakawa na msukumo ndani ya mioyo yao unaowataka kutenda nao wakatii na kuwaelekeza wanadamu wasiomwamini Yesu na kutii kwa uaminifu amri zake, ya kwamba wamwamini na kuziacha njia zao mbaya na wajiandae kwa siku ile iliyo kuu yenye kutisha. Kwa namna hii tunasema juhudi na jitihada hizo ni effort. Mcheni Mungu na kumtukuza kwa maana saa ya hukumu yake imekuja msujudieni yeye aliyeziumba mbingu na nchi na bahari na chemichemi za maji Ufunuo 14:7
Nuhu ni mmoja wa watu wa Mungu wanaoshuhudiwa na biblia kuwa walifanya effort kwa mda mrefu sana. Ni ukweli usiopingika hata kidogo kwamba waadventista tuna nuru kubwa ajabu yenye uwezo wa kulifukuza giza upesi.
Maisha yetu katika jamii inayotuzunguka ni effort ya pekee sana na ndefu kuliko zote katika kizazi hiki. Tangu tulipoongoka hadi sasa maisha yetu, matendo yetu na mwenendo na mzungumzo yetu ni effort nzuri yenye uwezo wa kuwaleta watu wengi sana toka gizani na kuja kwa Yesu. Hebu nijiulize swali hili; tangu nilipoongoka hadi leo hii wangapi kupitia maisha yangu wamemuona huyu Yesu tunayemtaja kila siku,waliobatizwa ni wangapi, wangapi wamebarikiwa na namna wanavyo akisiwa na ile nuru njema toka kwa Yesu ? Effort ngapi nimezifanya kupitia maisha yangu zanye nia madhubuti ya kulitukanisha jina la huyu Yesu tunayejiita kwamba nasi tu wafuasi wake!
Tujifunze mfano toka kwa viumbe vya asili. Maua yana maisha mafupi sana lakini huwavuta watu wa kila namna. Utayakuta maua kwenye meza za wafalme, kwenye ofisi za wenye mamlaka na katika sehemu zote zenye kuheshimiwa. Macho ya watu hayachoki kuyaona maua. Huwavutia hata wadudu kwa aina zao, vipepeo, nyuki n.k. Wengi hupenda kupiga picha katika mazingira yenye maua. Hii ni kwa sababu ya mvuto,harufu na mg‟oro mzuri wa maua. Mfalme Sulemani ambaye hajawahi kutokea tena mfalme yeyote kama yeye hata leo, katika maisha yake yote hakuwahi kuvikwa uzuri wa kupendeza unaozidi maua Mathayo 6:29 .Jambo la ajabu ni kuwa pamoja na uzuri wote na tabia nzuri maua hayana maisha marefu kama yangu na yako.
Kama ningekuwa na tabia nzuri kama maua na uwezo wa kutumia vizuri talanta nilizopewa na Mungu , tangu nilipoongoka ningekuwa nimewaleta wangapi kwa Yesu? Matendo yangu nananukiaje chuoni kwangu, yanaukiaje kanisani kwangu, darasani kwangu yanaukiaje, nyumbani na kwa jamii inayonizunguka yanaukiaje? Je, ninatofauti gani na bomba la maji taka lililotoboka na kuchuruzisha uozo na harufu mbaya mahali ambapo sio haikutarajiwa iwe hivyo na sasa hakuna anayetamani kuwa mahala hapo. Hakuna anayetamani kuwa karibu na mimi,wewe kwa mda merefu, mara ngapi waadventista tumeitwa wanafiki! Mjumbe wa Mungu Elen White anasema“ Tuna haja ya kuwafikia watu, iwe ni shauku yetu kuhakikisha kwamba
KUPAJENGA PALIPOBOMOKA NA KUPASIMAMISHA UPYA 2014/2015
TUCASA | Southern Tanzania Union Mission 10
wadhambi wajutie dhambi zao na watubu kabla ya muda wao wa kuokolewa haujaisha na mwisho wakawa katika kuomboleza wakisema „wakati wa mavuno umepita wakati wa hari nao umepita wala sisi hatukuokoka. ” 1Testmonies for the Church pp 51.
Maisha yangu na na yako ni effort nzuri na yenye mda wa kutosha. Kama tukikubali kufanya matengenezo na kubadilika maisha yetu yataipindua jamii tunayioshi juu chini. Tutashuhudia matokeo chanya yatakayoletwa na Roho mtakatifu. Maandiko matakatifu yanashuhudia kuwa tangu utoto wako (kuongoka kwako) umeyafahamu maandiko ambayo yanaweza kukuhekimisha katika Kristo Yesu. Mpendwa katika Kristo tumepewa agizo la kuwafanya mataifa yote kuwa wanafunzi, ni ole wangu na wako kama tusipotii agizo hilo. Mpenzi, Mungu akutie nguvu, upate badiliko litakaloleta matokeo chanya kwa Kristo na mwisho wa safari yetu mbingu zitushuhudie Mungu wetu akituambia “vema mtumwa mema ulikuwa mwaminifu kwa machache ingia katika furaha yangu.

SOMO HILI LINAENDELEA.................

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni