Ni mwendelezo wa somo la kupajenga
palipobomoka, usisite kutoa maoni yako kupitia sehemu ya maoni hapo
chini kwa masiliano zaidi piga simu 0712672894
Limeandaliwa na Lazaro K. Erick, Mkuu wa Mawasiliano TUCASA-STUM
FUNGU KUU: YEREMIA 1: 18-19
WIMBO NO: 127Je unafahamu maisha yetu kuwa mazuri sio tu kwa kupata elimu ya dunia hii? Mungu ana njia maelufu ya kufanya mtu afanikiwe katika maisha ya duniani, Pia tunatakiwa kujua kuwa imetupasa kwanza kuutafuta ufalme wa Mungu na haki yake na haya mengine ya duniani ni zawadi tu toka kwa Mungu.
Ni kweli tunatakiwa kutafuta elimu ya kidunia kwani pia inatupa mwangaza wa maisha lakini pia tunatakiwa kujua kuwa pamoja na elimu ya kidunia tunayoipata inatakiwa kutuweka karibu na msalaba wa Yesu.
Daniel 3, Katika kitabu hiki ch Daniel sura ya tatu inatuonesha vijana watatu yaani Shadraka, Meshaki na Abednego walivyo jitoa kumsimamia Mungu katika nchi ya Ugenini, na hii ni baada ya kujaribiwa kutii kitu amacho kipo nje ya Maagizo ya Mungu. Moja kati ya amri za Mungu ni pamoja na kutaa kujifanyia sanamu za kuchonga na kuvisujudia kama tusomavyo katika Kutoka 20:4-5.
Vijana hawa walisimama kumtetea Mungu na hata bila kuogopa vitisho mbalimbali na vifo bali waliamua kuutangazia umati wa watu kuwa Mungu pekee ndie anayetakiwa kuabudiwa, Lakini mwisho wa yote vijana hao watatu walimuinua Mungu na Mungu naye akaja kuwainua na mpaka wakawa ni watu wenye maisha mazuri na watu wenye hekima kuu na kutegemewa sio nchini Babeli tu hadi hivi leo tunazisoma habari zao na zinatweka karbu na Mungu.
Ni kweli wana TUCASA imani yetu imekuwa ikipoa sana hasa tunapokuwa chuoni na kw bahati mbaya ikatokea mitihani imepagwa siku ya sabato hii ni sababu kubwa inayotufanya baadhi ya wasabato wengi hata wakiwa chuo hawataki kujulikana kuwa ni wasabato ili waendelee kuikanyaga amri ya kuiheshimu siku ya sabato.
Pia wengine japo tumekuwa ni wana TUCASA yaani wana chama kamili tumekuwa pia tukiendelea kufanya mitihan siku ya sabato au kusoma siku ya jumamosi hasa tunapokuwa tunakabiliana na mitihani, Hali tukijua kuwa Mungu wetu anaona yote ya wazi nay a sirini pia.
Ndugu mpedwa kumbuka hii ni dhambi ya wazi na inawezekana tumewafanya wengi wasio wasabato kushidwa kukata shauri ya kuungana na kanisa la Mungu kwa kuwa wamekuwa wakituona tukishiriki nao katika kuikanyaga amri hii kuu.
KUPAJENGA PALIPOBOMOKA NA KUPASIMAMISHA UPYA 2014/2015
TUCASA | Southern Tanzania Union Mission 20
ZINGATIA YAFUATAYO
1. Sio kwamba hao watu wanapotangaza kufanya mitihani siku ya sabato hawajui kuwa ni kinyume na mapenzi ya Mungu, jibu ni kwamba walio wengi wanatambua napengine wanafanya hivyo ili kujua imani zetu kuwa ni dhabiti au sio dhabiti mbele za Mungu
2. Lakin pia tujue kuwa hakuna aliye amua kumsimamia Mungu na kumtetea Mungu akamuacha, tuna ushahidi wa watu wengi waliofukuzwa chuo kwa sababu ya kusimamia ukweli wa biblia na bado wapo na wakiwa na maisha mazuri tu.
YEREMIA 1: 18-19
Hili ni tumaini kubwa kwetu na la faraja ya kuwa pamoja tunakutana na chanamoto za dunia hii,Mungu wetu ni wa huruma na upendo yeye anayetuwekea ulinzi wake mkubwa sisi tulio wadhambi , je vipi sasa tutapoamua kumtetea yeye ni hakika ataturinda daima na kututunza. Na hivyo watapigana nasi lakini hawatawezi maana yupo nasi ili atuoko.
TAFAKARI FUPI:
Inawezekana tumekuwa mbali na uso wa Mungu kwa ajili ya dhambi mbalimbali tunazozitenda za wazi na za siri , pia inawezekana tumeuwa msitar wa mbele kumuaibisha Mungu wetu katika swala la utunzaji wa sabato kwa kufanya mitihani mbalimbali na kuudhuria vipindi mbalimbali vya masomo, lakini Mungu amekuwa akituhurumia na kuendelea kutupakila kitu kinachostahiri kwetu, lakini ni Muda sasa wa kumwambia Munguya kuwa “NARUDI NYUMBANI ” wimbo no. 118 , tukiwa tunatafakari
Tunaendelea kuwaletea masomo mengine katika mpangilio wake, karibuni sana tunawategemea sana na Mungu awabariki sana!!!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni