Alhamisi, 7 Julai 2016

Kupajenga palipobomoka sehemu ya pili.

Ni mwendelezo wa Masomo ya kupajenga palipobomoka, kama kuna maswali usisite kuwasiliana nami kupitie nafasi ya maoni hapo chini au kupitia namba hizi 0712656298 na 0712672894.
hakimiliki Tucasa stum 2014/2015
 
2. MWANA-TUCASA NENO NA MAOMBI BINAFSI
Limeandaliwa na Frank Mwita Edward, Katibu msaidizi TUCASA-STUM
(Hebu waalike washiriki kusali sala ya Baba yetu kabla na baada ya kuanza somo hili)
Maombi ni kitendo cha kufungua moyo kwa Mungu kama rafiki. Si kwa kuufanya ufahamike kwa Mungu kwamba ukoje la! Bali ni kwa ajili yetu kuwa tayali kumpokea. Maombi hayamshushi Mungu chini baali hutuinua sisi juu mbinguni.
Maombi ni mukondo wa mawasiliano kati ya nafsi zetu na Mungu. Mungu anasema nasi kupitia neno lake takatifu [Biblia] nasi huitikia kwa njia ya maombi, yatupasa kujifuza nguvu ya maombi. Mungu yupo tayali kusikiliza na kujibu maombi ya kicho bila kujali hali zetu. Kwa maana yeye ni Baba wa upendo „‟1Yh 4:16…Mungu ni upendo, naye akaaye katika pendo, hukaa ndani ya Mungu…‟‟.
Kristo alipokuwa hapa duniani aliwafundisha wanafunzi wake kwa kipindi hicho namna ya kusali na sisi kama wanafunzi wake wa kipindi hiki yatupasa kusali hivyo soma Mt 6:9-13. Sala hii ndiyo inapaswa kuwa kanuni ya sala zetu zote, lakini cha kushangaza sala hii imekuwa ikinukuliwa bila tafakuri tena kwa kufukuzana ni nani atakaeimaliza mapema kuisoma huku aliepewa kuomba kama mtangulizi ameomba ombi refu sana ndipo humalizia kwa kusema „‟Nanyi mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke, kama watu wa mataifa…‟‟ Bali salini hivi, sasa anaachia mashindano. Swali ambalo nimekuwa nikijiuliza mbali na mwendokasi huu ni kwamba je tunazingatia sala hii sawa na hitaji la Yesu alivyo tuachia kama kielelezo cha sala zetu zote?
Leo ningependa kukualika tujifuze sala hii kwa mapana yake.
Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Hapana baba mwingine wala jina lingine lifaalo kutukuzwa katika maisha yako isipokuwa Baba wa mbinguni [MUNGU] Kut 20:1-3, na utalitukuza pale tu utakapokaa ndani yake nae ukamruhusu ndani yako siku zote za maisha yako tena ataonekana katika maisha yako halisi ya kila siku Yh 15:4 popote utaenda nae, uingiapo na kutoka.
KUPAJENGA PALIPOBOMOKA NA KUPASIMAMISHA UPYA 2014/2015
TUCASA | Southern Tanzania Union Mission 6
Ufalme wako uje, Ufalme wa Mungu hautakuja kamwe hadi neno lake limehubiriwa kwanza Mt 28:19, Mdo 1:8, 1Pet 2:9-10. Jiulize wewe ndani ya kanisa la Mungu umeshiriki kiasi gani katika kutimiza wito huu wa Kristo ulimwenguni wa kuwaeleza wengine tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu? Kama bado ni wakati wako sasa kutekeleza sawa na sala hii.
Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni, Ni mara ngapi umetaja maneno haya lakini tayali una msitakabali wa ombi lako? Na pengine unayasema ili kukamirisha ombi lakini humaanishi mapenzi ya Bwana kutimizwa, bali mapenzi yako kutimizwa? [Mwombaji] jifunze katika ombi la kiwete huyu mwenye umri wa miaka arobaini [kama ni kiwete kutoka tumboni mwa mama yake, inamaana amehangaika kwa muda wa miaka 40 akitafuta uponyaji] kwa watumishi wa Mungu na majibu ya ombi lake (Ellen G. White-The Act of the Apostles chpt6,ppg57) Mdo 3:1-8 ambaye hapo awali alitazamia kupata sadaka lakini sasa anasikia sauti ikisema mimi sina fedha wala dhahabu, binafsi ninaona kama kiwete huyu, maana hakutajwa jina lake kama vile anaishiwa nguvu za kuwaangalia lakini hakukata tama kuwatazama huku akijiuliza hili ndilo jibu la ombi langu kweli! Lakini kwa subira, maana hakuchoka kuwaangalia yeye alingoja hatima ya Petro na Yohana kwa mikono aliyokwisha kunyoosha, ndipo sauti ya matumini inasikika ikisema nilicho nacho ndicho nikupacho, nadhani hakuamini kama baada ya maneno yale ya awali tena ya kuchosha, maneno mazuri kama haya yangesikika kwake, mpendwa katikati ya kukata tama ya majibu ya maombi yako, wewe usishushe mikono kama huyu muombaji tena usichoke kumuangalia Bwana na usigeuze macho yako kwingineko, na ukiomba kuwa tayali kupokea lolote lililo bora machoni pa Mungu kwa moyo wa shukurani.
Utupe leo riziki yetu, Siku zote tambuya yakwamba Mungu ndiye mpaji wa yote, anaye tupatia mahitaji yetu yote, hivyo vitu vyote ulivyonavyo ni mali ya Bwana, Mt 7:11, Zab 24:1, Mhu 5:20, 6:2, 2Nya 1:12. Unapotambua kuwa Bwana ndiye mtoaji hivyo imekupasa kukiri kwa kumrudishia sehemu ya kumi ya pato lako halali Ml 3:10. Kama sala hii uliitaja hapo awali bila ya kutambua hili ni wakati wako sasa wa kujenga palipobomoka.
Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu, [soma Mt 6:14-15… msipowasamehe watu wengine makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu] katika hilo fungu, na hapa ndipo wengi tunapokosea katika kuomba. Mara nyingi tumekuwa na mafundo ya chuki tena yumkini katikati ya jamii ya waminio lakini hatuchoki katika kunukuu
KUPAJENGA PALIPOBOMOKA NA KUPASIMAMISHA UPYA 2014/2015
TUCASA | Southern Tanzania Union Mission 7
sala hii, lakini Yesu anasema soma Mt 5:23,24. Muda mwingi mpendwa unaoutumia kujiuliza kwa nini mimi kwa nini Mungu hajibu maombi yangu jiulize kwa nafsi yako ni wangapi na mara ngapi umekataa kusamehee? Pengine yupo mtu fulani hutaki hata kusikia jina lake likitajwa mbele yako kutokana na magumu aliyokutendea tena mtu huyu hata akipewa kuhudumu hutaki kusikiliza na akiomba badala ya mwishoni kusema AMINA wewe husema AMUNA [HAPANA]. Na sasa umelisusia kanisa ukidhani umemususia fulani kumbe unasususia mwenye kanisa [KRISTO YESU] pengine hujaona madhara yake kwani husema moyoni mbona ninafanikiwa na mibaraka inaambatana na mimi? [Soma Mt 5:45 Yeye huwaangazia jua lake watu waovu na watu wema, naye huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki]. Na wewe uliekosa kumbuka ukatubu ili tumwendee Bwana kwa ujasiri kwani tumekwiisha kupatina ni bora zaidi, na hii ndio injili.
Na usitutie majabuni, lakini utuokoe na Yule mwovu [Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina] Yafaa kukili unyonge wetu mbele za Bwana na kumruhusu kutuongoza katika ushindi maana yeye ana nguvu za kumshinda yule muovu tangu zamani, Hebu fikiri ni kwa nini mara nyingi pengine umedumu katika dhambi fulani kwa muda mrefu si kwamba unapenda ila pengine ni kwa sababu ya kujifariji binafsi kuwa nilikosea sehemu fulani sasa sitarudia lakini unajikuta tena na tena unaanguka Efe 6:11.
Hivyo kwa kuwa vita yetu si ya damu na nyama hata mtu akapige pushapu na kujaza kifua ili kushinda au kwa ujanja wa maneno la! Efe 6:12, Yesu hatakuja kukushika mkono kwa namna ya kimwili kukutoa katika genge la watumia vileo au dimbwi la uzinzi, uasherati au useng‟enyaji au katika mengine mengi ya namna hiyo la! Bali Yesu anahitaji kuujenga utu wako wa ndani juu ya imani yako kwa Bwana, hii haipatikani popote bali ni kwa njia ya maombi na kulisoma neno la Mungu, soma Efe 6:18 Kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuaombea watakatifu wote.
Na katika kuomba lipo Jina tulilopewa ya kwamba tukiomba kwalo hilo nae Yesu atajibu Yh 14:13
Flp 4:6 …bali katika kila jambo kwa kuomba…., haja zenu na zijulikane na Mungu.
Mpendwa katika kipindi hiki kigumu tunachopitia ambacho tunaishi wakati ulimwengu umeharibika kwa nyanja zote kiuchumi na kimaadili tutasalimika kwa njia ya kusoma neno
KUPAJENGA PALIPOBOMOKA NA KUPASIMAMISHA UPYA 2014/2015
TUCASA | Southern Tanzania Union Mission 8
[Biblia] na maombi tu, na hapana ujanja mwingine, kipindi ambacho shetani anatumia mbinu na nguvu zake zote kuhakikisha amewateka wote waliitiao jina la KRISTO YESU, wakati mugumu kama huu ulimtokea Yesu akijua haya yote ndipo alipowachukuwa wanafunzi wake katika kuomba, hapo ndipo alipopata nguvu ya ushindi
Mungu yupo tayali kutenda kama tukimuomba kwa kicho bila waa [soma Mk 11:24 Kwa sababu hiyo nawaambia, yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mmeyapokea nayo yatakuwa yenu]. Tunakubali kwamba tunaitaji kumwagwa kwa Roho Mtakatifu katika kipindi hiki cha miisho ya dunia lakini hii itawezekana tu kwa kusoma neno la Mungu na maombi ya binafsi na yale ya makutano. Watu wa Mungu wakiomba kwa moyo safi, dhamiri njema na imani ya kweli maombi ya binafsi na yale ya pamoja ni hakika mambo makubwa yatatokea kama majibu ya maombi yao. Mt 26:36-44
Nakusihi mpendwa kwa huruma za Kristo Yesu usiwe mtu wa kupitwa na masomo mengi bila kujali, panga wiki hii uzibe nyufa zote hali kwamba zisipelekee kuanguka mpaka chini.
Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, na pendo la Mungu Baba, na ushirika wa Roho Mtakatifu ukae nanyi nyote.
Somo hili limeandaliwa na mtumishi wenu niliye mdogo kuliko yeye aliye mdogo wa watakatifu wote niliye pewa neema hii ya kuwaandikia haya ili tufahamishane jinsi itupasavyo kumwendea Bwana kwa jinsi ya maombi huku tukilisoma sana neno takatifu [Biblia] ili kufahamu siri ya ufalme wa mbingu.

Somo hili linaendelea......

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni