Somo; UTUNZAJI WA DUNIA
"Bwana Mungu akamtwaa huyo mtu, akamweka katika bustani ya Edeni, ailime na kuitunza." (Mwanzo 2:15). Ni kanuni zipi, kama zipo, tunazoweza kuchukua katika aya hii ambazo zitaathiri namna tunavyohusiana na sayari yetu kwa vigezo vya kuitunza?
Kabla ya dhambi, Adamu na Hawa walikuwa wamefanywa kuwa mawakili juu ya vyote ambavyo Mungu alikuwa amewakabidhi. Walikuwa wamepewa uwezo kamili juu ya maisha ya mimea na wanyama. Baada ya dhambi, hata hivyo, viumbe vyote vya asili vilionekana kuasi dhidi yao kwa kiwango kile kile walichokuwa wameasi dhidi ya Mungu. Wanadamu wakaanza kujiona kutokuwa na uwezo mbele ya vitu vya asili ( kama vile hali ya hewa, kilimo na jamii ya wanyama.)
" Miongoni mwa wanyama wengine wakawaida, Adamu alikuwa amesimama kama mfalme, lakin kama angebakia kuwa mwaminifu kwa Mungu, viumbe vyote vya asili vingeendelea kuutambua utawala wake; bali alipoasi, mamlaka haya yalipotea. Roho ya uasi aliyokuwa ameiruhusu mwenyewe kuingia ilisambaa pia kwa wanyama wengine. Kwa namna hiyo, sio tu maisha ya mwanadamu, yaliyokuwa yanasimulia kisa cha huzuni cha somo la ujuzi wa uovu, Bali pia hali ya asili ya wanyama, miti ya misituni, nyasi za uwandani, na hata hewa yenyewe aliyokuwa anavuta, vyote vilisimulia somo la kuhuzunisha la ujuzi Wa mabaya." Ellen G. White, Education, uk. 26,27.
Mpaka sasa, bado tunasumbuliwa na kuteketezwa na majanga ya asili pamoja na mfumo wa ekolojia unaochakaa kila leo, yumkini katika baadhi ya maeneo duniani. Na kwa hiyo, tunatumia juhudi nyingi za kutumia teknolojia na maendeleo ya viwanda kujihami. Hata hivyo, ingawa teknolojia na maendeleo ya viwanda yanaweza kutusaidia kujikinga, wakati mwingine teknolojia hiyo hiyo inaweza kuiharibu sayari yetu. Ekolojia ni suala mtambuko linalohusika kimafundisho, kimaadili, na kiteolojia, hasa pale ambapo matumizi ya rasilimali zilizomo duniani kunaweza kuwaweka watu wengine kwenye hali ngumu kupindukia.
"Waadventista Wa sabato hutetea mtindo Wa maisha ulio sahili na wenye kuleta siha kamili, mahali ambapo watu hawarukii kwenye gurudumu LA kuendesha mashine isiyodhibitiwa ya ufujaji, kunipatia vitu na uzalishaji Wa taka. Tunawataka watu waheshimu viumbe vya Mungu, kujizuia katika matumizi ya rasilimali zilizomo duniani, kutathmini upya mahitaji ya kila mmoja wetu, na kutilia mkazo kuheshimu viumbe wengine."- kutoka katika "Official Statement of the Seventh - day Adventist Church on Environment, [Tamko Rasmi la kabisa la Waadventista Wa Sabato kuhusu mazingira]" 1995.
Tunafikiaje mapatano ya haki katika mtazamo wetu juu ya dunia: kuwa mawakili wema Wa makao tuliyopewa na wakati huo huo tukijiepusha na hatari ya kuifanya dunia na mazingira kuwa miungu tunayoiabudu? Warumi 1:25 hapa ina onyo gani kwetu?
➖➖➖➖➖➖➖➖➖
MWISHO WA NUKUU
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni